Kama kuna mtu amepitia madhira kama ya Mbowe basi amnyoshee mkono

Mto wa mbu

JF-Expert Member
Aug 8, 2021
2,200
3,008
Kuna kitu nakiona binafsi naumia Sana, yaani watu hasa CCM na vyama shikizi wanatumia sakata la Covid-19 ili kumdhiahaki Mbowe na kimdharirisha. Sasa Kama Kuna mwanasiasa yeyote Tanzania ambaye amapitia haya Basi amnyooshee Mbowe kidole, lakini Kama wewe ni keyboard worriors ata mahabusu hujawai kulala. Funga Domo lako

- Mbowe alitumia muda mwingi kutafuta vijana vyuoni, kuwasaidia Kampeini, kifedha na kweli baadhi ya hao vijana walipata madaraka na umaarufu kupitia Chadema ya Mbowe, mtu Kama Nassari, Mdee, Nusrat,Zitto, Mashinji,Lijualikali etc wote Mbowe aliwashika mkono Ila mwishoni walimsaliti.lakini hakukata tamaa.

-Mbowe alifilisiwa Mali, Account zake zikafungwa, Mashamba yake yakafyekwa, Billicanas ikavunjwa, Gazeti lake likafungwa, hotel zake zilikuwa zinatizwa Kodi Kali lakini bado Mbowe hakukata tamaa.

-wabunge wa chama chake wakanunuliwa kina Silinde, Lijualikali, Mollel, Waitara, etc katibu mkuu wake Mashinji akanunuliwa, lakini Mbowe hakukata tamaa.

-Mbowe alipewa kesi ngumu ya Ugaidi, amesota jera miezi nane, hakuwapigia magoti watawala Hadi wakamuachia kwa aibu kubwa. Hakuna ata mtanzania ATA mmoja aliyeandamana ata kushinikiza Mbowe aachiwe, wote waliufyata wa kuwa na keyboard worriors. Na kuchafua madaraja na Vibao kuwa Mbowe sio gaidi.

Mbowe ni tajiri, hategemei siasa ili mkono uende kinywani. Lakini bado amepambana na kupigania haki na Katiba mpya, Hadi watawala wanabuni mbinu za kijinasua na movement za katiba zilizoanzishwa na Mbowe, ndo maana mnaona vikosi kazi vya Mchongo

Narudia Kama Kuna Mwanasiasa hapa Tanzania amepitia madhira na misukosuko ya kisiasa aliyopitia Mbowe mtajeni na Mnyooshe Mbowe kidole.

Ila Kama Ni keyboard worriors shut up and keep quiet.
 
Pole sana Joy... I can see your sorrows but mind you... Sympath ya wana CCM ndiyo iliyomtoa Mboe koro koroni.
Hakuna mtu mwenye chuki na Mboe as a person... Ni hoja za kisiasa ndio zinaibua yote hayo!
 
Mbowe amepitia Kama ya Kubenea alipewa mpaka tindikali!

Mbowe kapitia ya Lissu kupigwa Risasi?

Mbowe muweke kundi la Nusrat hanje na Mdee kuwekwa ndani tu !
 
Mbowe amepitia Kama ya Kubenea alipewa mpaka tindikali!

Mbowe kapitia ya Lissu kupigwa Risasi?

Mbowe muweke kundi la Nusrat hanje na Mdee kuwekwa ndani tu !

..lakini Ccm inatia aibu sana.

..inatesa mpaka wanawake wa upinzani?

..sikuwahi kusikia mkoloni mngereza amewaweka mahabusu wakina mama wa Tanu kwa mfano Bibi Titi Mohamed, na wengine.

..hivi ina maana Mkoloni alikuwa na utu kuliko wana-Ccm?
 
Kuna kitu nakiona binafsi naumia Sana, yaani watu hasa CCM na vyama shikizi wanatumia sakata la Covid-19 ili kumdhiahaki Mbowe na kimdharirisha. Sasa Kama Kuna mwanasiasa yeyote Tanzania ambaye amapitia haya Basi amnyooshee Mbowe kidole, lakini Kama wewe ni keyboard worriors ata mahabusu hujawai kulala. Funga Domo lako

- Mbowe alitumia muda mwingi kutafuta vijana vyuoni, kuwasaidia Kampeini, kifedha na kweli baadhi ya hao vijana walipata madaraka na umaarufu kupitia Chadema ya Mbowe, mtu Kama Nassari, Mdee, Nusrat,Zitto, Mashinji,Lijualikali etc wote Mbowe aliwashika mkono Ila mwishoni walimsaliti.lakini hakukata tamaa.

-Mbowe alifilisiwa Mali, Account zake zikafungwa, Mashamba yake yakafyekwa, Billicanas ikavunjwa, Gazeti lake likafungwa, hotel zake zilikuwa zinatizwa Kodi Kali lakini bado Mbowe hakukata tamaa.

-wabunge wa chama chake wakanunuliwa kina Silinde, Lijualikali, Mollel, Waitara, etc katibu mkuu wake Mashinji akanunuliwa, lakini Mbowe hakukata tamaa.

-Mbowe alipewa kesi ngumu ya Ugaidi, amesota jera miezi nane, hakuwapigia magoti watawala Hadi wakamuachia kwa aibu kubwa. Hakuna ata mtanzania ATA mmoja aliyeandamana ata kushinikiza Mbowe aachiwe, wote waliufyata wa kuwa na keyboard worriors. Na kuchafua madaraja na Vibao kuwa Mbowe sio gaidi.

Mbowe ni tajiri, hategemei siasa ili mkono uende kinywani. Lakini bado amepambana na kupigania haki na Katiba mpya, Hadi watawala wanabuni mbinu za kijinasua na movement za katiba zilizoanzishwa na Mbowe, ndo maana mnaona vikosi kazi vya Mchongo

Narudia Kama Kuna Mwanasiasa hapa Tanzania amepitia madhira na misukosuko ya kisiasa aliyopitia Mbowe mtajeni na Mnyooshe Mbowe kidole.

Ila Kama Ni keyboard worriors shut up and keep quiet.

Kwahiyo baada ya kuteseka hivyo sasa hivi amenyosha mkono. Amepewa nini?

Kazi yake sasa ni kumtukana JPM, sio kujali mfumuko wa bei, bei za pembejeo, ujenzi,maisha ya Watanzania wengi, kuwapigania Watanzania.

Unatoka jela unaenda ikulu, uliitwa gaidi, ila hujali. Anapigania tumbo lake, famikia yake.
 
..alinywesha sumu na nani?

..Jpm angekuwa amenyweshwa sumu angemshughulikia mbaya wake baada ya kuwa raisi.

..kwa maoni yangu madai ya Jpm na Dr.Mwakyembe kwamba walipewa sumu yalikuwa ni uzushi.
Mbowe hajapitia madhila ya kutisha kama JPM kuwekewa sumu ili afe.

Mbowe anawekwa ndani siku mbili tatu anajiita kamanda anauza chama.

Angekuwa jembe kama Magufuli aliyepambana na watu wazito wa dunia kina acacia si ingekuwa balaa
 
Mbowe ni Shujaa

FB_IMG_1589397986327.jpg
 
Magufuli alinyweshwa sumu lakini hakuiuza CCM kama mbowe anavyoiuza Chadema sasa hivi
Unatakiwa usaidie jeshi la polisi.

- Magufuli kunyweshwa sumu.

- Mbowe muamala kusoma.

Peleka ushahidi wa hizo tuhuma zako polisi.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Suala hapa sio Mbowe kutoaminiwa, tatizo ni hekima yake iliyopitiliza naona inaanza kutumiwa vibaya na CCM kwa manufaa ya serikali yake.

Tangu waanze mazungumzo na Samia hakuna lolote lililofanyika kwa upande wa serikali, hata mikutano ya siasa tu iliyopo kisheria bado, hii maana yake nini?

Hapo hapo unawaona Covid bado wanakingiwa kifua na Spika wa bunge la CCM, na mawakili wa serikali, hii maana yake nini?

Uvumilivu una kikomo, atleast waoneshe wako tayari kutenda wanachozungumza kwa kuruhusu jambo moja ili kuleta kuaminiana, lakini kila siku wanapiga hadithi tu ikulu huku mambo yakizidi kuwa hovyo kiutendaji.

Huku yeye Mbowe akiambiwa waambie wale wa mitandaoni wanyamaze, anakuja kutuambia, aamke sasa, nae awape wenzie conditions, wakishindwa kuzifuata hayo mazungumzo bora yafe.
 
Narudia tena ukiona adui wako anakusifia jua kuna mahali unakosea, na ukiona anakushambulia jua umekanyaga yenyewe
 
Back
Top Bottom