Kama kweli Serikali hii inatengeneza pato kubwa kuliko Serikali zilizopita, mbona haitoi ajira za walimu na watumishi wa afya kama serikali zilizopita

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
2,919
3,047
Ukweli ni kwamba kabla ya awamu ya tano haijaingia madarakani, ajira za walimu na watumishi wa afya zilikuwa ni za kila mwaka, na kama sikosei, wahitimu wote walikuwa wanapata ajira.

Baada tu ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani, kumekuwa hakuna ajira za uhakika kwa wahitimu wote wa kada hizi(na zingine), kwa visingizio vingi, vya kwanza vilikuwa ni "UHAKIKI WA WATUMISHI' na kingine ni " KUJENGA UCHUMI KWANZA(2016)".

Ukweli uhakiki ukaisha na uchumi ukaimarika na sasa tupo kwenye "UCHUMI WA KATI".

Swali la msingi ni je, kwa nini sasa Serikali hii iliyo imara kiuchumi kuliko serikali zilizopita inasuasua kutoa ajira za walimu na watumishi wa afya?
 
Kuna kitu ambacho sikielewi, kuna kundi kubwa la walimu halina ajira, halafu kuna kundi kubwa la waliomaliza la saba hawana nafasi secondary, si mwenge tu madarasa?
 
kwa iyo indicator ya pato kuwa juu mpaka walimu waajiliwe?? VP wanasheria, mifugo, uvuvi, wachumi, mainjinia, waandish wa habari, utalii, mambo ya masoko, polisi, jeshi, etc...
Jamaa mbinafsi sana.. hizo kazi ndio ana maslahi nazo
 
kwa iyo indicator ya pato kuwa juu mpaka walimu waajiliwe?? VP wanasheria, mifugo, uvuvi, wachumi, mainjinia, waandishi wa habari, utalii, mambo ya masoko, polisi, jeshi, etc...
Hao ni watu walio kwenye vipau mbele vya nchi,na wengine pia.Na hebu jibu hoja,kwa nini siku hizi watu hawaajiriwi wote kila mwaka?
Jamaa mbinafsi sana.. hizo kazi ndio ana maslahi nazo
Tatizo hamuwezi kufikiria na kujua kuwa hizo kada mbili ndizo zenye watumishi wengi zaidi,ukiacha Askari polisi na majeshi mengine ambao bado wanaajiriwa.maafisa mifugo hata enzi za JK walikuwa wanaajiriwa kwa uchache.Mnabisha wakati ukweli huu hata wakubwa zenu wanaujua.
 
Mkuu ajira za Ualimu hazijatoka juzi au ulikua Canada na ndiyo umerudi?
Kuna watu huwa mnajitoa akili sana.Hebu sema wewe uliona lini awamu zilizopita,walimu wakituma maombi ya ajira?na Kisha wanaajiriwa baadhi tu?Walikuwa wanaajiriwa wote automatically.Fungua akili yako,isishikwe na shetani.
 
Kwenye upande wa elimu kidogo wanajitahidi!

Mwaka ambao hawakutoa ni 2016 tu! Lakini kuanzia 2017, 2018, 2019 na 2020 wamekuwa wakitoa! Probably na mwaka huu watatoa sema wanatoa kwa idadi ndogo mno ndio maana unaweza usione kama kuna chochote kinafanyika!
 
Hao ni watu walio kwenye vipau mbele vya nchi,na wengine pia.Na hebu jibu hoja,kwa nini siku hizi watu haawshawaajiriwi wote,kila mwaka?

Tatizo hamuwezi kufikiria na kujua kuwa hizo kada mbili ndizo zenye watumishi wengi zaidi,ukiacha Askari polisi na majeshi mengine ambao bado wanaajiriwa.maafisa mifugo hata enzi za JK walikuwa wanaajiriwa kwa uchache.Mnabisha wakati ukweli huu hata wakubwa zenu wanaujua.
Hata Jeshini siku hizi Ajira ni za kulenga kwa manati.

Masuala ya uchumi kukua no propaganda tu, ila ukweli ni kwamba HALI NI TETEEEÉ
 
ni wakati sasa kuwepo usawa wa fani zote sababu wote ni wahitimu..walimu na afya mna lia lia sana utadhani mnasoma peke yenu
 
Kwa hiyo wanatudanganya?
Tena kwa macho makavu kabisa.

Mimi nimegraduate 2016 sekta ya afya nikiwa na miaka 26 mpaka leo 2021 nina miaka 31 ajira hakuna, bila bila.

Tena bora ualimu wanatoa toa ingawa vijiajira vichache, Afya ndio kabisaa utafikiri haipo.

Mwaka jana walitoa ajira 555 ( imagine ) mwaka juzi hawakutoa kabisa.

Yaani tokea 2016 ajira ambazo wamewahi kutoa nyi gi sekta ya afya ni 2000 (2017) na 7000+ ( 2018 )
 
Kuna watu huwa mnajitoa akili sana.Hebu sema wewe uliona lini awamu zilizopita,walimu wakituma maombi ya ajira?na Kisha wanaajiriwa baadhi tu?Walikuwa wanaajiriwa wote automatically.Fungua akili yako,isishikwe na shetani.
Kila awamu ina utaratibu wake...jiwe ataondoka na majaliwa naye atakuja na mfumo wake..kwahy tulia.

We huoni ndege zinaagizwa tuu?
 
Kuna watu huwa mnajitoa akili sana.Hebu sema wewe uliona lini awamu zilizopita,walimu wakituma maombi ya ajira?na Kisha wanaajiriwa baadhi tu?Walikuwa wanaajiriwa wote automatically.Fungua akili yako,isishikwe na shetani.
Kwa kuwa walikuwa hawachujwi ndio maana hata wanafunzi enzi hizo walikuwa mbumbumbu na hata sasa madhara yake yanaonekana. Bado kuondoa dhana potofu ya ufundishaji mashuleni ni kikwazo kutokana na hao waluoingizwa kiholela
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom