Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,396
Niliyaona hayo maswali na pasco akayakwepa ila kelele hazikuisha.Hembu tujiulize kama Mh E.L nae yupo determined akachukua njia ya kufanya "things right", nini itakuwa matokeo yake ndani na nje ya CCM ?Pi si yeye mwenyewe aliyeambiwa hafai,hata JK alipewa lugha nyepesi kuwa bado hajakomaa.Ila mwalimu Nyerere hakuweka timeframe atakomaa lini, wala vigezo kuwa akikomaa tutamjuaje?Kijana akampisha Mkapa kwa manung`uniko km leo tumuonavyo Zitto ,huku udini ukiongeza mashinikizo.Baadaye akaja na huu kelele zikisema kuwa keshakomaa na mengine mengi sana.
Sasa tupo hapa tulipo hata yale madini tuliyoambiwa tusubiri hadi tupate uwezo yamechimbwa na kuthibiika kuwa hatuna uwezo na hii ni kwa vile hatukuwa na vipimo kutuonyesha kama tumekomaa.Mheshimiwa EL kama atakuja tutegemee kauli kama alitubu kwa Joshua, na ahadi za vijana,na pia hayo masalia pia yatakuwa na kelele zao nyingi.
Nini maoni yako kama atatangaza nia.Akubalia achia kitu ambacho andhani kuwa ni haki yake kuweka ktk malengo na kupenda kuyafikia na kubaki akijilaumu kwa maisha yake yote?Arudi katika drawing board na kujipanga upya?au aamue kuwapa watanzania zawadi kwa kuivunja CCM kabisa na kubaki kama mzee mwenye furaha kwa alichowapa watanzania?Je kama watu wanaamini ni fisadi je atakuwa salama CDM au hata CCm yenye mtu nje ya mtandao akichukua nchi?
Kwa kuwa watanzania wanataka mabadiliko yenye kumaanisha chama mbadala ikiwa atatangaza nia, maana amekuwa akijaribu kufanya PR kampeni nyingi tu akidhani watu hawaelewi anachokifanya, basi huo ndio mwisho wa EL na itakuwa CCM imeanguka mwanguko mkuu.
Kama mkuu Kwitega alivyotanabaisha kuhusu hili swali lako nami naongeza kwamba atajiunga na walewale aliowaharibia kwama 2005 na watafurahi sana.