Kama kuna mgao wa Umeme si mtangaze tu, mnamuonea nani aibu wakati Nchi kweli ni masikini?

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
7,277
2,000
Wakuu Salaam;

Hivi Serikali mnaona aibu gani kutangaza kuwa kuna mgao wa umeme nchini?

Kila siku mnakata umeme mnarudisha muda mnaotaka, jana mmezima kuanzia asubuhi mkarudisha jioni na leo mmeuacha kuanzia asubuhi mmekata tena jioni hii!

Hii nchi ni maskini bado, tusiaminishane kila kitu mnaweza, kama Umeme ni wa mgao si mseme tu, shida iko wapi?

Mficha uchi hazai.

Rais wewe ndiye unasimama na kipaza sauti kusema mambo yako safi! Safi kwa mgao?
 
fredericko

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
2,397
2,000
Uchumi wetu wa kati ni inversely proportional na tunayoyaona. Ni aibu nchi ina 60+years mpaka leo haina umeme wa uhakika
Very shameful
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,494
2,000
Ukweli ambao TANESCO hawataki kuusema wazi ni kuwa, hali ya shirika kifedha ni mbaya sana, hawana tena pesa za kuwalipa wazabuni wanaoweza kutuuzia umeme wa dharula wakati umeme wa uhakika unapokuwa hautoleshelezi kwenye gridi ya taifa. Sasa TANESCO inakufa na tai shingoni.

Kwa sasa TANESCO wamepewa maelekezo ya kukusanya pesa za madeni ya wadaiwa sugu kwa nguvu zote ili zitumike kununua umeme wa dharula, maana hazina hawatatoa hata senti tano. Mbaya ni kwamba wadaiwa sugu ni taasisi za umma, kama polisi, jeshi, magereza, ikulu, halmashauri, wizara, shule, vyuo na hospitali za serikali. Yaani hapo ni sawa na kutoboa mtumbwi ambao wewe ni abiria pia.
 
Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
5,219
2,000
Ukweli ambao TANESCO hawataki kuusema wazi ni kuwa, hali ya shirika kifedha ni mbaya sana, hawana tena pesa za kuwalipa wazabuni wanaoweza kutuuzia umeme wa dharula wakati umeme wa uhakika unapokuwa hauteleshelezi kwenye gridi ya taifa. Sasa TANESCO inakufa na tai shingoni.

Sheria ilitoka wakatiwe sasa kama wanaogopa imekula kwao
 
Cha ajabu jiwe anatangaza hali shwari ilihal umeme siku nzima hamna.

Kama hadi ikulu inadaiwa bill...umaskini ni mkubwa sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom