Kama kulonga JK kalonga,mawaziri mnataka Mungu aseme ndo mtoke? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama kulonga JK kalonga,mawaziri mnataka Mungu aseme ndo mtoke?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, May 2, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Madaraka ni dhamana tu wanayo tunukiwa viongozi ilikuwaongoza/kuwaonyesha njia kwa wale wanao waongoza.Bunge ni chombo cha uwakilishi cha wananchi kwa kuwatumia wabunge kuelezeayale yote wananchi wanayoyataka.Rais ni mtumishi wa wananchi ikiwa ni pamoja na wale wote aliowateuwa kumsaidia kazi.Serikali ni watu,na watu ndiyo wenye maamuzi juu ya mustakabali wa nchi yao iendeshwe vipi.Sasa basi mawaziri waliokuwa wanadhani rais ambaye ni mtumishi mtukuka wa nchi hii atawabeba,amepima ameona hambebeki,ndo maana ametoa kauli kali kwa watendaji mnao jifanya kupe kunyonya rasilimali ya taifa.Kwa kitendo hiki mnataka nini zaidi ya kuita press conference na kutangaza yale yaliyokuwa yanategemewa kwa muda na waajiri wenu(wananchi) kwa kujiuzuru na kupisha ofisini ili tuweze kujiridhisha huenda ikawa mmekula zaidi ya kilichoanikwa!Msisubiri nguvu ya umma tuingie barabarani hatutakuwa na salia Mtume.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  utakuwa kilaza
  JK hastahili kulalamika, kuleta tantarira

  Yeye atangaze Waziri flani si waziri tena sasa huyo waziri flani akatalie kutoka hapo ndio kauli yako ingekuwa na mashiko

  JK anadanganya mno ni bingwa wa maneno na watu wenye uelewa mdogo kama wako anawafaidi sana
   
 3. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ukilaza hapo ni kwa mtu aliye na mtazamo finyu,kama kasema ulitegemea nini zaidi ya sisi kuwashinikiza,jaribu kurudia kusoma mada then ndo ulalamike.Suluhisho ni wao kujiuzuru ikishindikana nguvu ya umma itaingia barabarani hata kama ni wewe utakwenda na maji
   
 4. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Panya akiwa anang'ata hupuliza pia. Hakuna kutukuka Bali kupumbazwa.
  Mara ngapi baraza la mawaziri lilivunjwa na makatibu wakuu kuwa wasimamizi wa wizara.
  Kama umemteua waziri akachemsha kwa nini usimfukuze tena hunahaja ya kumwita ikulu Bali unatoa tangazo kwenye redio kama unajiona mnyonge kumwambia uso kwa uso. May be it is time for all who want to be presidents to undergo a rigorous executive management training.
  It's pathetic especially when you see citizens are pleased of no show.
  Mr. President should stop whining in the podiums and become a Country first executive.
  Tumechoshwa na sijui hana watu wakureplace mawaziri sijui nini. Kati ya wabunge wake kuna watu vichwa mle msidanganyike bajameni!Aah.
   
 5. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kalonga nini? Tunantaka awatimue si kulonga huku akiwa kajificha sura.
   
 6. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Watu wengine bana, sasa cha kumpongeza hapo ni nini? Yaani watu aliowateua yeye mwenyewe wanamshinda kuwaondoa mpaka aende kupiga taralila majukwaani?! Halafu watu mmakuja hapa kusema amelnga! How pathetic!
   
 7. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Akufukuzae hakuambi toka,waliodhani atanyamaza na kuwakumbatia amewageuka ndiyo maana kama wao ni waungwana they should step down.Kulonga kwake si vibaya na ni ishara njema,wanacho takiwa wasisubiri mpaka awaambie kama walivyokuwa wanategemea.
   
Loading...