kama kweli hii ni aibu kwa PCCB....

mwanadaresalaam

New Member
Nov 10, 2010
3
0
habari ndio hiyo. PCCB kimeo mwanawane....:israel:
 

Attachments

  • barua.jpg
    barua.jpg
    69.3 KB · Views: 302
Kwa nchi zinazozingatia utawala bora, 'mnene' wa PCCB angeshaachia ngazi kwa utumbo huu. Lakini bongo anaendelea kutesa utadhani hakuna kilichotokea!
 
Kama kuna asasi zimelitia taifa hasara na kulihaini ni asasi mbili; nazo ni Usalama wa Taifa (TISS) ambao mara kadhaa wametumika kuficha hila za kuliangamiza taifa badala ya kuliokoa! Nashindwa kuelewa ni vipi uhalifu mkubwa kama ule wa mitakaba hatari kwa maisha ya watanzania kama ya EPA, Richmond, IPTL, Meremeta, Buzwagi , Kagoda na mingine lukuki yenye madhara makubwa kwa taifa letu ifanikiwe bila ya kuchukuliwa hatua na Intelligence organ hiyo. Ninavyofahamu intelligence and security work inahusisha viashirio vya maafa kwa taifa hata kama si ya kutumia silaha. TISS wamejikita kwenye kuwalinda viongozi hata wanapolihaini taifa kwa kufanya vitendo ambavyo ni potentially catastrophic kama vya kuingia mikataba mibovu, kuiba kura, kuruhusu magari na vitendea vyao kutumika kwa shughuli zisizo rasmi na tija kwa taifa kama hivi karibuni ilivyoshuhudiwa magari yao na ya ikulu kubandikwa namba za kiraiana kutumika na familia ya mgombea urais mmoja. Kwa wenzetu asasi kama hii haikubali kumvumilia hata Rais akitenda kitendo kinachohatarisha mustakbali wa taifa kama ilivyokuwa kwa Rais Nixon ambaye baada ya vyombo vya kutulia shaka hila katika kampeni viliendesha uchunguzi mkali ulioishia na kushtakiwa na kuhukumiwa wengi na Rais kuondolewa madarakani.
Na kuhusu TAKUKURU ndiyo kabisaa; yaelekea shughuli wanayoifahamu vyema ni kuwa - flagi na kuwasafisha wala rushwa wakubwa na si kuzuia. Uhalifu uliofanywa na taasisi hii katika uchunguzi wa Richmond na sasa hii ya "kumsafisha" Chenge ni vielelezo wazi katika hili. Asasi hii ni nyepesi kutafuta "simple popularity" kama walivyofanya wakati wa mchakato wa kura za maoni ambapo hakuna kilichoendelea baadae. Taifa limeingia katika aibu nyingine kubwa kutokana na kitendo cha asasi hii kukurupuka na kujaribu kumsafisha Chenge, na muda mfupi baadae Ubalozi wa Uingereza kukanusha jambo hilo hilo! Ni kutokana na nchi yetu kukosa utamaduni wa kuwajibika, vinginevyo kwa mara nyingine tena Mkuu wa taasisi hiyo alipaswa kuachia ngazi angalau kwa asasi yake kuliaibisha taifa kiasi hicho.

Kwa mitaji hii TISS na PCCB zimepoteza moral authority mbele ya macho ya watanzania na wanaonekana kama part of the existing problems. Njia pekee ya kurudisha imani kwa wananchi ni kumpata kiongozi atakayekuwa na guts za kuvunja vyombo hivi na kuviunda upya.
 
Tusitegemee chochote kwa PCCB, ni moja ya chombo cha CCM cha propaganda. Mikashfa yote hii kwenye hili taifa lkn watu wanasafishwa tuu na hawa hawa PCCB. Aibu tupu kweli Mnene wa PCCB achia ngazi kashfa kubwa sana hii.
 
Kwa nchi zinazozingatia utawala bora, 'mnene' wa PCCB angeshaachia ngazi kwa utumbo huu. Lakini bongo anaendelea kutesa utadhani hakuna kilichotokea!
Ni kweli na ndio maana viongozi wetu wanatudharau hivi
 
PCCB walidhani Waingereza-SFO wanaendeshwa kwa maslahi binafsi kama wao. Aibu imewapata sijui watakuja na hadithi gani tena!
 
bila kuchukua jukumu la sisi wanachi kuwatandika hawa viongozi na yeyote
atakae kuwa nyuma yao hatutafanikiwa kuwaona wanaachia madaraka waliyoshindwa
kuyatekeleza, hapa ni mtaani tu na kuchapa fimbo heshima itarudi
 
Tusitegemee chochote kwa PCCB, ni moja ya chombo cha CCM cha propaganda. Mikashfa yote hii kwenye hili taifa lkn watu wanasafishwa tuu na hawa hawa PCCB. Aibu tupu kweli Mnene wa PCCB achia ngazi kashfa kubwa sana hii.

Kuna umbea umezagaa mitaani kwamba sio rahisi mzee wa vijihela kushitakiwa kwa kuwa;
1.Hosea - mkuu wa takukuru "ale nsukuma"
2.Feleshi - DPP "ale nsukuma"
3.Manumba - DCI "ale nsukuma"
4.Chenge - mzee wa vijisenti "ale nsukuma"

sijui kama kuna ka ukweli ama ni umbea tu wa wadanganyika.
 
Hata kushtushwa na habari hii hawatashtuka zaidi ya kujibu tope tena kwa balozi hawa ndio pacha wa mafisadi, nani wa kumfanya nini zaidi ya aliyemtua? mtapiga domo mtaishia kwenye forum zenu. hii ndio jeuri ya watu wanaolipwa mishahara kwa kodi za umma, mapambano bado tuyaendeleze ipo siku haina jina tuombe uhai na afya njema kama si sisi basi wenetu na vijikuu
 
Kuna umbea umezagaa mitaani kwamba sio rahisi mzee wa vijihela kushitakiwa kwa kuwa;
1.Hosea - mkuu wa takukuru "ale nsukuma"
2.Feleshi - DPP "ale nsukuma"
3.Manumba - DCI "ale nsukuma"
4.Chenge - mzee wa vijisenti "ale nsukuma"

sijui kama kuna ka ukweli ama ni umbea tu wa wadanganyika.

ni umbea kivipi ilhali kila kitu kiko wazi? tena wote Wanyantuzu hao.
 
Huyo mnene wa PCCB ni bingwa wa kusafisha nakumbuka aliwahi kusafisha pia Richmond, kwa hiyo sio jambo la kushangaa kabisa. ila ni mgumu kuwajibika kinyama
 
Takukuru ni taasisi ya kuwalinda mafisadi,Kati ya watu wa ajabu duniani nadhani hosea ni namba moja,tumuombe mungu sana maana tunako elekea ni kubaya sana,watu kama hosea awaitajiki hapa duniani,maana ni waongo na wanafiki.
 
hamjui kuwa haya mambo yanawagusa watu wakubwa wengi sana km mkapa,mramba.............ndiyo maana chenge alisema ni 1.4bil. ni "VIJISENTI" Kwani wenyewe wapo na wametulia na ni wale ambao kikwete anawalinda kwa gharama kubwa kwa kusema tuwaache wapumzike
 
Back
Top Bottom