Kama kweli simu za Mnyika na Lissu ziliingiliwa ni Kosa la Jinai: POLISI

Teh..teh..teh..Sidhani kama hilo lawezekana. Hata kama kungekuwa na ukweli wake DHAIFU hawezi kutoa Viza kwa hao waingereza. Atoe viza ili aumbuke.....ooohh please.
 
Nilipata kusikia (sina uhakika kama ni kweli)kuwa Scotland Yard waweza kuwakodi kufanya upelelezi juu ya jambo fulani kwa gharama zako. Jee hii ni kweli? kama ni kweli Chadema wawaite na sisi tuchangie gharama kama tunavyochangia M4C ili kuwaumbua hawa wenye mbinu za kigaida na wananchi wajue ukweli wa nini kinafanywa na CCM.

Teh..teh..teh..Sidhani kama hilo lawezekana. Hata kama kungekuwa na ukweli wake DHAIFU hawezi kutoa Viza kwa hao waingereza. Atoe viza ili aumbuke.....ooohh please.
 
Jeshi la polisi na intelijensia watupe kwanza report ya zile sms zilizosambazwa kipindi cha uchaguzi mkuu 2010 zikitukana dr. Slaa na cdm. Siku hizi watz hatusahau.namba zile ilionekana ni za nje ya nchi lakini waliotuma walikuwa hapa nchini.
 
J
Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza ni kwa nini kumekuwapo na uundaji wa kamati nyingi za uchunguzi wa matukio yanayojitokea pasipokuwa na mrejesho wake kwa jamii, Senso alisema matukio ya uchunguzi hufanywa pole pole ili kutoa majibu ya uhakika.

Aliwataka wananchi kuwa na imani ya Jeshi la Polisi, kwani limejipanga kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kuliongoza, licha ya kuwapo na kasoro ndogondogo.

Source:Mtanzania
Hapo kwenye Red imeniacha hoi!!! kwahiyo hiyo polepole ndio haina Mwisho? kama ndio utaratibu wa Polisi ndio huu nimegundua kwanini kesi zinachelewa sana kuisha kwa sababu ya utaratibu wao unawaruhusu kuwa wazembe... na kwa mmtaji huo wamekuwa wadhaifu kamili... kwani hata akianza uchunguzi na akachoka atauacha na akiulizwa atakuambia tunaendelea ila utachukua muda mrefu ili kupata majibu ya uhakika... sometime wanazembea hadi watuhumiwa hufa...

Kwa hili la SMS litachukuliwa polepole na wananchi muendelee kusubiria hadi umri wenu wa kustaafu ufike miaka 55 au 60 mkipata mafao yenu na majibu ya uchunguzi yatakuwa yashapatikana... Movie lingine hili limeongezeka kama bollywood vile halijaisha hili limeanza lingine
 
JESHI la Polisi nchini, limesema linaendesha uchunguzi wa madai yaliyotolewa hivi karibuni na Wakili Mwandamizi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando, kuwa kuna mtambo wa kunasa mawasiliano ya simu za mikononi umeingizwa nchini kinyemela.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Msemaji jeshi hilo, Advera Senso, alisema baada ya madai hayo kutolewa wiki iliyopita, jeshi hilo, kupitia Kitengo cha Simu na Ufuatiliaji, limeanza kazi ya kuchunguza ukweli wa mashine hiyo na kama kweli kuna aliyefanya kitendo hicho hatua kali sana zitachukuliwa.

“Taarifa za kuwapo na mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu ya mtu mwingine zimetufikia, tunachunguza kwa ukaribu, tunajua suala hili lilianzia bungeni na sasa lipo ndani ya jamii.

“Kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine bila ridhaa yake ni kosa la jinai, sasa tusianze kuhukumu kitu ambacho hatuna uhakika nacho, tusubiri kazi ya uchunguzi ikamilike,” alisema Senso.

Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza ni kwa nini kumekuwapo na uundaji wa kamati nyingi za uchunguzi wa matukio yanayojitokea pasipokuwa na mrejesho wake kwa jamii, Senso alisema matukio ya uchunguzi hufanywa pole pole ili kutoa majibu ya uhakika.

Aliwataka wananchi kuwa na imani ya Jeshi la Polisi, kwani limejipanga kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kuliongoza, licha ya kuwapo na kasoro ndogondogo.

Source:Mtanzania
kama kawida, nchi ya matukio.

Sasa hawa akina Mwigulu na Nape lao linasahauliwa na mambo yote yanahamia kwenye issues za kamati za umeme na nishati. Kiuhalisia lilikuwa ni kosa kubwa sana.

Back
Top Bottom