Kama kuna mtu yeyote wa TBS humu ndani, naomba kufahamu kuhusu Endorsed/Approved Vehicle Inspectors in Italy

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,624
2,000
Guys,

Sallaam! Kuna gari inataka kuwa shipped kutoka Italy to Dar es salaam. Utaratibu wa TBS ni kwamba, kabla gari haijanusa Bongo, inatakiwa kukaguliwa huko huko inakotoka unless kama upo tayari kutandikwa penalt.

So, kama kuna mtu yeyote wa TBS humu ndani, naomba kufahamu kuhusu Endorsed/Approved Vehicle Inspectors in Italy. Nimeshawa-email lakini bado sijapata feeback!

Aidha, kama kuna yeyote humu jamvini mwenye namba ya simu ya mkononi ya mtu wa TBS, basi naomba msaada wa hiyo namba niongee na muhusika kuwaambia wacheki email yangu! Kwa bahati mbaya, website ya TBS imeorodhesha namba za mezani tu ambazo, sio tu ni bit expensive lakini vile vile hazi-connect!

Natanguliza shukrani zangu!

UPDATE:

Nimeshamalizana Nao!

Kwa faida ya Wengine:-
Unapoagiza gari toka kokote duniani ambako hakuna Wakala wa TBS wa ukaguzi, then unaruhusiwa kuingiza gari yako nchini kabla ya kukaguliwa lakini ikishafika TZ, kabla ya yote inatakiwa kukaguliwa na NIT.
 
myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,624
2,000
Hoyaa Moderator,

Hiyo title hapo juu imekumbwa na maswahibu gani tena?! Title niliyoweka ilikuwa simple and clear:

ATTN: TANZANIA BUREAU OF STANDARDS-- PRE-IMPORT VEHICLES INSPECTION FROM ITALY.

Hiyo ndiyo title ambayo niliweka!
 
myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,624
2,000
Wadau, bado naomba msaada wa mobile contacts ya mtu wa TBS manake nahisi emails zao zimefungiwa😀😀
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,431
2,000
Ninavyo fahamu kama nchi unayoagiza gari Tbs hana wakala , huwa wanaruhusu kuleta gari na wao hukagua likiwa nchini, unaandika tu barua kuelezea hali halisi

Penalt huwa inahusika kama nchi unayotoa gari Tbs wana wakala wa kukagua lkn wewe hukutaka kukagua huko.
 
Na ndicho nilichomaanisha! Kwahiyo moja ya majibu ninayotarajia kutoka TBS ni official response ikiwa wana Wakala Italy au hawana ingawaje I doubt ikiwa wanae!

Lakini siwezi ku-risk kwa ku-assume hawana Wakala wakati si ajabu wanae!

Ilikuwa ni issue ndogo sana ambayo ningeweza kujibiwa jana ile ile; sema ndo hivyo tena!
 
Tembo Jeuri

New Member
Nov 14, 2018
4
45
Na ndicho nilichomaanisha! Kwahiyo moja ya majibu ninayotarajia kutoka TBS ni official response ikiwa wana Wakala Italy au hawana ingawaje I doubt ikiwa wanae!

Lakini siwezi ku-risk kwa ku-assume hawana Wakala wakati si ajabu wanae!

Ilikuwa ni issue ndogo sana ambayo ningeweza kujibiwa jana ile ile; sema ndo hivyo tena!
Njoo PM nikutumie namba ya jamaa wa TBS
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom