Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,149
2,000
Ukitaka kujua motive zao jaribu kufikiria waliposimamia, mama Samia anatuambia hata madini adimu ambayo mwenda zake aliyaangalia Kwa wivu wa kupindukia tuwaachie waje tu wachimbe, Ndugai anasema Kwa SGR wajichange wabunge walete hayo mabehewa, mchina tunaejua anavyofuonza damu aje tu ajenge Bagamoyo. Hapo mie naamini hawa ni majambazi walio na agenda zao Ila muda utaongea

Ndugai alipewa hela china, JPM alivyostopisha deal la bagamoyo wachina wakadai chao🤣🤣🤣

Leo anashangaa eti kwa nini bagamoyo haijajengwa
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,997
2,000
expand...
MATAGA mmepatwa na kiwewe.

Pambio mfululizo niaka 5 limewalemaza kabisa, mmekuwa vibudu. Jiwe aliwashika vibaya sana.

Mambo ya brainwashing na cultifollowing.

Niseme tu CORONA BABA LAO. Mtu kazikwa na mavi yake😂😂😂😂

Natagas, The honeymoon is over.
 

Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
3,534
2,000
Mzee Mwanakijiji keshaingia makubaliano na upande fulani (compromised, samahani kwa spelling error)!

Ndiyo tatizo lenu nyinyi wenye mlengo tofauti,huwa mnataka kila mtu akubaliane na mitazamo yenu,haiko hivyo Mkuu,watu hubadirika na wala siyo jambo la ajabu,binafsi nilikuwa Pro CHADEMA enzi hizo za kina Zitto,Slaa na hapa JF ukifuatilia huko nyuma utaelewa. But kwa sasa kuwa na mtazamo tofauti na wa Upinzani siyo dhambi. Pengine nikuulize swali,wakati hajawa Compromised alikuwa na makubaliano na huo upande ulipo wewe?
 

Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
3,534
2,000
Ndugai alipewa hela china, JPM alivyostopisha deal la bagamoyo wachina wakadai chao

Leo anashangaa eti kwa nini bagamoyo haijajengwa

Nakubaliana na unachokisema,haiwezekani mtu mzima kama Ndungai kujifanya hamnazo kiasi hicho.Amin nakwambia hawawezi fanikiwa,uzuri JPM aliweka mambo hadharani,hakukataa Bandari isijengwe bali aliwaambia hayo masharti waliyotaka ndiyo hapana. Swali langu kama kweli huo mradi ni “muhimu” sana kama tunavyoaminishwa ni nini basi kiliwafanya Wachina wakimbie moja kwa moja baada tu ya kuambiwa hizo terms hapana,turekebishe na tusonge mbele na ujenzi, nimesoma sehemu,JPM alishaanza hata maongezi na Waturuki waje kujenga hiyo bandari kwa terms zinazoeleweka.
 

Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
3,534
2,000
MATAGA mmepatwa na kiwewe.

Pambio mfululizo niaka 5 limewalemaza kabisa, mmekuwa vibudu. Jiwe aliwashika vibaya sana.

Mambo ya brainwashing na cultifollowing.

Niseme tu CORONA BABA LAO. Mtu kazikwa na mavi yake

Natagas, The honeymoon is over.

Ukisikia kuishiwa hoja na kubaki na vioja ndiko huku sasa
 

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
3,925
2,000
Ndiyo tatizo lenu nyinyi wenye mlengo tofauti,huwa mnataka kila mtu akubaliane na mitazamo yenu,haiko hivyo Mkuu,watu hubadirika na wala siyo jambo la ajabu,binafsi nilikuwa Pro CHADEMA enzi hizo za kina Zitto,Slaa na hapa JF ukifuatilia huko nyuma utaelewa. But kwa sasa kuwa na mtazamo tofauti na wa Upinzani siyo dhambi. Pengine nikuulize swali,wakati hajawa Comromised alikuwa na makubaliano na huo upande ulipo wewe?
... kabla hajawa compromised alikuwa anatoa hoja zilizopimwa kwa mizani, ... nafikiri, kwa utamaduni wa siasa za Bongo, hiyo ilikuwa kabla mzee Mwanakijiji mwenzie wa kwao HAJAUKWAA ULAJI!
 

Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
3,534
2,000
... kabla hajawa compromised alikuwa anatoa hoja zilizopimwa kwa mizani, ... nafikiri, kwa utamaduni wa siasa za Bongo, hiyo ilikuwa kabla mzee Mwanakijiji mwenzie wa kwao HAJAUKWAA ULAJI!

Bado unazunguka tu naomba ujibu swali langu,ni dhambi kuwa na mtazamo tofauti na wa Upinzani? Ukubali tu hapa,watu wote hawawezi kuwa na mtazamo mmoja,wewe baki na huo upande mwache na yeye awe na upande anaouhitaji,sasa rudi kwenye hoja yake na uipinge kwa nguvu ya hoja.
 

Nyangomboli

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
3,342
2,000
Ukitaka kujua motive zao jaribu kufikiria waliposimamia, mama Samia anatuambia hata madini adimu ambayo mwenda zake aliyaangalia Kwa wivu wa kupindukia tuwaachie waje tu wachimbe, Ndugai anasema Kwa SGR wajichange wabunge walete hayo mabehewa, mchina tunaejua anavyofuonza damu aje tu ajenge Bagamoyo. Hapo mie naamini hawa ni majambazi walio na agenda zao Ila muda utaongea
Jana ndiyo nimegundua JPM alikuwa mzalendo wa pekee Nchi hii. Ndugai kasahau hata ushindi wake wa Ubunge ni kwa sababu watu walimuamini Rais. Ndugai kaonyesha wazi kwamba yeye alihongwa na hao wachina wa Bandari kama spika ili awatetee. Ndugai kaniogopesha. Mdugai wa Juzi wanamuaga JPM alikuwa tofauti ma huyu wa jana. Usimwamini mtu.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 

Herbert Nkuluzi

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,584
2,000
Hivi alipodai nchi imepinda hivyo ni lazima aionyoshe, je yeye hakuwa moja katika walioipindisha? Mkapa hakuwa na mawaziri, yeye jiwe akiwa moja wao? Kikwete hakuwa na mawaziri, yeye jiwe akiwa moja wao?

Kwa nini ilipofika tuhuma za ufisadi katika uuzwaji wa nyumba za serikali uliosimamiwa na Waziri wa Mkapa, mwendazake John Pombe Magufuli, mlimtetea jiwe mkidai kwamba alikuwa ni mtekelezaji tu?

Kwa miaka zaidi ya ishirini, jiwe alikuwa waziri katika awamu zote mbili, na hata mara moja hakufikiria kujiuzulu kwa kutokubaliana na bosi wake. Lakini leo lawama zote mnataka watupiwe wasaidizi wake, kweli?

Kumbuka hakutaka ushauri wowote kutoka kwa yeyote, sasa atetewe kwa lipi?

Mbona mwepesi kusahau, Mungu keshatenda miujiza yake!
Umeongea fact sana hapa ,lawama lazima zimguse maana hata akina JK ziliwagusa wakatukaniwa hizo japo wasaidizi wao ndiyo waliokutwa na hatia
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,563
2,000
Msiwagawe watanzania kwa sera zenu za ukabila.

Mimi niko kanda ya ziwa,mbona sijasikia hayo unayojaribu kudanganya mchana kweupe.
Soma vizuri kabla ya kujibu chochote hapo utakuwa umefaulu matumizi sahihi ya akili. Hakuna kitu kinachoitwa ukabila kimelengwa hapo na hakuna sehemu imezungumziwa watu wote (watu mahali) unaelewa maana yake? Wewe sio mimi na mimi sio wewe, mahali ambapo upo mimi sipo na kinyume chake kwahiyo acha kutoa majibu ya kibabaishaji....tafiti kwanza
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,838
2,000
Kwamba kwa ufisadi uliofanyika maana yake timu nzima ya mwendazake inahusika hivyo iwajibike kuanzia yule mwongo wa msikitini hadi UKIZINGUA TUNAZINGUANA.

Hii ni kwasababu wote walikuwa ndio washauri wa karibu wa mwendazake na walijua kila kitu sasa leo hawawezi kumwachia jumba bovu mwendazake pekee. Hapa ni pamoja na yule kiranja mjinga wa mjengoni.
Nimesoma lakini sijaelewa unataka kufikisha ujumbe gani.
 

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,524
2,000
Ni kama kuna juhudi za makusudi za kumchafulia jina ilhali mwenyewe hayupo kujitetea!
Hivi unatumia nini hasa kufikiri?
1) wote waliompinga Magu walishughulikiwa. Tundu Lissu aliyemchambua kama karanga. Risasi 38, na amesurvive kwa muujiza wa Mungu tu. Ben Saanane aliyetilia mashaka PhD ya Magu, na kwa kweli wanataaluma wengi tu walioshuhudia muda aliotumia maabara pale idara ya kemia UDSM, waliosoma nae kabla, wana mashaka na hiyo PhD, Ben Saanane alipotezwa, tena alishapewa warning kabisa.

2) waliokuwa na hoja tofauti na zake, walikiona cha mtemakuni. Wabunge waliopinga mkakati wa Magu kuzipiga hela za Cashewnut Fundzote, baada ya kuzinguana aliponyofoa B. 200 za mfuko huo, wakamtaka azirudishe, yeye akaleta muswada wa kuzipiga zote. Walipolalamika akatishia kuwatimua wote, pamoja na waziri mkuu. Na pia akatishia 'kuanza na shangazi zao'.
3) waliodiriki kuongea kitu tofauti na msimamo wake, walitumbuliwa. Kuna yule msajili wa hazina, somebody Mafuru, aliyejaribu kufafanua ugumu wa kufisidi fedha zilizowekwa Deposit, alitumbuliwa. Dr. Likwelile aliyeshauri mradi wa kuhamia Dodoma usubiri next budget , baada ya Magu kuutangaza mara baada ya kuukwaa uenyekiti wa ccm, bajeti ishapitishwa.

4) alikuwa tayari kufanya kazi na waliosifu na kuabudu tu. Mwanzoni Ndugai alijikuta yuko chini ya Naibu Spika ambaye alipokea maelekezovmoja kwa moja toka ikulu. Ndugai akaamua kuunga mkono juhudi. Akaingizwa kwenye good books za Magu.

Huyo Samia mwenyewe mara kadhaa tulisikia nusura aachie ngazi. Naona alitafuta namna ya kuishi na ugonjwa huo unaoitwa MaguSyndrome. Wengi wa hawa, walioishi na ugonjwa huo, mara baada ya kifo chake, wamerudisha akili zao.
Binafsi siwalaumu. Katika mazingira hatarishi, mtu ana haki ya kujilinda. Katika tawala za kistaarabu, mkitofautiana unajiuzulu. Kwa Magu ni visasi.

Magu hajachafuliwa, amejichafua mwenyewe, hawa wengine walikuwa mateka wa Magu. Na ni wengi sana
 
  • Thanks
Reactions: SMU

BekaNurdin

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
2,264
2,000
JPM mwizi tu! Hayo mema kayafanya kwa pesa ya kutoka mfukoni mwake? Hivi nyie watu mbona wajinga namna hii? Kaifanyia mema nchi wakati huo huo kaiingiza nchi kwenye mizgo ya kipumbavu kama ile ya kununua ndege zinazoendelea kulitia hasara taifa? Isitoshe asilimia kubwa ya miradi Jiwe kaikuta, halafu mnataka kudanganya watu kwamba eti inatokana na "wema wa Jiwe"
Acha kutoa povu.
Kwa hiyo ameondoka na kuiacha nchi kama ilivyokuwa 2015?
Hao wengine unaowasifia waliyafanya kwa pesa kutoka mifukoni mwao?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom