Kama kweli Bunge ni dhaifu,taja udhaifu Wa Bunge ili nao wajipime

masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,738
2,279
Kama kichwa cha habari kinavyosema,

Mimi naanza ya langu
Udhaifu ninaouona ni kila mbunge Wa CCM kusimama na kuisifia Serikali na kilanja mkuu wakati sio wajibu wao.

Natamani ifikie hatua Serikali iliogope Bunge kiasi kwamba wakiwa wanaleta hoja kupitia mawaziri basi waonekane wanabembeleza na sio kama sasa unakuta waziri hadi anajingamba mbele ya bunge kuwa ni lazima lipite hiyo unaonesha udhaifu maana ni Bunge ndio linaiamlia serikali na sio serikali inaliamlia bunge.
Yaani unakuta serikali inakosea wazi wazi lakini bado wabunge wanashabikia kuwa ni sawa.

Halafu udhaifu mwingine ni namna wanavyopitisha mambo Kwa mkumbo. Yaani Kwa kutamka kwa pamoja tu ..NDIOOOO.Ni bora wangekuwa wanapiga kura za siri tena wanazima hadi C.C.TV. ndio serikali igejitathimini kama wabunge Wa chama chake wanaiunga mkono serikali.

Kwa maana naamini kabisa kuna mambo ambayo Serikali inakosea na wabunge wanaona hili ila mda Wa kupiga kura ukifika mda Wa kupiga kura inabidi wote wakubali Kwa mkumbo na sio kiuhalisia.

Mimi nimejilipua na wewe fuatisha
 
Spika Wa bunge kufukuza wabunge Wa upinzani kwa maelekezo ya ikulu. wakati bunge in mhimili unaojitegemea
 
Bunge letu sio dhaifu, wanaosema Bunge dhaifu, wanalisingizia tuu. Bunge letu ni imara sana, mfano mzuri ni lile Azimio la Bunge kuwa Bunge Halifanyi kazi na Ofisi ya CAG.

Walipogundua wamechemsha kuwa Bunge halina uwezo wa Kutofanya kazi na Ofisi ya CAG, Spika akafanya kitendo cha ushujaa mkubwa, akaliweka Azimio pembeni, kimya kimya na kumeza kauli ya Kutofanya kazi na Ofisi ya CAG, kuwa sasa watafanya kazi na Ofisi ya CAG ila hawatafanyakazi CAG Prof. Mussa Assad, na Spika akasisitiza Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof Assad, kamwe haitapokelewa, unless kama itasainiwa na mtu mwingine na sio Prof. Assad.

Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof Assad ndio iliyowasilishwa Bungeni na ikapokelewa, huo ni ushajaa mkubwa sana, kitendo cha kutoa Azimio kuwa hufanyi kazi na CAG, kisha ukaahidi hupokei ripoti ya CAG, lakini ukaipokea. Huu ni ushujaa mkubwa sana
P
 
P. kweli P!!! Yaani udhaifu huuoni kabisa kabisa? Kaka kesho ni pasaka embu ongea kaukweli kidogo japo kwa leo tu maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu....!
Mkuu unakifahamu kikao cha kamati ya kinga,maadili na madaraka ya bunge? mzee anaogopa kusukumizwa tena huko.huenda wakati anahojiwa na ile mibunge ya ccm alikula viapo vya kusifia bunge mazima hatar.
 
P. kweli P!!! Yaani udhaifu huuoni kabisa kabisa? Kaka kesho ni pasaka embu ongea kaukweli kidogo japo kwa leo tu maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu....!
Ukweli ndio huo, Bunge letu ni imara sana na sio Bunge la mchezo mchezo. Mfano japo katiba Imeelekeza CAG hawezi kuhojiwa na yeyote, lakini Bunge imara kuliko katiba, likamuita kumuhoji!.

Hakuna ubishi kuhusu udhaifu wa Bunge hili, lakini ili kuonyeshea uimara kila atakayeita Bunge dhaifu, cha moto atakipata.

Huu ni uimara wa aina yake, kitu dhaifu cha ukweli kikionyesha uimara wa kuzuia kuitwa dhaifu.

haahaa Mkuu naona umeamua kutupa mawe gizani eh. kumbuka ndugai bdo anakufuatilia na lile likamati lake La bunge linaloadhibu wasio wabunge. Hatar sana
 
Kuruhusu serikali kuzima matangazo ya moja kwa moja kutoka Bungeni kwa sababu dhaifu kabisa.

Bunge lilitakiwa kutetea kwa sababu, kwanza kodi zitumikazo kurusha matangazo ni za waTanzania na pili ni haki ya Watanzania kupata habari muhimu na moja kwa moja kutoka kwa wawakilishi wao.

Huu ni udhaifu mkubwa ambao Bunge lili onyesha.
 
Bunge letu sio dhaifu, wanaosema Bunge dhaifu, wanalisingizia tuu. Bunge letu ni imara sana, mfano mzuri ni lile Azimio la Bunge kuwa Bunge Halifanyi kazi na Ofisi ya CAG.

Walipogundua wamechemsha kuwa Bunge halina uwezo wa Kutofanya kazi na Ofisi ya CAG, Spika akafanya kitendo cha ushujaa mkubwa, akaliweka Azimio pembeni, kimya kimya na kumeza kauli ya Kutofanya kazi na Ofisi ya CAG, kuwa sasa watafanya kazi na Ofisi ya CAG ila hawatafanyakazi CAG Prof. Mussa Assad, na Spika akasisitiza Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof Assad, kamwe haitapokelewa, unless kama itasainiwa na mtu mwingine na sio Prof. Assad.

Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof Assad ndio iliyowasilishwa Bungeni na ikapokelewa, huo ni ushajaa mkubwa sana, kitendo cha kutoa Azimio kuwa hufanyi kazi na CAG, kisha ukaahidi hupokei ripoti ya CAG, lakini ukaipokea. Huu ni ushujaa mkubwa sana
P
Hahahahaha mayala wewe ngoja ndugai akusikie utaitwa na kamati ya fukuza fukuza
 
Back
Top Bottom