Kama kuvaa helment, na kufunga mkanda ukiwa kwenye gari au pikipiki ni sheria, kwanini kuvaa life jacket ukiwa majini isiwe ni sheria?

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
2,114
4,798
Jamani kwanini serikali isiangalie hili swala?
Idadi ya life jackets iwe Sawa na idadi ya abiria wanaoruhusiwa kupanda, na iwe ni sheria ukiingia tu kwenye usafiri Wa majini unapewa boya na ukitaka kutoka ysnakusanywa!
Serikari tunaomba mtusaidie tunaumia sana
Yani inauma sana kwa hata yanayotokea
Kwa sasa kwenye vivuko vyetu life jackets zimekua kama mapambo tuu zimefungiwa na makofuli hii INA maana gani? Yani ajari ikitokea ndio MTU aanze kutafuta ufunguo?

Jamani serikali itathmini hili swala litasaidia japo kupunguza idadi ya vifo pale ajari inapotokea
Raisi Magufuli RAIA kwako hatuna amani tena
 
Jamani kwanini serikali isiangalie hili swala?
Idadi ya life jackets iwe Sawa na idadi ya abiria wanaoruhusiwa kupanda, na iwe ni sheria ukiingia tu kwenye usafiri Wa majini unapewa boya na ukitaka kutoka ysnakusanywa!
Serikari tunaomba mtusaidie tunaumia sana
Yani inauma sana kwa hata yanayotokea

Raisi Magufuli RAIA kwako hatuna amani tena
Najiulizaga hilo swali mara nyingi sana? Au labda hiyo life jacket ni expensive sana
 
Ni ajabu sana kwenye Meli kubwa life jacket zipo kila mahari engine room,vyumba vya kulala,sehemu ya kula na decker juu ndio za kumwaga wafanyakazi unakuta mpo wachache kuna mtu mmoja yeye anateuliwa kwa ajili ya fire extinguisher na life jacket au mambo ya safety tuu yaani kivuko kinabeba abiria 300 life jacket hakuna kabisa?
 
Duh unasikitisha walahi!
Kwa hiyo kwenye ndege pia uvae oxygen mask ukiingia, melini crew wote wavae life jacket! Uwiii are you serious? Unatisha walahi
 
Kama kuvaa helment, na kufunga mkanda ukiwa kwenye gari au pikipiki ni sheria, kwanini kuvaa life jacket ukiwa majini isiwe ni sheria?

Tujiulize, hao wanaoambiwa hayo, wanasafiri kwa vyombo gani, unakumbuka kuna viongozi waliwahi kupata ajali majini tena kwenye ziwa hilohilo, je kuna aliyejifunza kuchukua tahadhari baada ya pale?

Hizo pikipiki wameshindwa kabisa kusimamia suala la helmet

Kwenye mabasi kuna abiria wanakaliswa kwenye mfuniko wa injini hawana mikanda ya usalama, na askari wa usalama barabarani wapo wanaona hawachukui hatua

Majini nako tunaambiwa life jackets zimefungiwa store tena na makufuli, je nani wa kusimamia hilo kama viongozi wenyewe wa vyombo vya majini hawafiki kufanya ukaguzi?

Jamani kwanini serikali isiangalie hili swala?
Idadi ya life jackets iwe Sawa na idadi ya abiria wanaoruhusiwa kupanda, na iwe ni sheria ukiingia tu kwenye usafiri Wa majini unapewa boya na ukitaka kutoka ysnakusanywa!
Serikari tunaomba mtusaidie tunaumia sana
Yani inauma sana kwa hata yanayotokea

Raisi Magufuli RAIA kwako hatuna amani tena
 
Ishu sio lifejacket ila tatizo lipo kwenye meli zenyewe.
Meli chakavu zilizopo ziwa Victoria ni za kuziondoa kabisa
Tatizo sio meli kijana mdogo, tatizo liko kwa Watu ambao hawathamini uhai wa binadamu hata kidogo! MELI IMEJAZA MARA NNE KULIKO UWEZO WAKE!
Acha unafiki na kuwa mkweli kwenye hii issue hakika utapona walahi hivi hivi mtaangamia kwenye kila jambo, KUANZIA BODABODA MSHIKAKI NA MABASI KUJAZA walahi!
 
tatizo la meli watu wengi hufa kutokana na heka heka za kutaka kutoka kujiokoa na wengi hufa sababu ya msongamano hasa kama ikigeuka huku asilimia kubwa wakiwa ndani ya meli lakin naamini kwa wazo lako hilo itasaidia sana kupunguza ingawa yawezekana pia ukafa na lifejacket mwilini, ila wazo hili lingesaidia sana kupunguza vifo vya namna hii wazo zuri.
 
Nnachokijua kwa ziwa Victoria ukipanda Boat za mbao ni lazima uvae life jacket. Ukipanda meli or ferry kubwa si lazima, japo zinakuwepo na mhala zilipo hazijafungwa na kitu chochote.
 
Wewe unajua meliz zipo.victoria tu...na sio meli.nayosemea hapo kuna boti za kwenda saa nane life zipo ni wewe tu kuchukua uvae ...kuna boti ziwa tanganyika kwenda gombe life.zipo.na watu wanagaiwa wengi hawavai..tena boti za mbao local kabisa....
Meli gani hiyo hasa za ziwa Victoria huwa unapewa wewe na kuvaa life jacket? Acha kupotosha watu.
 
Hahahahaa Bajeti ndogo ya kununua life jackets za kutosha abiria wote maana vivuko vingi vinamilikiwa na serikali ila serikali hiyo hiyo boti binafsi wanawashupalia wawe na lifejacket kama zote ila wao serikali boats/ferries zao lifejackets za kutafuta na tochi.
 
Life jacket zenyewe zinakuwaga kama mapambo tu unakuta zimefungiwa hapo ndio huwa nachoka kabisa.
 
Jamani kwanini serikali isiangalie hili swala?
Idadi ya life jackets iwe Sawa na idadi ya abiria wanaoruhusiwa kupanda, na iwe ni sheria ukiingia tu kwenye usafiri Wa majini unapewa boya na ukitaka kutoka ysnakusanywa!
Serikari tunaomba mtusaidie tunaumia sana
Yani inauma sana kwa hata yanayotokea

Raisi Magufuli RAIA kwako hatuna amani tena
Mpaka hapo ni sheria, tatizo ni utekelezaji wa sheria yenyewe kwa mamlaka husika na watoa huduma hizi za majini. Yaani unakuta hadi meli kubwa life jackets zipo lakini zimefungiwa sehemu fulani tena kwa kufuli kubwa, sasa hapo ikitokea ajali mhusika aanze kutafuta funguo, afungue ndo zigawiwe kwa abiria, na mda huo lazima abiria watagombania ili kila mmoja awahi kupata hiyo life jacket, hii itasababisha kukosekana kwa stability na lolote laweza kutokea. Huwa naona meli zinazotoa huduma ya usafiri kati ya ukerewe na mwanza ziku zote life jackets huwa zimefungwa kwa makufuli mazito kabisa.

lakini kuna maeneo wanajitahidi. Niliwahi kuona kituo kimoja kuna hawa vijana wa suma JKT wako wanahakiki kila abiria anayepanda anapewa life jacket yake na ng`ambo ya pili pia wapo kuhakiki kila anayeteremka anateremka na life jacket alokuwa amevaa.
 
Sheria za usafiri majini haziruhusu chombo kuondoka bila ya kuthibitisha kuwa life jackets zinawatosha wafanyakazi na abiria wote
 
Nnachokijua kwa ziwa Victoria ukipanda Boat za mbao ni lazima uvae life jacket. Ukipanda meli or ferry kubwa si lazima, japo zinakuwepo na mhala zilipo hazijafungwa na kitu chochote.
Si kweli zinakuaga zimefungiwa tena na kufuli juu
 
Ukimsikiliza yule majeruhi alisema Kile kivuko mwendeshaji alikata kona ghafla kulikuwa na gari aina ya Center kwa hiyo kile kivuko baada ya kukata kona ghafla kililala upande ile gari nayo ikaelekea huko huko ikasababisha kile kivuko kisirudi kikaenda moja kwa moja na kupinduka.
 
Mpaka hapo ni sheria, tatizo ni utekelezaji wa sheria yenyewe kwa mamlaka husika na watoa huduma hizi za majini. Yaani unakuta hadi meli kubwa life jackets zipo lakini zimefungiwa sehemu fulani tena kwa kufuli kubwa, sasa hapo ikitokea ajali mhusika aanze kutafuta funguo, afungue ndo zigawiwe kwa abiria, na mda huo lazima abiria watagombania ili kila mmoja awahi kupata hiyo life jacket, hii itasababisha kukosekana kwa stability na lolote laweza kutokea. Huwa naona meli zinazotoa huduma ya usafiri kati ya ukerewe na mwanza ziku zote life jackets huwa zimefungwa kwa makufuli mazito kabisa.

lakini kuna maeneo wanajitahidi. Niliwahi kuona kituo kimoja kuna hawa vijana wa suma JKT wako wanahakiki kila abiria anayepanda anapewa life jacket yake na ng`ambo ya pili pia wapo kuhakiki kila anayeteremka anateremka na life jacket alokuwa amevaa.
Ni vyema serikali ikatilia mkazo hili swala kwani itasaidia kupunguza idadi ya vifo pale ajari inapotokea
 
Back
Top Bottom