mwanadaresalaam
New Member
- Nov 10, 2010
- 3
- 0
Kama kuna asasi zimelitia taifa hasara na kulihaini ni asasi mbili; nazo ni Usalama wa Taifa (TISS) ambao mara kadhaa wametumika kuficha hila za kuliangamiza taifa badala ya kuliokoa! Nashindwa kuelewa ni vipi uhalifu mkubwa kama ule wa mitakaba hatari kwa maisha ya watanzania kama ya EPA, Richmond, IPTL, Meremeta, Buzwagi , Kagoda na mingine lukuki yenye madhara makubwa kwa taifa letu ifanikiwe bila ya kuchukuliwa hatua na Intelligence organ hiyo. Ninavyofahamu intelligence and security work inahusisha viashirio vya maafa kwa taifa hata kama si ya kutumia silaha. TISS wamejikita kwenye kuwalinda viongozi hata wanapolihaini taifa kwa kufanya vitendo ambavyo ni potentially catastrophic kama vya kuingia mikataba mibovu, kuiba kura, kuruhusu magari na vitendea vyao kutumika kwa shughuli zisizo rasmi na tija kwa taifa kama hivi karibuni ilivyoshuhudiwa magari yao na ya ikulu kubandikwa namba za kiraiana kutumika na familia ya mgombea urais mmoja. Kwa wenzetu asasi kama hii haikubali kumvumilia hata Rais akitenda kitendo kinachohatarisha mustakbali wa taifa kama ilivyokuwa kwa Rais Nixon ambaye baada ya vyombo vya kutulia shaka hila katika kampeni viliendesha uchunguzi mkali ulioishia na kushtakiwa na kuhukumiwa wengi na Rais kuondolewa madarakani.
Ni kweli na ndio maana viongozi wetu wanatudharau hiviKwa nchi zinazozingatia utawala bora, 'mnene' wa PCCB angeshaachia ngazi kwa utumbo huu. Lakini bongo anaendelea kutesa utadhani hakuna kilichotokea!
Tusitegemee chochote kwa PCCB, ni moja ya chombo cha CCM cha propaganda. Mikashfa yote hii kwenye hili taifa lkn watu wanasafishwa tuu na hawa hawa PCCB. Aibu tupu kweli Mnene wa PCCB achia ngazi kashfa kubwa sana hii.
Kuna umbea umezagaa mitaani kwamba sio rahisi mzee wa vijihela kushitakiwa kwa kuwa;
1.Hosea - mkuu wa takukuru "ale nsukuma"
2.Feleshi - DPP "ale nsukuma"
3.Manumba - DCI "ale nsukuma"
4.Chenge - mzee wa vijisenti "ale nsukuma"
sijui kama kuna ka ukweli ama ni umbea tu wa wadanganyika.
Hao wenzetu wameweza kuwa waungwana kiasi hicho, swali, Je hizo exgrantia zitamfikia mwanachi wa Tanzania ambaye ndiye mhanga au zitapelekwa kufidia gharama za exagirated campaignes za CCM?habari ndio hiyo. PCCB kimeo mwanawane....:israel: