Kama kuna mtu hauna malengo ya kuja kumuoa basi achana nae

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
Leo Tujifunze kitu

Kama una date binti wa umri wa kuanzia miaka 23 huna mpango wa kumuoa fanya jambo la kiungwana na kumuambia ukweli.

Sikuambii umuambie kua humtaki na hutaki kuoa bali muambie kua wewe si muoaji na unaona kua utampotezea muda wake bure na kuja kumuumiza.

Ongea kiungwana na ikishindikana muache hata kibabe. Hii ni kwasababu mwanamke anawekeza vitu vingi katika mahusiano, anawekeza akili yake, mali zake, hisia na kubwa kabisa anawekeza umri wake katika mahusiano.

Unampunguzia uwezekano wa kukutana na mtu sahihi kwa kuendelea kumdanganya. *Kwa Mwanamke,* ```"Age is not just a Number, Age is Everything".```

Wakati ukimuacha wewe utatafuta Binti mdogo zadi yake, yeye atalazimika kutafuta Kijana mwenye Umri Mkubwa zaidi yake. Ndiyo ilivyo sote Wanaume na Wanawake huangalia Umri katika Mahusiano.

Ukimchezea na kumuacha akiwa katika Umri wa Miaka 30, inamaana atafute kijana mwenye Umri kuanzia Miaka 32 ambaye bado ni Single.

Wako wachache sana wa namna hiyo, sisemi kua hawezi kupata, hapana.. Nasema utampa Wakati Mgumu na Uhuru wa Kuchagua.

Kuna Umri ambao Mabinti wengi huamua Kuolewa tu, si kwasababu ya Mapenzi bali kwakua hawana namna wanaona kusubiri Mtu Sahihi watapishana na Kalenda.

Badilika, haikufanyi Mwanaume zaidi kwa kumpotezea Binti wa watu Miaka Mitano halafu unamuambia ```"Wewe si Type yangu".``` Fanya jambo la Kiungwana na Malizaneni Mapema.

Lakini najua kuna Mabinti ambao hawasikii wakiambiwa kuwa mambo yameisha, Mlazimishe asikie na Usimtumie na Kumuumiza kwakua anakupenda
 
Mtu anakaa na wewe miaka sita hata kwao hupajui. Na ww mwanamke umeridhika tu hata hukurupuki kuuliza future yenu n nn. Kwakwel unahitaj maombi ya gwajima
Watu Kama hao wanatakiwa kupigwa kofi la Kichwa ili Kurestore Libichwa lake
 
Tatizo mabinti wengi hawasomi alama za nyakati.ukiwa una pesa hata umwambie sina mpngo wa kukuoa atakuganda tu.
 
I don't know the question but the answer is SEX. Kuoa au kutokuoa haiondoi umuhimu wa sex katika mahusiano; kuoana syo lazima bali sex.
NB: Mapenzi matamu ni kati ya mwanaume na msichana; siyo mwanaume na mwanamke. Never underestimate the power of sex.
 
Dah hii nibusara iliyotukuka, ila mimi hii imenitokea nampaka hivi sasa bado cjajua nn chakuamua nahisi nahuruma yangu inachangia, kuna bint nipo nae ila kiukweli cna malengo nae nayeye anajua hilo nadhani kwasababu ishamwambia nahata msichana niliyenae anamjua nandio ninamalengo nae, ila chaajabu huyu binti hataki kuamini nachomwambia yeye anachodai kuwa anaamini mimi ndiye mme wake wahapo badae ila kiukweli mimi cna malengo nae naishamwambia sana nanilishajaribu kumuacha ila amekuwa akinililia sana najikuta huruma inanishika naendelea kuwa nae. Sasa mkuu kama huyu utamfanyaje? naumri wake bado ajafikisha 25
 
Back
Top Bottom