Kama kuna mtu anadhani anaweza kuua CHADEMA basi ni lazima atakuwa Mwehu , mwenye akili timamu hawezi kuwaza kwa kiwango duni kiasi hicho

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,618
218,040
Wakuu natanguliza salamu , baada ya salamu najikita kwenye mada bila kuremba , kwa mtu yeyote anayedhani anaweza kuua Chadema kwa njia yeyote anayoitumia , iwe biashara ya binadamu , iwe kwa kutumia MA DC , MA RC ama labda kwa kutumia polisi au watu wasiojulikana basi afya yake ya akili itazamwe upya
IMG-20180807-WA0008.jpg

Baada ya kwenda Lusaka nchini Zambia kwa usafiri wa anga na kuhudhuria onyesho la Music la Koffie Olomide Mopao ( ikumbukwe kwamba mimi ni Kijana Tajiri na mpenzi wa kutupwa wa music wa kikongo , ambao kwa sasa si rahisi kuupata nchini Tanzania baada ya mapromota wote kufirisika kutokana na matatizo makubwa ya uchumi ) nikaamua kufanya ziara maalum kwa kutumia gari ili kukagua uhai wa Chadema , Nimepita Nyanda za Juu kusini , kwa maana ya mikoa ya Rukwa , Songwe , Mbeya na wilaya zake zote , Iringa , Njombe na kumalizia mkoa wa Ruvuma , ama kwa hakika ukiwa na akili timamu huwezi hata kuthubutu kufikiria kuua chadema achilia mbali kutamka hadharani.
IMG-20180807-WA0007.jpg


Mizizi iliyojikita nayo Chadema kwenye eneo hili si tu kwamba si rahisi kuing'oa bali haiwezekani kamwe ! Chadema inaongoza mitaa , kata na halmashauri kadhaa na jambo kubwa zaidi ni namna wananchi wanavyoheshimu uongozi wa chadema kwenye maeneo yao
IMG-20180807-WA0010.jpg


Taarifa nilizokusanya zinaonyesha kwamba ile mbinu ya kizamani ya kuhonga vibaba vya unga ili kushawishi wananchi kuunga mkono ccm kwenye ukanda huu imegonga mwamba kutokana na uwezo wa wananchi wa eneo hilo kujitosheleza karibu kwa kila kitu hivyo kuwa na uwezo wao wa kiuchumi
IMG-20180807-WA0009.jpg


Nguzo kuu ya Chadema ni utulivu wa viongozi wake unaotokana na weredi na usomi wao , kama unataka kupoteza muda wako endelea na mawazo mgando ya kudhani unaweza kuua chadema
 
Mnatumia nguvu kubwa sana katika kuhalalisha madudu ya pale Ufipa. CCM ina madhambi yake mengi tu lakini CDM imeonyesha kwamba ikipewa nafasi ya kuongoza nchi tofauti itakuwa ni ndogo sana.
 
Mnatumia nguvu kubwa sana katika kuhalalisha madudu ya pale Ufipa. CCM ina madhambi yake mengi tu lakini CDM imeonyesha kwamba ikipewa nafasi ya kuongoza nchi tofauti itakuwa ni ndogo sana.
hushangai kwanini kila anayenunuliwa ni lazima apokelewe na Polepole ! Mnatumikishwa humu weeee !! halafu wasaliti akina Kafulila wanaula !
 
Kamanda, unataka CHADEMA ife mara ngapi? Kifo hutokea mara moja tu
Liz born upo? Long time sana sijakusoma humu! Shida ni bundle au ni nini mbaya? Cdm mnaiua mitandaoni bali kwenye mioyo ya watu imejaa tele! Ulishawahi kuliona tabasamu la mbwa? Hilo ndilo mnalopewa ccm na wanacdm kuwaonyesha kuwa mpo pamoja machoni lakini siyo moyoni! Anzia kwa vijana wa rika zote na wasomi wanaohangaika kitaa kutafuta ajira na familia zao zilizojikimu kuwasomesha wakitaraji kupata ajira wote ni cdm kindakindaki na bado hujagusa kundi la wafanyakazi na wafanyabiashara! Mbona mtataabika sana kwa kukurupuka bila kufanya utafiti! Sina chama zaidi ya kile cha kufa na kuzikana!
 
Back
Top Bottom