Kama kuna mfanyakazi wa HESLB anifanyie connection rufaa yangu ifanikiwe nitamshukuru sana

Kuna mtu ni mfanyakazi wa heslb alinambia atanisaidia kuappel ishu ya bodi nipate mkopo kwa 100% akanambia kunisaidia nimpe elfu 30

Kweli nilimpa lakini kilichotokea hakunisaidia chochote alichukua hela hakuhangaika chochote kile

Nimeteseka sana, leo nimeingia mwaka wa 3 ada, kodi vinaniumiza kichwa, nina asilimia 40 tu ya mkopo

MwanaJf yoyote yule anayeweza nisaidia rufaa yangu ya bodi ikafanikiwa nikapata hata 100 ili tu nimalize mwaka na mm kwa kuweza kumudu kulipiwa ada na bodi ningemshukuru sana


Najua humu watu wa heslb mpo pls nisaidieni mwenye connection
Kuna mwamba aliambiwa atoe 1 M afanyiwe mchongo loan board matokeo yk kapigwa chini na hela hakurudishiwa.
 
Kinachotoa mikopo HESLB sio mtu ni system ambayo Iko programmed na vigezo hivyo hakuna mtu anaeeza kukusaidia kupata mkopo.

Hata kama ungekua Shemeji yake Badru au Ngole hawezi kukubeba hivyo usiruhusu mtu akuanbie atakusaidia hiyo kitu haipo.

NB
Kufahamiana na Board member wa VODACOM/TIGO/AIRTEL nk hakuwezi kukusababisha kununua Salio ilihali huna pesa kwenye akaunti yako.

Najua vijana wengi mnateseka kwa kudhani connection itakutoa ukweli mchungu ni kwamba haiwezi kukusaidia chochote.
 
Back
Top Bottom