Kama kuna mgao wa Umeme si mtangaze tu, mnamuonea nani aibu wakati Nchi kweli ni masikini?

Hata mimi nashangaa, Dodoma hakuna hiyo habari umeme upo Saa 24 siku 7 za wiki!
Unatembea mitaa yote ya Dodoma?! Kuna wakati nilienda Dar es salaam na kule nilikofikia ilikuwa kila wiki lazima wakate umeme siku za Jumanne lakini maeneo mengine umeme ulikuwa kama kawaida. Hata hivi sasa, huko wanakolalamika suala la umeme haimaanishi maeneo yote, kwa sababu ndivyo inavyokuwa; leo huku, kesho kule. Mwanzoni nilidhani ni Temeke tu kwavile Temeke na kwenyewe wanaonewa sana. Cha ajabu jana, Flavian Matata akawa analalamika kama alivyolalamika mdau hapo juu. Imeniwea ngumu kuamini kama Flaviana nae anaishi Temeke.
 
Ukweli ambao TANESCO hawataki kuusema wazi ni kuwa, hali ya shirika kifedha ni mbaya sana, hawana tena pesa za kuwalipa wazabuni wanaoweza kutuuzia umeme wa dharula wakati umeme wa uhakika unapokuwa hautoleshelezi kwenye gridi ya taifa. Sasa TANESCO inakufa na tai shingoni.

Kwa sasa TANESCO wamepewa maelekezo ya kukusanya pesa za madeni ya wadaiwa sugu kwa nguvu zote ili zitumike kununua umeme wa dharula, maana hazina hawatatoa hata senti tano. Mbaya ni kwamba wadaiwa sugu ni taasisi za umma, kama polisi, jeshi, magereza, ikulu, halmashauri, wizara, shule, vyuo na hospitali za serikali. Yaani hapo ni sawa na kutoboa mtumbwi ambao wewe ni abiria pia.
Hahahahah hii nimeipenda.
 
Hali ni tete
Unatoa pesa mfuko wa shati unaipeleka kwa surualee
 
Back
Top Bottom