Kama kuna moto mbona tayari tupo motoni, tusilichukulie 'serious' hili andiko

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
Wanasema baada ya haya maisha kuna upembuzi. kuna watakaopimwa na mzani wao kudondokea peponi (naskia kuna raha sana huku) na wapo watakaodondokea motoni (simulizi zake humtisha hata muuwaji huku duniani).

Je, mungu alituumba tuje kuishi kwa raha au shida? wakati huo unaambiwa sio kua masikini ndio utauona ufalme wa mbingu na wala siyo kuwa tajiri basi ni wa motoni hapo siku ya mwisho. Wapo matajiri wanatenda mema sana na hivyo ufalme wa mbingu pia ni wao (hawa watakula raha mbinguni na duniani wanakula)

Wapo masikini na wataingia motoni kwakua hawana moyo safi (heri wenye moyo safi kwa maana watamwona mungu) kosa lao ni kutotimiza yampasayo kutoka kwa kile anachohitaji mungu.

Masikini maisha yake tu ya duniani ni moto tosha.

Serikali yake inamchoma

Kazaliwa maskini anakufa maskini na sio kama alilala, anataabika kupambana ila kama ilivyo kawaida na kuna baadhi ya nchi kama India ukizaliwa koo maskini utakufa masikini au Kenya na Uganda. Uwe slum dweller alafu uje kuwa tajiri, si rahisi japo inawezekana.

Kuzaliwa masikini na kuufikia utajiri sio kazi ndogo na wengi wanakufa wakiwa masikini au wakipata kidogo vinapotea na wanakufa maskini kwasababu (poor people dont have time for investment, because poor people are too busy trying not to be poor) watu maskini hawana/hatuna muda wa kuwekeza kwakua tunapambana tusiwe maskini - haswaa kwenye mambo ya misosi, TULE TUISHI JAMANI.

Maisha yake yanamchoma

Pale masikini anapojitahid kuutafuta utajiri anatabika sana. Wengi wamechomwa moto wakiwa wanautafuta utajiri hahaaa huyu akifa anakutana na moto mwingine huko juu kwaajili ya dhambi zake.

Dini yake pia inamchoma (anatia huruma sana masikini)

Baadhi ya dini huyu masikini akijaribu hata kuiba anakatwa mkono. Angezaliwa tajiri huyu sidhani kama angechomoa simu ya elfu 15 mfukoni mwa mtu.Hayo hayawezi kumpata tajiri.

* Tajiri yupo karibu na serikali
* Jamii inamuabudu na
* Katika nyumba za ibada yeye huwa juu na huonekana hana dhambi na anaaminika kabisa ila walau yeye tajiri mtenda dhambi atakavyokutana na moto mbinguni (atakua amebalance), ila masikini mwenye dhambi duniani atakapokutana na moto mbinguni itakua ni KASHESHE.

Maskini anaenda kukutana na moto wa pili mbinguni) nadhani maskini huyu anataman hata kusiwe na uzao upya baada ya kifo (reincanation)

*Kama kuna moto mbona tayari tupo motoni*
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom