Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,829
- 4,169
Nilishawahi kumsikia Bwana Sita akijitapa kuwa yeye ni Chuma Cha Pua. Alikuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio.
Sasa mafisadi wamemfanyizia.
Ninamuomba bwana Sita aoneshe uzalendo wake kwa Tanzania. Alichofanyiwa Sita na mafisadi ni usaliti mwingine kwa utawala wa mkwere kwa Watanzania. CCM na mafisadi wamedhihirisha tena ukweli kuwa wanadharau Watanzania kwani Watanzania kwa mamilioni walikuwa wanaomba kwa Mungu bwana Sita apewe nafasi nyingine ya kuliongoza bunge la nchi yetu. CCM (wasiozidi hata 100) wameweka watu wao. Watanzania wameachwa kwenye mataa. Wamedharauliwa. Kokoto (kauli ya Mkapa). Majuha (kauli ya Mkwere). Mabaamedi (kauli ya Makongolo Mahanga). Tumeachwa tukilia na kusaga meno.
Ninamuomba Sita ajitenge nao. Wabunge wote watiifu kwa Tanzania wajitenge na mafisadi. Wapige kura kuwakataa 'vibaraka wa mafisadi' waliopendekezwa kugombea nafasi adhimu ya Spika. Nchi hii haiwezi kubadilika bila watu 'wakubwa na wenye heshima' kama Sita kuthubutu.
Fanya hivyo Bwana Chuma Cha Pua. Sisi tutakuunga mkono.