Kama kunajengwa Madarasa Mapya, Vipi kuhusu Ajira mpya za Walimu?

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
478
962
Nawasalim kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Kimsingi sasa hivi serikali ipo katika mchakato mkubwa wa kitaifa wa kujenga madarasa 15,000 nchi nzima, ikiwa madarasa 12,000 kwaajili ya watoto wanaoanza mwakani kidato cha kwanza na madarasa 3,000 kwajili ya shule shikizi za msingi.

Ujenzi huu wa madarasa ya wanafunzi umekuwa very sensitive kiasi kwamba mpaka wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi kutoruhusiwa kusafiri wabaki maeneo yao ya kazi wasimamie ujenzi, na kiongozi atatoka nje ya mkoa au wilaya endapo tu akiwa na kibali cha mh Rais.

Katika hali ya uzito zaidi tumeona na mh Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu akitaka kukabidhiwa madarasa hayo tarehe 15 mwezi Disemba mwaka 2021.

Sasa swali la msingi ikiwa ujenzi umepamba moto wa madarasa ili idadi kubwa ya wanafunzi wetu wasome wakiwa madarasani je mh Waziri wa Tamisemi, Mh Rais ni vipi mchakato wa kuajiri walimu wapya ili watoto wetu wapate walimu wa kuwafundsha katika madarasa hayo mapya?

Ni lini ajira mpya za walimu zitatoka ili kuondoa hadha ya uhaba wa walimu mashuleni ukizingatia madarasa yanaongezwa? Au hawa watoto wataenda kufundishwa na vibwengo huko kwenye madarasa mapya?
 
Ni kwel mkuu ,huu ujenzi wa madarasa lazima uendane na kuajiri walam wapya , naomba serekali iyatupilie mbali Yale mawazo ya ndugai
 
Haya na utuambie wenye mbunge wa wapi? Au kama maswali hayo yaliwahi ulizwa na mbunge wako, au hata kama ataweza kuyauliza!
 
Wasisahau kujenga nyumba za walimu, sio wajenge madarasa tu kana kwamba hao wanafunzi ndani ya madarasa watafundishana wenyewe
 
Wasisahau na kujenga nyumba za wafanyakazi wanapojenga ayo madarasa. Najiuliza shule nyingi za mkoloni au nyerere zilijengwa pamoja na nyumba za wafanyakazi iweje sasa tushindwe
 
Wajenge tuuuu..
Wakimaliza kujenga wajenge nyumba za walimu..
Aaaaafuuuu kwenye campenii sela yao iwe tutawaajir walimu wakutosha ili wakakae kwenye nyumba tulizo zijenga,,,

Sisiemu hoyeeeeeeeee..
 
Back
Top Bottom