Kama kweli Rais Samia alimaanisha hicho, basi huenda Lukuvi ni Waziri Mkuu anayengoja kuapishwa

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,115
35,129
Kama Rais Samia kile alichokisema kuhusu Lukuvi (kuwa amemtoa kwenye uwaziri na sasa anamleta ikulu kuja kumsaidia kuwasimamia mawaziri, na atampa kazi maalum ambayo watanzania tusubiri kuja kutangaziwa) basi huenda ikawa ni nafasi ya uwaziri mkuu!

Huenda kinachofanyika sasa ni kupima upepo wa kisiasa, kuvuta muda ili mchakato wa kumpata spika mpya ukamilike, bunge liitishwe na labda jina la waziri mkuu mpya likatangazwa.

Sote tunajua kung'olewa kwa Spika Ndugai ulikuwa ni mkakati wa kumdhoofisha Majaliwa kwenye mbio zake za urais kuelekea 2025, na lengo la kutaka kuundwa upya kwa baraza la mawaziri kulilenga kumtoa Majaliwa lakini ili kuboteza maboya tusijui chochote kilichokusudiwa baada ya kuhisi na taarifa kusambaa ikabidi yafanyike marekebisho tu kwenye baraza la mawaziri na kuvuta muda ambapo utekelezaji uliokusudiwa utanyika vizuri.

Ngoja tujipe muda.
Mambo ni mengi sana.
 
Za ndani zilizopigwa ni kwamba bwana kasimu ameshaandika barua ya kuachia ngazi. Bi mkubwa hajaisaini. Mchezo Utakuwa kama kwa Lowasa.
Lukuvi anaweza kukamata kiti kiulaini kabisa.
Kasimu tulikuambia baba diblo . Hakuna PM aliwahi kuwa president humu nchini
 
Tulieni snitch Au sio snitch ndio mtajua kunaswa na kuogopwa lipi bora = Maja baki Au Maja sepa
 
Back
Top Bottom