Kama kuna mtu anahitaji ushahidi kuwa watendaji serikalini huwa hawafanyi utafiti, basi ni huu hapa

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,636
8,774
Miezi kadhaa iliyopita serikali iliamua kuongeza kodi maradufu (kama si zaidi) kwenye mabango ya matangazo (billboards na hata kwenye magari).

Aliefikiri hivyo obviously hajui the first thing about business management. HAKUNA mfanyabiashara HATA MMOJA atakayelipa shilingi moja kama haimpi return inayozidi shilingi moja.

Advertising costs itabebwa tu na mfanyabiashara kama manufaa yake yatazidi alicholipa. Sasa serikali ya Rais Magufuli imepandisha mara kadhaa ushuru wa mabango; nini kimetokea?

Wafanyabiashara wameondoa mabango yao which means hata hicho kilichokuwa kinalipwa mwanzoni kabla ya "uduwanzi" wa kupandisha ushuru hakilipwi tena.

Kwa manufaa yenu waimba mapambio; naomba msisadiki maneno yangu bila ya kufanya uchunguzi ufuatao:

Hebu angalia magari unayokutana nayo barabarani, ni mangapi yenye mabango sasa hivi?
 
Binafsi,
Nmeondoa bango la biashara dukan kwangu baada ya watu wa Manispaa kunitaka nilipie Ada ya bango sh.475,000 kwa mwaka.

Afu wanasema inatakiwa ilipwe Double, maana wanasema eti wameanza kuliona tangu mwaka juzi na Halijalipiwa chochote.

Huu Ni Uhuni na Haukubaliki kwa Namna yoyote ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DeepPond, Hebu tuelimishane Kidogo, ni mabango ya aina gani yanayostahili kulipiwa kodi? Na ni mabango yanayokuwa maeneo yapi yanalipiwa kodi?

Nilidhani yanayolipiwa ni yale yanayokuwa maeneo ya stendi, kwenye stem za taa za barabarani na maeneo yanayofanana na hayo

Kumbe hata nikibandika bango linalotanga biashara yangu dukani kwangu natakiwa kulilipia?
 
Sio dukani kwako tu, hata ukiweka bango nyumbani kwako (nyumba uliyoijenga wewe mwenyewe) utatozwa kodi ya bango.
 
Back
Top Bottom