Kama kweli sisi ni wacha Mungu, tufute hii Mada Shuleni!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Tuache unafiki kama kweli sisi ni wacha Mungu na tunaamini Mungu yupo, basi tuache kuwafundisha watoto wetu Darwin's evolution, tufute hii Mada, kinyume na hapo ni unafiki tu na kukesha Kanisani na Msikitini hakumaanishi chochote kama haumuamini Mungu na uumbaji wake, ...
 
Mambo ya kaisari mpe kaisari na mambo ya Mungu mpe Mungu.
Unacholalamikia nn? Ww mwafrika kwa akili zako ulikubali kupokea dini na Elimu ya kikoloni.
Kufuta au kuedit haiwezekani. Hii ni sawa na viongozi wa nchi kwenda kutibiwa nchi za nje.
Nafikiri umenielewa mfagia jengo wa chama cha makinikia(CCM)
 
Wengine physics ilitupiga chenga hebu tufafanulie maana ya iyo theory kwanza ili tupambanue km hoja yako inamashiko
 
Ma~ccem majinga sana!!!kwa mada za kijingajinga ndio yenyewe
 
Wengine physics ilitupiga chenga hebu tufafanulie maana ya iyo theory kwanza ili tupambanue km hoja yako inamashiko


Siyo Fizikia bali ni Sayansi ya Viumbe (Bailojia) kwa kifupi inasema kwamba hakuna kitu kama Mungu Dunia hii na kila kitu kilichopo hp Duniani pmj Duniani hatujaumbwa na Mungu bali ni nature!
 
Iyooo ni theory mzeeeee
No one prove it right so unawezaaa itemaaa you don't need to go that far from ure thinking capacity ##mchezo huu haujawah mwacha mtu Salama
 
Ni wapi nimeongelea Dunia yote? Nimeongelea Tanzania!
Hakuna popote ulipoongelea Tanzania Mkuu.

Aliyekuuliza swali ilibidi umjibu swali na si kumkimbia.Duniani si sote tunaoamini katika Mungu.Hivyo wanafunzi kufundishwa theories mbalimbali zinazoenda kinyume na Imani yako usione kesi saana (Just cool down and argue it Logically, not emotionally).

Pia unapozungumzia Dini kama source ya Uamini wa Mungu unakosea na tujifunze kuelewa na si kukariri.Msingi wa Imani yeyote si Uislamu na Ukristo.

Kuku pia ana Imani, ndiyo maana ikifika saa kumi na mbili imani yake inamtuma kwenda kwenye banda lake na saa kumi na mbili alfajiri kuamka.Nina mtu, jirani yangu hapa ambaye kuku wakimwona wanamkimbia, Je hii si imani kwa kuku?.

Kabla ya hizi dini (Uislamu, Uhindu, Uyahudi, Ukristu nk) watu walikuwa wanaamini katika Mungu, tena zaidi ya sasa ya Imani ya ki-abra kadabra.Kwahiyo unapozungumzia Uamini wa Mungu usiwe-biased tu katika Dini, ingia deep sana (Kabla na baada ya ujio wa Dini).
 
Siyo Fizikia bali ni Sayansi ya Viumbe (Bailojia) kwa kifupi inasema kwamba hakuna kitu kama Mungu Dunia hii na kila kitu kilichopo hp Duniani pmj Duniani hatujaumbwa na Mungu bali ni nature!
Naomba nikuulize swali Mkuu.

Mungu kwako ni kitu gani?.Sihitaji jibu la hovyo (kumradhi), naomba unijibu kwa kutumia Mantiki na si hisia wala ushabiki.

Nb;Jibu utakalonipa uwe na ushahidi nao, Logically.Si haditi wala ngano.
 
Unajua maana ya "theory" kwenye sayansi?kwanza theory ya Creation kuendelea kufundishwa ndio makosa maana haina evidence zozote
Creation theory ipigwe chini iekwe Big Bang theory
 
Tuache unafiki kama kweli sisi ni wacha Mungu na tunaamini Mungu yupo, basi tuache kuwafundisha watoto wetu Darwin's evolution, tufute hii Mada, kinyume na hapo ni unafiki tu na kukesha Kanisani na Msikitini hakumaanishi chochote kama haumuamini Mungu na uumbaji wake, ...
Elimu ya mkoloni. Dini ya mkoloni. Mwafrika hata haelewi ni kwa nini aliletewa hivi vitu na leo anataka afanye jambo ambalo hata waliomletea hawafanyi. Ngozi nyeusi hii ni balaa!

Kule jimbo la Texas nchini Marekani baadhi ya wilaya (counties), kama siyo jimbo zima, wamebadilisha syllabus na Evolution na Creation vinafundishwa vyote kwa pamoja na mwanafunzi anaamua mwenyewe cha kuamini.
Kimsingi sayansi na dini havikinzani bali vinakamilishana. Kuna vitu sayansi haiwezi kueleza na kuna vitu dini haiwezi kueleza. Evolution (ambayo ni nadharia tu) kuna vitu ambavyo inaweza kuvielezea vizuri zaidi kuliko dini and vice versa...

By the way Jamhuri ya Muungano wa Tanzania HAINA DINI. Sasa utafuta syllabus katika misingi ipi? Kuna nchi yo yote inayofanya hivyo? Hata huko Uarabuni kwenye Islamic states, syllabus zao katika secular schools zikoje?
 
Back
Top Bottom