Kama kweli Sabaya ana hii hatia leo aburutwe Mahakamani

Kama kweli alimteka na kumtesa kwa kipigo kikali Diwani wa Kata ya Sombetini, Bakari Msangi huko jijini Arusha basi alifanya kosa kubwa sana.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sauti Kubwa ni kuwa Bakari Msangi alienda kutoa msaada kwa vijana waliokuwa wamewekwa chini ya ulinzi na Sabaya na timu yake kwa tuhuma ya kufanya biashara ya fedha za kigeni bila kibari. Diwani Msangi alipigiwa simu na ndugu Ally Saady ili akatoea msaada.

Inasadikiwa vijana waliowekwa chini ya ulinzi na Sabaya na timu yake walipigwa kipigo kikali na baadhi yao kujisadia haja kubwa na ndogo na kujeruhiwa vibaya. Diwani Msangi alipofika kutoa msaada nae alipata kichapo.

My take; kama hizi tuhuma ni kweli leo hii Sabaya akamatwe na jumatatu afikishwe mahakamani. Asipofikishwa mahakamani basi tunajua ni unafiki wa kisiasa unaendelea.
Damu ya diwani huyu ni kiboko
 
Back
Top Bottom