Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

popote uliko JPM nimeamini ulikuwa shujaa wa propaganda nyingi sana
ukageuza umasikini wa watanzania kuwa kichaka cha kujificha na kuficha maovu yako
ukajificha kwenye dini watanzania wakuombee umejitoa sadaka kwa ajili ya maisha ya watanzania
wanyonge kumbe bonge la kibaka hakika ulikuwa shujaa ukawaponda wenzako wametufikisha hapa
kumbe nawe jambazi jpm sina hamu hata kidogo niluikufahamu miaka ya 1983
huko uliko natamani sana ungemaliza muhula wako then tukusute kwa haya madudu yako basi tu
 
Nimezipenda hoja zako si kwasababu ni nzito sana , bali ni kwasababu zina maswali magumu unayoyapatia majibu rahisi sana. Mwl Nyerere aliwahi kusema kwamba watanzania ni watu wa ajabu sana kwasababu wana majibu rahisi kwa maswali magumu sana. Nami nasema usemi huo ni wako muandika thread hii.

Kwa mfano unashangaa watu waliokuwa wakimuunga mkono sana Magu leo wamemgeuka na hata miradi yote iliyokuwa inatajwa ni kama haipo/haikufanywa. Umeenda mbali zaidi na kumtaja Ndugai kwa kushangaa kwanin bandari ya Baga-yo haikujengwa. Na na na............

Swali langu kwako ni moja tu, sijui mwenzetu ulikuwa wapi kati ya 2015-2020? Kwa sababu katika kipindi hicho sauti ilikuwa moja tu na kila aliyejaribu kufungua kinywa cha alikipata cha mtemakuni. Hivyo ulitaka Ndugai wakati ule aseme nini? Na hapo ndio utafahamu umuhimu wa kuwapa watu wako uhuru wa kuzungumza na kutoa mawazo yao amaye pengine ni tafauti nawe.

Hayati Magu, nilimpenda lakini doa kubwa lililoniudhi ni kuwabana wanataaluma kuzungumza wanayoyaju. Kilichompata Prof Assad si kikla mmoja anaujasiri namna hiyo, na wataalam wengine wengi tu waliosahau taaluma zao, kisa eti kuna simba mmoja tu anayojua kila kitu.

Swali langu ninalojiuliza mwenyewe ni moja tu; Hivi Hayati ukali wote ule juu ya wanataaluma (Kuzuia takwimu n.k), alikuwa anaogopa nini? Au alikuwa anaficha nini? Kama kulikuwa alichokificha, pengine ndicho kinachoanikwa hapa hadharani leo. Endelea na uchambuzi wako bila kusahau maswali hayo makuu na utupe jibu. Alamsik!
Jibu
1. Mtei- alimbishia Nyerere na kujiuzulu
2. Balali - alijiuzulu akarudi zake marekani
3. Assad - aliondolewa baada ya kusema ukweli

Ndugai hata Mama Samia kama walikuwa hawakubaliani wangetoa mawazo yao. Wabaki au wafukuzwe au wajiuzulu huo ndiyo uungwana
 
Kaka huijui vizuri system ilivyokaa, na inaonekana ni aidha haujamwelewa CAG au akili yako ndogo kuchanganua mambo. Tafuta mtu mwenye uelewa mzuri akuelekeze hali halisi ilivyo
Ni haki yako kuchangia. Lakini kusema mzee mwana kijiji

Ana akili ndogo ya kuchanganua mambo?
Mlipofika sasa hapana.............

Embu jitafakari asee
 
Hivi unatumia nini hasa kufikiri?
1) wote waliompinga Magu walishughulikiwa. Tundu Lissu aliyemchambua kama karanga. Risasi 38, na amesurvive kwa muujiza wa Mungu tu. Ben Saanane aliyetilia mashaka PhD ya Magu, na kwa kweli wanataaluma wengi tu walioshuhudia muda aliotumia maabara pale idara ya kemia UDSM, waliosoma nae kabla, wana mashaka na hiyo PhD, Ben Saanane alipotezwa, tena alishapewa warning kabisa.

2) waliokuwa na hoja tofauti na zake, walikiona cha mtemakuni. Wabunge waliopinga mkakati wa Magu kuzipiga hela za Cashewnut Fundzote, baada ya kuzinguana aliponyofoa B. 200 za mfuko huo, wakamtaka azirudishe, yeye akaleta muswada wa kuzipiga zote. Walipolalamika akatishia kuwatimua wote, pamoja na waziri mkuu. Na pia akatishia 'kuanza na shangazi zao'.
3) waliodiriki kuongea kitu tofauti na msimamo wake, walitumbuliwa. Kuna yule msajili wa hazina, somebody Mafuru, aliyejaribu kufafanua ugumu wa kufisidi fedha zilizowekwa Deposit, alitumbuliwa. Dr. Likwelile aliyeshauri mradi wa kuhamia Dodoma usubiri next budget , baada ya Magu kuutangaza mara baada ya kuukwaa uenyekiti wa ccm, bajeti ishapitishwa.

4) alikuwa tayari kufanya kazi na waliosifu na kuabudu tu. Mwanzoni Ndugai alijikuta yuko chini ya Naibu Spika ambaye alipokea maelekezovmoja kwa moja toka ikulu. Ndugai akaamua kuunga mkono juhudi. Akaingizwa kwenye good books za Magu.

Huyo Samia mwenyewe mara kadhaa tulisikia nusura aachie ngazi. Naona alitafuta namna ya kuishi na ugonjwa huo unaoitwa MaguSyndrome. Wengi wa hawa, walioishi na ugonjwa huo, mara baada ya kifo chake, wamerudisha akili zao.
Binafsi siwalaumu. Katika mazingira hatarishi, mtu ana haki ya kujilinda. Katika tawala za kistaarabu, mkitofautiana unajiuzulu. Kwa Magu ni visasi.

Magu hajachafuliwa, amejichafua mwenyewe, hawa wengine walikuwa mateka wa Magu. Na ni wengi sana
Umetoa madai meeeengi! Lakini ushahidi sifuri!

Nothing new. Not impressed.
 
Acha kutoa povu.
Kwa hiyo ameondoka na kuiacha nchi kama ilivyokuwa 2015?
Hao wengine unaowasifia waliyafanya kwa pesa kutoka mifukoni mwao?
Nimemsifia nani?! Tunachosema JIWE NI MWIZI, PERIOD! Hana tofauti na hao wengine! Na miradi mingine ambayo anasifiwa na misukule wake, kaikuta! Mradi mpekee "aliouasisi" yeye kama yeye ni ununuzi wa ndege!! Lakini cha ajabu hata hizo ndege alizinunua bila kuwapo comprehensive business plan! Na kuna kila dalili kwenye ndege nako kumejaa wizi ndo maana Wakala wa Ndege akaihamishia Ikulu, and since then haikuwahi kukaguliwa! Sasa kama ni msafi alikuwa anaogopa nini kuweka mambo wazi?!
 
Jibu
1. Mtei- alimbishia Nyerere na kujiuzulu
2. Balali - alijiuzulu akarudi zake marekani
3. Assad - aliondolewa baada ya kusema ukweli

Ndugai hata Mama Samia kama walikuwa hawakubaliani wangetoa mawazo yao. Wabaki au wafukuzwe au wajiuzulu huo ndiyo uungwana
Sasa maamuzi hayo yangemsaidia nini mtanzania? Si wakati wowote utatuzi wa matatizo hutatuliwa kwa maamuzi mamoja? Jifunze kitu katika hili, usipitwe na wakati.

Kwani Magu Miaka 20 aliyokuwa waziri alimbishie mkuu ganu wa nchi?
 
Umetoa madai meeeengi! Lakini ushahidi sifuri!

Nothing new. Not impressed.
Hayo mambo ya korosho yoote yalizungumzwa Bungeni, tena kwa detail nyingi tu akina Hawa Ghasia, Nape Nnauye, na Bwege. Magufuli alitoa vitisho hadharani, kauli zoote nilizonukuu.

Suala la msajili wa hazina lilikuwa public pia, na mara akawekwa kando. Sijamtaja Benno Ndulu, RIP, aliyepinga kauli kadhaa za serikali, mojawapo kuhusu VAT kwenye miamala ya Benki, inalipwa na benki au na mteja. Sijamtaja Prof. Assad. Mtifuano wake na JPM kuhusu 1.5 T. Jinsi Assad alivyoichomeka between the lines, akakwepa kuitoa kama query, pamoja na mengine anayoyataja sasa hivi mwenyewe, ila wenye akili tulishayaona kutokana na chuki ya Magu kwa Assad, akamtumia Ndugai kama Stooge wake.

Sawa, naondoa la Samia, maana halikutangazwa, japo majibu yako wazi hivi sasa.

Point ni kwamba watu wanapenda taifa lao lakini wanakwepa kutofautiana na serikali au na Rais, kwa sababu mbalimbali . Wengine wanajali zaidi matumbovyao, lakini wengine sivyo.

Hakuna ubaya wowote kumkosoa rais, hata kama ni marehemu. Watu bado wanamkosoa Nyerere, Mkapa na wengine. Historia nayo hutoa hukumu zake. Ndio maisha. Ukigombea urais, uwe tayari kwa yote. Unapewa fedha zote za walipa kodi. Lakini unawajibika pia
 
Kwanza kuhamia dodoma ilikuwa kukurupuka kwa jpm. Ndo Mana hela zote zikaelekezw huko huku ajira zikitoweka maazima. Sema ni hivi jpm alikuwa mtu hatari Sana na alikuwa Yuko radhi watu wote wafe ila yeye apatr ujiko tu. Watu wanasuffer mtaani kwa kukosa ajira miaka yote sita. Hata madaktari ambao tulizoea kipindi Cha jk wanaajiliwa bila kubaki lakini nao wanaendesha bodaboda na anajisifu eti ni rais wa wawanyonge. Mungu asingemchukua au akina jk wasingefanya yao nchi nzima ingejaa wamachinga.
Unasema kuhamia Dodoma ilikuwa ni kukurupuka. Hivi unajua plan ya kuhamia Dodoma ilikuwa ni ya mwaka gani?
 
Sasa maamuzi hayo yangemsaidia nini mtanzania? Si wakati wowote utatuzi wa matatizo hutatuliwa kwa maamuzi mamoja? Jifunze kitu katika hili, usipitwe na wakati.

Kwani Magu Miaka 20 aliyokuwa waziri alimbishie mkuu ganu wa nchi?
Alimbishia JK kuhusu kubomoa jengo la TANESCO. Ikabidi aamrishwe kusitisha ubomoaji.
 
Mimi kiongozi (Rais) wa nchi anayewawainda wakosoaji wa Sera na utawala wake kwa ujumla kwa kutumia bunduki/risasi za moto usiku na mchana ili awaue tu kwa sababu anashindwa kujibu na kukabiliana na hoja zao kwangu mimi ni wakala wa shetani 100%, mshenzi na hafai kuwa kiongozi wa nchi yangu...!!

Huyu ndiyo alikuwa Magufuli kabla hajafa...

Kwa hiyo, hata mtu amteteeje mtu huyu, kwangu mimi kamwe siwezi kumwelewa...

Rais huyu angeweza kufanya yote iwe ni wizi, ufisadi, uasherati, uzinzi nk nk na tukamsamehe na tusijali sana...

Lakini dhambi ya kumwaga damu za watu eti tu kwa sababu wanakosoa utawala wako, haikubaliki na ilikuwa ni lazima intervention ya Mungu muumba ifanyike...

Kwa kweli ni HAPANA, HAPANA mpaka mwisho...

Hii ni kasoro kubwa sana kwa Mwendazake isiyolinganishwa na kiasi chochote cha pesa ambacho angeweza kuiba...!!!

Yes, ameacha legacy. Ni ni legacy ya uovu bila kujali alitenda mema mangapi kwa sababu baya moja hufuta mazuri 1000...!!
 
Pro Magu mnaruka ruka mno, kwanza hamna moral authority ya kuwakosoa mnaowaita "wapigaji wapya" Kwasababu kipindi cha Hayati tumepigwa sana ninyi mkiwa busy kusifia na kuimba mapambio. Ninini kinawafanya mjione mna haki ya kuwakosoa hao ikiwa ninyi hamkupenda kukosolewa wakati wa utawala wa hayati?


Pili, Kama ambavyo Hayati hakujiuzulu wakati nchi inaibiwa na kikwete na genge lake akiwa yeye ni mmoja wa hilo genge maana amekuwa waziri kwa takribani mihula mitatu, badala yake alisubiri akapata urais akaanza kuwakosoa vikali, kwa maneno makali watangulizi wake. Formula hiyo hiyo aliyoitumia hayati kuwaponda watangulizi wake ndiyo hiyo hiyo wanaitumia viongozi waliokuwa na hayati kumponda yeye, Tena yeye alienda mbali zaidi kutumia mtutu kumnyamazisha kila mtu ili a"shine" pekeyake.

Tatu, kwa ubovu wa katiba tuliyonayo tunatakiwa kufanya siasa ya kuchagua "mwenye uovu mchache" Wamatumbi wanaita "The lesser evil" ili nchi iwe na ahueni hadi hapo ninyi majizi mtapoamua tupate katiba mpya bora inayosimamia misingi ya utawala bora, haki na uwajibikaji ambayo nayo hamtaki kuisikia. Hivyo kwa sasa Mama Samiah ni mtu sahihi.

Nne, Hakuna sehemu yoyote CAG aliposema miradi ya Hayati ni mibaya, haifai na iondolewe, Acheni kumlisha maneno, nendeni mkasome mapendekezo ya report ya CAG vizuri.

Tano, Tushawajua kuwa hii "panick" yenu ni ya kunyang'anyana tonge na hilo kundi mnaloliita "wapigaji wapya" Mngekuwa na uzalendo huo mngeungana na waTz wanaodai katiba mpya, katiba inayoendana na matakwa na mahitaji ya nyakati hizi Kisiasa, kiuchumi na kijamii. Tatizo lenu mna uzalendo feki wenye version mbili, moja ni ile ya kuimba pambio na kusifu kila kitu pale mnapopewa ulaji, na version nyingine ni ile ya kuwaponda walaji wapya. Mna kale kamsemo kenu ati "watanzania si wajinga wanaona" huu ubadilisheni, semeni timu Magu tunaona, msitusingizie Watz wote kwenye kunyang'anyana keki, wengine wako mbali hata hiyo keki haijawafikia.

Cha mwisho, kama hatuna ushahidi tangible wa kumhukumu nao hayati basi hata kauli zake zinamhukumu, Mfano; Tunajenga kwa pesa zetu, katika serikali yangu ni afadhali mtu apotee kuliko pesa ya umma ipotee. Wakati deni la taifa ndani ya miaka mitano limekua maradufu na pesa zimepotea za kutosha kwa mujibu wa report ya CAG.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Iwavyo vyovyote kama alisimama pale hadi jamaa anatutoka maana yake alishirikiana nae. So na yeye ni mwizi tu. Kama wanadhani kumchafua JPM kutawaacha wao salama basi wanajidanganya. Kichekesho ni kuwa hata wapinzani nao wameungana kutuchezea hii futuhi,wangesimama pembeni na ngojera hizi then wakaenda kwa wananchi kuwaambia tu kuwa kama rais alikuwa hivi basi na mfumo mzima wa ccm ukijumuisha hawa waliobaki wote umeoza tuutoe kuweka wengine wangepata sapoti kubwa sana. Sasa kwa sababu wanaongozwa na chuki binafsi kwa mwendazake hata fursa hii waneshindwa kuitambua wamejiunga

Vyovyote iwavyo kama alisimama na jamaa hadi mwisho anahesabika kuwa alikubaliana na kilichotokea
Ili muwashukie kwa masifa yenu na muanze kuwapa majina ya vibaraka ohh sijui wanatumiwa na mabeberu? Wapinzani toka mwanzo walisema serikali ya awamu ya tano haina uhalali wa kuongoza wananchi, ninyi wafia madaraka mliwajibuje vile...?

Leo hii mnawashauri wapinzani waseme serikali ya Bi samia haina uhalali, mtawasililiza? mwanzo mliwasikiliza? Look, who is a fool here!!!!

Ninyi mnaompinga Samia na serikali yake kwanini msisimame mseme serikali haina uhalali wa kuongoza badala yake mnawasakizia wapinzani hilo jambo, ninyi ni akina nani mnaotaka kujificha katika kivuli cha wapinzani na mnatamani wapinzani wawasemee matakwa yenu.
 
Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.

Watu wanajifanya kushangaa ATCL kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara? By the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia Tanesco, TPDC, TTCL, ATCL, NHC na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa ATCL?

Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.

Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
Acha mihemuko,unafikiri kwa nini Mungu alitusaidia afe mapema???
 
Akiwa CAG BANDARI YA BAGAMOYO HAKUONGEA, PRES YAKE YA JANA HAJARUDIA KUZUGUMUZIA BUNGE NI DHAIFU AU ANASUBIRIA SPIKA ASTAAFU?
Pole, kwasababu huhitaji tafsiri nyingine au ushuhuda kuwa bunge limedhihirisha sasa hivi kuwa lilikuwa dhaifu baada ya Spika wake kutoa matamko kama ya Bandari ya Bagamoyo yakipingana na matamko yake wakati ule. Muhimili wake ndio uliokuwa na uwezo wa kuiuliza serikali kimaandishi ili apate ufafanuzi kwanini mradi mzuri kama ule unapigwa chini.

Badala yake eti anaiuliza serikali sasa hivi kupata maelezo juu ya ubaya wa mradi huo. Huu ni udhaifu mkuibwa sana. Prof hana haja ya kurudia, kama watanzania kama wewe hamkumuelewa wakati ule hata akirudia mara 100 hamtamuelewa.
 
ingia kwenye website ya CAG uone vitu usome ndio uje hapa kuandika hizi chakala chakala
unazijua principle za Auditing wewe?
unajua mpaka ripoti itoke inapitia mchakato gani?
unafikiri Kichere ndio anaenda field kukagua?
kwenye uhasibu kuna
understandability ambayo wewe huijui na hujui kama huijui
kuna verifiability ambayo CAG kaitumia na hao unaowatetea wameshindwa kumpa CAG na team yake.
kuna issues kama, Efficiency, Effectiveness na Economy ambavyo vyote vinazingatiwa na team ya CAG
 
Back
Top Bottom