Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Raisi Magufuli,kama kweli una nia ya kuwatumikia watanzania na kujua matatizo yao,achana kabisa na utaratibu wa mtangulizi wako wa kukutana na wanaoitwa "Wazee wa Dar-es-salaam" na badala yake anzisha utaratibu mpya wa kukutana na watanzania pale Uwanja w Taifa.
Mh.Raisi,hili linawezekana kabisa ukiagiza litekelezwa.Njoo na timu yako(baraza zima la mawaziri na wasaidizi wako wengine) na viandaliwe vipaza sauti vya kutosha na spika za kutosha na mkutano wako huu na watanzania wa kawaida uwe unafanyika siku ya Jumapili jioni na uwe ni kila baada ya muda maalumu,mfano maro moja kila baada ya miezi mitatu.
Uwanja wa Taifa ndio sehemu sahihi na sio viwanja vya Ikulu,ukumbi wa Diamond, n.k ambapo walala hoi wengi na watanzania wa kawaida wanasita kufika au hawawezi kabisa pata nafasi hiyo ili hali nao ni watanzania kama hao wanaoitwa Wazee wa Dar-es-salaam.
Wanaoitwa Wazee wa Dar-es-salaam hawezi kukupa picha kamili ya maisha ya huku uraini zaidi ya kukupigia makofi na kukkufanya uridhild ukaona watanzania wote wanaridhika na kazi unayoifanya.
Kutanana na watanzania wa kawaida kisha wape nafasi watoe mawazo yao, wakushauri, wakukosoe na ujibu maswali utakayoulizwa na wale watakaopata nafasi ya kuongea na wewe moja kwa moja uwanjani hapo.Pia mawaziri wako nao wajibu/watolee ufafanuzi mswala yatakayowahusu.
Kama wakati wa kampeni mnawafuata watanzania hawa popote pale walipo hata kwenye vijiwe vya kawaha, iweje mkipata madaraka iwe ajabu (nongwa) kufanya hivyo?
Hii inaweza kuwa style mpya na ya kipekee kabisa duniani lakini ikawa ni ya msaada mkubwa sana katika uendeshaji wa nchi na ikawa mfano hata kwa mataifa mengine.