Kama kweli Mhe. EL alikubali kuwa kafara..basi sasa hivi anasubiri vinguvu vidogo kama Samsom. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama kweli Mhe. EL alikubali kuwa kafara..basi sasa hivi anasubiri vinguvu vidogo kama Samsom.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Sep 6, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Najiuliza.Kama kweli Mheshimiwa E.L alikubali jitoa kafara.Kwa imani yangu sioni jinsi gani atatoka katika tope ili akawapige wafilist, bila kutoa kafara kubwa zaidi(tayai riba imeongezeka).Kwa hali inavyoendelea katika nchi na katika chama tawala sioni kabisa kama mh atakuwa tofauti na samson alipoanguka(kwa hadaa ya Delila) na aliponyanyuka aliomba apelekwe katika nguzo na alichoweza ni kuvunja mihimili ya jengo na kujimaliza na watesi wake wa kifilisti.

  katika options zilizopo ni kwamba:

  1. Kupambana katika chama ambapo pamekaa vibaya kwani mchuano wa mwisho lazima uharibu chama kabisa.Wote wanaotega nyavu wanajua miaka 10 mingine ya kusubiri ni kama hukumu ya kifo(umri mkubwa), ni bora kupambana na kufia ikulu.Kazi itakuwa ngumu sana kuwashinda wengine ambao hawapo tayari kuacha kete ya "kashfa" ambazo hapajawa na nia thabaiti ya kuzisafisha.
   Na hata zikifutwa bado kuna watu watapita nyumba kuzieneza kupitia mlango wa nyuma ili kumpunguza nguvu zake na kuondoa hasira. Hapa panahitajika big fish kufanya endorsement,itakayo dwarf visauti vyao.Na sasa hivi CCM hakuna big fish wa kuweza simama jukwaani na kuach aimpact yoyote noticeable.Ila wa kutoa kafara yenye impact wapo.
  2. Kwa yeyote atakayesimama na kiongozi yeyote wa CDM katik uchaguzi mkuu.Kuna maneno CDM wakiyasema "ufisadi ", "rasilimali", na matukio yanayohusishwa na polisi yatakuwa kama "cluster bomb" achilia mbali disperate loosers wa mchakato wa CCM watakuwa kama mbogo aliyejeruhiwa.
  Kwani hakuna atakayekuwa tayari kutegemea aje igia katika kinyang`anyiro kigumu katika chama akiwa na miaka 80.Kwanza hana hakika ya kuishi huo umri, pili hajui kama atakuwa anauzika tena, tatu hajui kama chama kitakuwa hai tena.Mpaka ifike hapo CDM watakuwa tuu si wanaleta matumaini bali wanawapa watu kiu ya kuwataka tena.
  Watakuwa katika mioyo na mavazi ya wananchi.watakuwa wakivutia kama mechi za mpira.Na watakuwa na "margin of error" kubwa. Kama nchi za kijamaa zikikosea huwa hazilaumiwi kama za kimagharibi.
  Kwa hayo hapo juu ni wazi number moja haiwezi pita bila kuharibu CCM big time.Number mbili "uchaguzi mkuu" hautakuwa tena ulivyokuwa miaka yote, CDM watakuwa celebrities of their own, mateso watakayopitia watakuwa wamegeuzwa kuwa manabii.They will rock the world kama latest lamborghini in the highway.​
  Watakuwa na uwezo wa kutangaza wanahitaji defectors wangapi na kuwapata instantly. Mh. E.L bado ana idadi ya watu wanamkumbuka kama mtu wa actions,ila ana doa. Doa halina mjadala linahitaji "big mwanakondo" na mwenye thamani.

  Hakuna blah, blah zitakazozimisha muziki wa CDM, ikipigwa anthem yao "people`s power " masikioni mwa watu italia kama baragumu, hakuna mtutu utakaowasimamisha, na kwa sasa kila risasi inayotoka ni ushindi kwa CDM mara millions na damage kwa CCM mara billions.

  Mbaya time inavyokwenda resources zinapungua na problems zinazidi kwa upande wa CCM.Mfano.Taasisi na balozi za mataifa zitakuwa hakimu dhidi ya CCM, waandishi wa habari watakuwa na migomo au wataandika habari za kuimaliza CCM kwa vile tayari CCM haina public relationship inayojenga.

  Kuchangnayikiwa kutakuwa kukubwa kwa vile CCM watakuwa busy kuburazana katik NEC wakitoka huko wamevuana nguo kwa kashfa ambazo zimewachafua kabisa. CCM watakuwa na inteligensia za uongo zinazopikwa na wapambe kila dakika hap dar n ahivyo kujikuta surprices haziishi. Na atakayekwenda simama na CDM atajikuta raia ndio wanamjibu kwa vile wanajuana na CDM kwa sana.

  CDM watakuwa busy wakijituma kupanga ulinzi wa kura na kupanga safu ya uongozi, kwani watakuwa wamesaidiwa sana kazi na machinery ya CCM. Kwa aliyeona mzee 6 atakubali jinsi upepo ulivyompitia, sasa hivi sie shida tena kwa CDM,ila ni liability kwa CCM. Na wengi watakuwa liabilities by 2015.

  Kwa mhe..E.L itabidi atoe kafara kubwa, na aitoe now kafara hiyo watu waanze shuhudia,watu waanze pata muda wa kufuta mabaya halafu pia wapate muda kumjengea taswira njema(Yaani kufuta mbaya+kuwekwa mpya).Bila hivyo yetu macho.Mhe. atakuza vinwele vidogo kwa kumpatia vinguvu vidogo vya kutosha kuvunja mihimili ya nyumba na kujimaliza yeye na adui zake.

  Hao wanomdanganya kumsafisha kwa kauli nyepesi hadharani na kumponda kwa kwauli nzito faraghani wanampofusha macho ili akimaka asione njia.Na hapa hata waliomtoa kafara hakuna tena mwenye kauli ya nguvu ya kuweza msafisha(cdm wanamalizia kuwa disable)..wote watakuwa kama vinywele vidogo katika mwili wa samsom na havitoshi rudisha nguvu alizopewa kiasili...

  Mheshimiwa ataishia washinda wapinzani dhaifu CCM na kuomba wafuasi wake wamfikishe katika nguzo za CCM na kuzivunja kwa vile hatokuwa na macho ya kuona njia ya kwenda mbali hadi uwanja wa vita "uchaguzi mkuu"....Kila eventuality sasa hivi kwa ccm ni bora jana..CCM si brand Tena, na hawana tena populist kama Kikwete term ya kwanza.So Lazima hero azaliwe kwa kufanya mambo makubwa na magumu kwa faida ya jamii,tena sasa hivi.Aliyesikia na asikie....wa kuikumbuka hii na aikumbuke....Fuuuuuuull Stoooop.

   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ni muda sasa CCM wachukue mzigo wao wa failures, watuachie nchi yetu salama na watu wenye uwezo wa kuwasaidia wananchi wawasaidie. Hatuhitaji blah blah tena!!
   
 3. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  mnaona mbali sana. this is a political vision
   
 4. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona unaongea kama Nabii vile!
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Lowasa kitakacho mfanya haeshimike ni kutojihusisha na kuikashifu na kuiadaa chadema.....samwel sita ameonekana mpumbavu kwasababu ya kuangaika na chadema na slaa matokeo yake watu wamemwona mpumbavu.....lowasa na tuhuma zake akae kimya akiivagaa cdm tu huo utakuwa ndiop mwisho wake kisiasa.......
   
 6. d

  dotto JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kujitoa kafara ili kuficha ukweli halafu huyu ndo jasiri mwenye maamuzi magumu!!
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Sasa ni aje ataweza pata nguvu kubwa bila kutoa kafara kubwa?Kwa sababu akiingia kama alivyo (huku raia wakiamini waaminicho)katika uchaguzi mkuu CDM wana kila njia ya kushinda .Zoezi la Kufuta CDM halitakuwa na faida kwa CCM na litawarudisha CCM ground Zero kama si underground kwani kuna taasisi za kimataifa zinapiga jicho na wananchi wana hisia kazli sana kuhusu CDM.

  Sioni mwana ccm yeyote mwenye "moral authority ya kuweza simama na kumsafisha jukwaani kwa mafanikio".Akisimama hata mwehu anaweza rudisha matokeo sifuri.Kama kweli mh. alikubali hilo litokee kama sadaka,kweli kawapa CCM sadaka kuu na hiyo itakuwa ndio blunder kubwa sana.Huwezi jitoa mhanga kwa "kukubali kuitwa mbakaji halafu ukategemea kusafisha hilo".Tatizo ni kwamba suala la ufisadi si rahisi lizmisha kwani kila siku kuna report inayozumzia "ufisadi" na hivyo kuwakumbusha watu habari ileile ambayo haijawekwa sawa.Wengi watasema kumbe ha huyu ni "fisadi" kama fulani.

  Mbaya zaidi, ni kwamba vita za makundi ya CCM, hakuna hakika kama hata hao wanaosema mema hadharani ,hawaongei maovu mara dufu sirini na katika faragha zao.Hizi habari za nyuma ya mgongo zinaaminika kirahisi na zinaenea kwa kasi "ni habari amabzo mara zitokapo ni kama zinakuwa hai na janja, ni kama zinakimbia ili zisifutwe"

  Zuma alitoa kafara kubwa, Malema naye anaweza toa kubwa sana na akarudi ktk siasa.Ila sasa yeye ana wananchi waliokuwa active katika siasa kwa miaka zaidi ya 70.Yaani Malema alichoongea kilikua ni ubaguzi ila kuuwawa kwa wachimbaji, halafu kushitakiwa ni "sabuni nzuri sana kwake juu ya hao wamiliki ambao ni weupe"

  Kwa mtu mzembe atadhani nina mshambulia au ninambeba mheshimiwa ila kiu kweli ni kuwa ni suala lilitoka fikra zangu
  .NI KAMA -KAMA JIGSAW ambayo ikipangika ni worth kuandikiwa kitabu.Ikichezwa in a fair way ni Test ya urais in itself.KWani CCM wapo ktk deadlock, wamepita katika njia isiyotokeza mtaa wa pili.

  Mpaka sasa mgombea yoyote wa CCM atakaye kimbizana kupata ridhaa ya CCM anahitaji nguvu kubwa sana.Kwani nguvu za wengi kama si wote zitaishia siku CCM inamteua km itafaika salama.Kwani mshindi atajikuta kashinda na CCM imekufa.

  CCM wamejiweka sehemu ya kuwa na wagombea wasiongalia chochote zaidi ya kushinda vyote,hata kama kwa kuharibu wakigombaniacho.CCM wamekiweka chama mahali ambapo " Ama mgombea awe Liability au chama kiwe liability " na si vinginevyo. Mchakato wa kumpata mgombea hadi kupata anakuwa kachafuka kiasi hawezi wakilisha chama, na kama akifika akiwa msafi basi CCM inakuwa ni mzigo kwa vile tayari haipendwi.Na CDM wamejiweka mahali pa kuwa kipimo cha vyma vingine na hawagusiki, yaani chochote kibaya kiwapatacho automatically CCM ndio wanoneka kuwa wachawi.Sasa CCM ndio atapewa kazi ya kumtumza CDM kwani kila dhara ni si hasara kubwa kwa CCM na viongozi wanaolinda wasijepotea dkdk za mwisho kama ghaddafi.Yaani wameshakuwa mahali pa kuambiwa "Mchawi mpe mtoto".
   
 8. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Yeah hiyo ndio njia sahihi.Ila mwisho wa siku watajikuta sehemu moja kama wapinzani kati mchuano wa kufa na kupona na hatkutakuwa na ujanja wa kukwepana.Kama mheshimiwa ataamu aingia katika kiyang`anyiro.Hapa ndipo napaangalia.Je katik CCM kuna takayefika akiwa na nguvu tena?Kwani mgombea yoyoe atakayefika atakuwa na makovu sana, na CCM inyopigana na wawakilishi itakuwa hoi kwani nayo ilikuwa vitani.Nadhani unapata Picture iliyonipa iliyonifanya nijiulize maswali mengi.
   
 9. k

  kwitega Senior Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowassa alikataliwa na Mwalimu tangu mwanzo juu ya uadirifu wake na hadi Baba wa Taifa anaenda kaburini, Lowassa hakuwahi kujitokeza kueleza jinsi alivyopata mali zake. Iweje mtu yule yule aliyetiliwa shaka juu ya uadirifu wake tujipendekeze kwake eti anatakiwa kufanya hivi na vile ili asafishike? Huyo alishachafuka tangu zamani na hawezi kujisafisha akatakasika. Kashfa ya Richmond iliyozaa Dowans ambayo imeamriwa kulipwa bilioni 96 itaendelea kumwandama hadi siku ya mwisho. watu wanadiriki kusema eti alichkuwa anakifanya kuhusu Richmond hadi JK alikuwa anakifahamu. Je, hiyo yatosha kwake kusema hahusiki na kashfa hiyo? Kama alikuwa hakubaliani na mchakato wa kuipa Richmond Mkataba kwa nini hakujiuzuru? Hapo tungemwelewa na tungemuunga mkono. Hata hivyo, hatujawahi kusikia akisema hivyo. Alichokisema ni kwamba hakuna ambacho swahiba wake, JK hajui kuhusu Richmond. Huyu hafai kuwa kiongozi Mkuu wa nchi. Angalia juzi umetokea mgogoro wa mpaka kati yetu na Malawi; hamkusikia kauli zake? Baadaye hamkusikia jinsi JK alivyomsiriba yeye na Membe? Huyo ndiye leo tunajikomba eti ajisafishe? Analipwa mafao na kupewa stahili zote kama PM mstaafu; ni mstaafu kweli? Tusizoee kuunga mkono hoja za hovyo kwa maslahi binafsi. Tuweke maslahi ya Taifa mbele kwanza. Tuseme Taifa kwanza, matumbo yetu nyuma full stop.
   
 10. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Hakuna anayemtetea au kuchabikia yeye kujisafisha,ila as long as nia yake inaweza kuwa katika siasa na nortion nzima ya ukweli wa hii habari kuwa alikuwa kafara ya kisiasa, panibuka challenge ya ni vipi ataweza jinasua? majibu tutakayotoa na maswali tutakayouliza yanaweza saidia leta fikra tofauti,yanaweza fanya watu wapige mahesabu yao vizuri na kuona kama kuna haja ya kumshauri agombee.Na akigombea basi nini kinaweza kuwa matokeo yake kwa nchi na kwake binafsi.

  Ukweli ni kwamba akiamua gombea hakuna doubt matokeo ya kugombea yataathiri kila mtu.Haijalishi jina gani kapewa Jamaa bado ana nguvu katik siasa sa CCM na automatically za Nchi.So si kitu rahisi kupotezea,ila ni vizuri kuangalia possibilies.

  Kwa jinsi ulivyoongea mwenyewe ni kwamba mh.. anahitaji zaidi ya maneno matupu kuweza hata kushawishi wewe.Sasa kama ana nia na nguvu ya kugombea, nadhani utakwazika na mkikwazika wengi inakuweje?Ndio maana najiuliza kama kuna ukweli wa yasemwayo.Je kwanini alikubalia iwe hivyo?Kumbuka kama ni "kafara" basi imeshakuwa na "riba" na kuikomboa hiyo kafara kunahitaji kafara kubwa zaidi.Na hakuna raia atakayependa kusikia kuwa CCM wameamua mteua huku wameshindwa msafisha halafu waamue lazimisha raia kumchagua.
   
 11. k

  kwitega Senior Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisema alikuwa kafara ya kisiasa unamaanisha nini? Kama nimekusoma vema na kukuelewa, unamaanisha alibebeshwa mslaba usio wake kwa ajli ya wengine? Kama unamaana hiyo ndugu yangu samahani sana. Soma tena ripoti ya Mwakyembe kuhusu Richmond utaona kama kweli EL alikuwa kafara ya kisiasa. Narudia tena kusema kwamba; hata kama atajieleza vipi, ni vigumu kusafishika. Richmond na hatimaye Dowans imesababisha maafa makubwa kwa nchi yetu. wapo watanzania waliopoteza maisha kutokana na kukosa huduma za upasuaji mahospitalini kwa kukosa umeme. Kusua sua kwa uchumi wetu kunachangiwa na kupanda kwa gharama za mafuta lakini pia mgao mkubwa wa umeme uliokumba taifa kwa miezi minne mwaka jana. Haya ni matokeo ya Richmond. Huyo jamaa angeonekana wa maana tu pale ambapo angekataa kuingia kwenye tope hili hata kama alilazimishwa na mtu awaye yote.

  Nguvu katika chama kwa maana gani? Ni masuala yale yale ya mitandao binafsi yenye malengo ya kuchukua dola kwa maslahi binafsi lakini si maslahi ya umma. Yeye huyo huyo ndiye alikuwa Mwenyekiti wa mtandao 2005. Matokeo yake yanaathiri nchi hadi sasa. Ni rahisi kusema ana nguvu ndani ya Chama chake kwa mtazamo huo hasa kama anaota urais 2015. Mtandao aliokuwa anaongoza 2015 ulizusha mambo mengi ya kipuuzi na kuwaacha baadhi ya wanasiasa wanaoheshimika ndani na nje ya nchi wakiwa na majeraha makubwa. Mfano ni Dk. Salim Ahmed Salim. Huyu alizushiwa eti alikuwa mwanachama wa Hizbu, mara sijui alishiriki kumuua nani, mara anandugu Uarabuni ambaye ni Afisa wa ngazi za juu jeshini. Upuuzi mtupu! Hatuwezi tukaendesha siasa na ushindani wa kistaarabu na kuheshimiana? EL alifurukuta kuleta Teknolojia ya mvua kutoka Thailand. Mwisho wa siku tunaambiwa mradi huo ulikuwa hauihitajiki kwa Taifa. Lakini hadi unasitishwa tuliambiwa 1.5 Tsh zilikuwa zimetumika. Je, kama mradi ulikuwa hauhitajiki ilikuwaje EL aliupigia chapuo hadi ukalamba kodi zetu hizo? Je, hilo lilikuwa li-Richmond jingine? Tunajua mipango ya serikali ni endelevu, kwa nini mara baada ya yeye kubwaga manyanga kwa kashfa ya Richomd, mradi huo haukuendelezwa? mara eti anajitokeza kusema anapinga sera ya kilimo kwanza. Anasema elimu kwanza, kilimo kifuate baadaye. Amekuwa serikalini kwa muda gani? Hayo mawazo na ushauri alikuwa wapi kuutoa hadi leo hii ndiyo anajitokeza kukosoa? Kwa muda mfupi aliokuwa PM aliacha nini kuhusu sekta ya kilimo ambacho mrithi wake alikikuta? Kama jibu ni hakuna, iweje akosoe kilichoanzishwa na Pinda? Au kama kipo ajitokeze aseme ili tujue kumbe alikuwa na mawazo mema ya kuendeleza sekta ya kilimo lakini yamepuuzwa. Hatajisafisha kwa kumuingiza swahiba wake kwenye kashfa ya Richmond, kuponda kilimo kwanza, kusema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kuripuka, kushambulia serikali iliyoko madarakani nk. Alichokisema Baba wa Taifa 1995 dhidi yake ni mwisho wa tamaa yake ya kutaka madarka makubwa zaidi katika nchi hii.
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama ulinotice neno "km ni kweli"...sijaconclude usafi wake wala kumlaani.Ila nilijikita kuangalia uwezekano wake na CCM kuwa na impact katika Uchaguzi kama atakuwa na nia na kuweza washinda wengine katika CCM.Pia nimejaribu angalia kama atagombea hana budi kujisafisha, na zoezi zima la kujisafisha kuonekana kuwa gumu tofauti sana na watu wanavyofikiria.
  Kama kweli anamiliki mtandao wenye uwezo hivyo ni wazi kuwa nguvu zake haziwezi dharaulika.weather ni nzuri au mbaya ila ni worth kutambua uwepo wa hizo nguvu. Halfu ndipo uje katika terms na Idea kama akigombea njia yake ipo vipi na impact zake kwa watanzania.Tutajidanganya kusema kwa vile watu wanaaamini kuwa "alikosa" na sio sacrifice basi ni rahisi kumuona kama hayupo alive katika politics za CCM na za Nchi.Ni bora tukubali hilo ili tuone options alizonazo ili kufikia apendapo au wapendapo wananchi wengine na wasipopenda baadhi ya wananchi.
   
 13. k

  kwitega Senior Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa mtazamo wako na maoni yako. Nadhani haka nako ni ka mkakati ka huyo bwana. Ulisema ana nguvu katika Chama nami nikakujibu bila kukuhoji ni wana CCM wangapi kwa mjibu wa utafiti wako umegundua wanamuunga mkonoi na kumkubali kiasi cha kusema ana nguvu katika chama. Lakini nikarudi nyuma juu ya yale yaliyotokea mwaka 2005 ambapo EL Lowassa alikuwa Mwenyekiti wa mtandao ambao matokeo yake yanatuumiza leo. Nikasema kama ni kwa mantiki hiyo unayoisema kwamba ana nguvu katika chama; basi inatokana na mtindo ule ule uliotumika kumwingiza swahiba wake; kutumia mtandao. Ni mtu gani iwe ni mwana CCM au la atakayekubali mtandao mwingine usio na maslahi kwa chama na kwa taifa utumiwe kumuingiza mtu madarakani? . EL mwenyewe siku alipokuwa anabwaga manyanga alisema, "tatizo ni u PM". Kivipi, anajua yeye maana hakutolea ufafanuzi. Masuala ya kwamba alichokifanya ni sacrifice, yanatoka wapi? Narudia tena, hata kama alikubali kuingia kwenye tope la Richmond kwa msukumo mwingine kutoka popote pale na yeye akakubali kwa hofu ya kupoteza kitumbua; conclusion ni kwamba anapungukiwa sifa za kuwa kiongozi Mkuu wa wa nchi. Huwezi ukalazimisha tukubali unachotaka wewe bila ya hoja na mantiki zitakazosababisha tufike huko. Inasemekana Tanzania ina wanachama zaidi ya milioni 5. Sijui kama takwimu hizi ni sahihi maana wanachama wanaoingia na kutoka ni wengi. Haijalishi, naomba utupe takwimu ulizonazo na source yake ambazo zinaonyesha kuwa EL ananguvu katika chama chake cha CCM. Kuwa na nguvu ni kukubalika na kuungwa mkono na wanachama walio wengi. Hatumchukii kwa jinsi alivyo, lakini tunachukizwa na baadhi ya maamuzi yake yanayolitafuna taifa hadi sasa. Hivi kwa mfano kama yeye ndiye angekuwa JK yuko Ikulu kwa muda huu, maana yake ni kwamba Taifa lingekuwa vitani na Malawi. Kauli aliyotoa ni ya kukurupuka. Ni ya mtu anayeota u- amiri jeshi Mkuu na ni watu wa hovyo tu ambao wanaweza kuwa na mawazo kwamba eti EL anaweza kuwa presidential candindate kupitia CCM. Yeye kwake kila jambo ni kufanya maamuzi magumu bila kuangalia sababu na athari za maamuzi hayo?. Noooooo, EL ana madoa mengi mno ya kisiasa ambayo ukichambua moja ya jingine utaishia kuambiwa unatumwa, unachuki binafsi nk. Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Nyerere hayuko nasi kimwili tu lakini anaishi bado kwani falsafa na wosia wake juu EL bado tunaukumbuka, hatoshi kwa nafasi unayotamani agombee.
   
 14. w

  wauwau JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 705
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa tuunge mkono hoja zako hata kama ni dhaifu hivyo?
   
 15. k

  kwitega Senior Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ambavyo huwezi kuunga mkono hoja zangu, vile vile siwezi kuunga mkono za kwako. kwako hoja ya Richmond na matokeo yake ni upuuzi! inawezekana unaishi peponi au kwenye Mars hivyo hujui yote hayo! Nimeuliza swali tupe takwimu wana CCM wangapi kati ya milioni 5 wanaomuunga mkono kiasi cha kusema ana nguvu ndani ya Chama. Tuambie na chanzo cha takwimu hizo. Acha kutoa majibu ya mkato jibu hoja kwa hoja. Kama hoja zangu dhaifu; ulizotoa wewe ziko wapi? Taifa kwanza, matumbo yetu nyuma!
   
 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Personally sijaona km umekataa nguvu zake ila umekataa njia unazoamini zilimpatia hizo nguvu bado hatunagongana.Kwani mimi naongelea nguvu zake na wewe unaongelea jinsi alivyozipta hizo nguvu.

  Kuna mengi sipingani nawe,ila pia siwezi yatolea majibu kuhusu nji ailiyomfikisha hapo alipo.Ni yangu nikuiliza kama anataka toka hapo alipo alipo nini effects zake kwa uchaguzi mkuu ujao?

  Naona umepoint out kuwa anafanya maamuzi ya kijasiri bila kunagalia madhara.sipendi shikilia kama hoja yangu ya kudiscuss uwepo wake katik siasa na effects zake kama tafanya maaduzi ya kuingia katika uchaguzi, na njia atakazoweza zitumia kujaribu jinasua.Sasa jaribu fikiria kama ataamua kijasiri kama ulivyompa hiyo sifa kuingia katika kinyang`anyiro cha kugombea urais?Sidhani kama utakuwa na muda tena wa kuuliza jinsi gani huo mtandao uusemao umetengezwa,bali nini kitafanywa na huo mtandao.Hapo ndipo ninaposema pana showdown ambayo itahusu watu wengi sana, kwani hata upinzania ndipo watapata maeneo ya kujenga silaha na mashambulizi yao.
   
 17. k

  kwitega Senior Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ananguvu zipi wewe ndugu yangu? wewe ndiye uliyesema awali kuwa ana nguvu katika chama na nimeshakujibu na kukuomba utupe takwimu na chanzo chake.Hujafanya hivyo, sijui kama unazo au hauna. Nyoka akitaka kufa huwa anajilaza barabarani kiulainiiii, kisha gari inapita juu yake anakuwa kama hakuwepo tangu zamani. Ndivyo itakavyokuwa kwa CCM kama watajidanganya kwa namna yoyote ile kusimamisha mgombea urais wa aina hii. CDM itapeta kiulaini mno. Kwa vile EL ni mtu wa kukurupuka na maamuzi magumu ambayo mwisho wake yanakuwa hayana maana, ajaribu karata yake kama mtanzania mwingine yeyote ili tuweze kuanika ***** zaidi hata ambao haujasemwa dhidi yake. Atajisafishaje kuhusu kashfa ya Richmond? Hilo moja tu linatosha kusema EL+urais 2015= 0
   
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Hembu tuwasikilize wana CCM kama watasema hana nguvu katik chama chao....sikuanzisha thread ili nijibu kila kitu mimi mwenyewe.

  Pengine hapo pa kujisafisha ndipo najisikia raha kusikia kwa wachagiaji wengine zaidi.kwanini mi sijaon njia rahisi zaidi ya kutoa kafara kubwa.
   
 19. k

  kwitega Senior Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi mwenyewe mwana CCM lakini aliyeokoka. Kwa hiyo mchango wa kwanza ni huo ndugu yangu, tuwaachie na wengine wachangie.
   
 20. K

  Kinombo JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 24, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  dowans/richmond ndo hiyo inalipwa bil.96....
   
Loading...