Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Na. M. M. Mwanakijiji

Ufisadi uliofanyika wakati wa miaka mitano ya Rais Magufuli tunaambiwa ni mkubwa sana. Kwamba, mabilioni ya fedha yameliwa na wajanja na kuwa fedha hizi zimeliwa na watu walioteuliwa na kusimamiwa na Rais Magufuli.

Kwa haraka haraka - kama kawaida naona siku hizi - wakosoaji wa Rais Magufuli (na hapa nawazungumzia wale wa kisiasa) wameruka ruka kwa shangwe wakisema "si tuliwaambia!". Na kinachosikitisha kidogo ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wamejitambulisha kuwa ni wapinzani nao wamerukia kwa furaha tu na hata hawajui ni kitu gani wanaandaliwa. Sijui ni nani anayewalengesha hawa lakini kilichofanyika na kinachoandaliwa labda ni cha kutisha zaidi kuliko kilichotokea.

Kuna mtu aliuliza (jamaa yangu Philemon Michael) wakati msiba ulipotangazwa maswali ambayo sidhani kama kuna mtu atakuja kuyauliza hadharani au kutaka kuyajibu yaeleweke. Na kuna mtu aliuliza tena wakati CAG amewasilisha Bungeni ripoti yake kwamba je hii ndio ile ile ripoti ambayo kama JPM angekuwa hai angekabidhiwa? Sijui jibu lake... Kama ni ile ile inawezekana hakukuwa na jinsi ripoti hii ingekutana na JPM meza moja... Kama ni nyingine... Magufuli alikuwa sahihi mara ya 1.

Hii miaka mitano tumeshuhudia miradi mikubwa ya kila namna na hata tukajisikia kuwa kuna kifu kinafanyika... lakini leo tunaambiwa lote ni changa la macho. Hizo hospitali hakuna zilizojengwa, hakuna masoko, hakuna vituo vya mabasi, hakuna shule zilizofanyiwa matengenezo makubwa, hakuna hiki wala kile na hata ndege tulizoambiwa zilinunuliwa kwa fedha taslimu kumbe hazikununuliwa... yaani, hata hii SGR na Bwawa la Umeme la Nyerere yote ni geresha tu! Kwamba kote huku watu walikuwa wanakula tu na tunachokiona hakipo na kama hili ni kweli basi Magufuli alikuwa sahihi mara 2.

Lakini kingine ni kuwa baadhi ya watu ambao waliteuliwa na Magufuli, walifanya naye kazi, na waliimba "maendeleo" "maendeleo" na hata kusifia kuwa tumeachiwa "urithi" kumbe si kweli; tumeachiwa madeni na ufisadi. Na kwa vile hakuna anayejitokeza kuwa na ujasiri wa kutetea walichokifanya kwa sababu kuna mtu anaitwa "Mwendazake" ameende na utetezi wake kumbe watu wamelia bure. Leo wengine (kina Ndugai) wanageuka wazi wazi; kumbe walikuwa wanaunga mkono uongo; walikuwa wanashangilia ulaghai, na walikuwa wanaficha ufisadi.. hapa watanyoshewa kidole wote kuanzia aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote (na wengi wamerudi au kuhamishwa) na kwa kweli inawezekana wabunge wote walioweza kuingia wakisimama nyuma ya Magufuli. Kama hili ni kweli kwamba ufisadi umetokea wakati watu wale wale ambao leo wanatufunulia ufisadi huo walikuwepo basi Magufuli alikuwa sahihi mara ya 3.

Swali kubwa ni usahihi gani ambao ninauzungumzia? Mwenye kusoma na aelewe. Kama kinachodaiwa na kushangiliwa leo ni kweli basi nchi haina kitu kingine cha kufanya bali kurudi kwenye uchaguzi mkuu mapema zaidi (labda Oktoba mwaka huu) kusafisha uchafu huu; ili wananchi wasisubiri kupigwa tena miaka mitano ijayo... Kama kina Majaliwa na wenzake wote hawakubaliani na assessment hii ya kuwa wamekuwa ni serikali ya kifisadi basi Waziri Mkuu aongoze kujiuzulu mara moja ili kumpa Rais nafasi kweli ya kuunda serikali anayoitaka ambamo ndani yake asirudi HATA MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA SERIKALI YA MAGUFULI. Ndio maana ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA.

Wakitaka kuendelea bila kuwajibika ni lazima kuna kitu kingine kinaandaliwa. Ajenda ya Magufuli haijafa, haitakufa na kwa hakina haitoachwa ife. Maana, kama ufisadi huu umefanyika kwa kiasi hiki basi inawezekana Magufuli alikuwa ni genius aliyepindukia. Yaani, kama ufisadi kama huu ungefanyika wakati wa Mkapa au JK hii nchi ingekuwa mbali sana!
 
Nime note kitu kimoja kutoka kwako nayo ni 'wapinzani' kumbe ulishajiweka tawi la watawala?

Ok ni haki yako lakini kwa binadamu kamili angehoji je, kwanini aliyeninasibu kuwa msafi mithili ya sufi apende kufanya mambo gizani kiasi kile?

Kweli mtu msafi ajiondoe kwenye mikataba ya uwazi?

Kwanini mtu msafi hakuitaji transparency ili umma umsaidie kuwa msafi?

Mnachofanya sasa ni nafsi zinawasuta, mmeachwa kwenye tope msijue nani atawachomoa, mli compromise nafsi zenu kwa vitu vya kipuuzi na kishenzi.

Kinachowauma zaidi mlizoea kuuza maneno sasa hakuna atakaewaamini tena.

Kwa tuliomfahamu Magufuli tangu enzi hatukua tayari kuuza nafsi zetu kwa sifa za kipuuzi na kijumla jumla namna ile.
Pole sana mtafute kazi ya kufanya sasa.
 
SGR, Rufiji Dam ni picha tu zile🤣

CAG kaamua kishabiki kusema bila aibu akiwa na watendaji wale wale, akitaka kujikomba kwa mama kumbe anachotwa akili!

wa kujiuzulu sio PM tu hata Rais!

Hakuna namna watamzima kirais JPM, he is here to stay with us for long long time
 
Nime note kitu kimoja kutoka kwako nayo ni 'wapinzani' kumbe ulishajiweka tawi la watawala?

Ok ni haki yako lakini kwa binadamu kamili angehoji je, kwanini aliyeninasibu kuwa msafi mithili ya sufi apende kufanya mambo gizani kiasi kile?

Kweli mtu msafi ajiondoe kwenye mikataba ya uwazi?

Kwanini mtu msafi hakuitaji transparency ili umma umsaidie kuwa msafi?

Mnachofanya sasa ni nafsi zinawasuta, mmeachwa kwenye tope msijue nani atawachomoa, mli compromise nafsi zenu kwa vitu vya kipuuzi na kishenzi.

Kinachowauma zaidi mlizoea kuuza maneno sasa hakuna atakaewaamini tena.

Kwa tuliomfahamu Magufuli tangu enzi hatukua tayari kuuza nafsi zetu kwa sifa za kipuuzi na kijumla jumla namna ile.
Pole sana mtafute kazi ya kufanya sasa.
Upinzani uko kwenye damu yangu; ila sasa hivi naona kama umepotea maana sijui ni nani amebakia upinzani kweli. Labda tuunde upya kabisa... maana upinzani umekubali jukumu lisilo lao...
 
Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.

Watu wanajifanya kushangaa ATCL kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara? By the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia Tanesco, TPDC, TTCL, ATCL, NHC na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa ATCL?

Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.

Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
 
Ukitaka kujua motive zao jaribu kufikiria waliposimamia, mama Samia anatuambia hata madini adimu ambayo mwenda zake aliyaangalia Kwa wivu wa kupindukia tuwaachie waje tu wachimbe, Ndugai anasema Kwa SGR wajichange wabunge walete hayo mabehewa, mchina tunaejua anavyofuonza damu aje tu ajenge Bagamoyo. Hapo mie naamini hawa ni majambazi walio na agenda zao Ila muda utaongea
 
Mwandishi ni kama vile hutaki kuamini kuwa Magufuli alikuwa fisadi namba moja wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Ripoti rasmi za kiuchunguzi wa pesa (CAG) za sasa zinaonyesha hivyo. Ni upigaji mtupu.

Kwanini ushangae hilo sasa wakati wakosoaji wa Magufuli walikuwa wakiyasema hayo kwa miaka mitano yote?

Ni akina nani waliohoji upotezi wa Trilioni 1.5 zilizotajwa na Professor Assad?
Kwanini Professor Assad alifukuzwa kimizengwe?

Kwanini vyombo vya habari vilizibwa midomo?

Kwanini wapinzani walipotezwa, kununuliwa, kuteswa na kuuwawa?

Kwanini wapinzani walinyimwa fursa ya kufanya siasa, kushika ikulu, kuingia bungeni, kutawala serikali za mitaa au mabaraza ya halmashauri ?

Kwanini genge la Magufuli lilikuwa likiratibu utawala wa Magufuli udumu milele?

Kwanini tender zote za miradi mikubwa ziwe siri ya Magufuli na ikulu tu?

Kwanini genge la Magufuli lilitaka kupindisha mambo kwa gharama yoyote ili kukamata kiti cha urais hata baada ya Magufuli kuwa mahututi/kufariki dunia?

Ukweli unaweza kuchelewa kujionyesha, lakini muda utaufunua ukweli wote. Muda umefika sasa kwa utawala wote wa Magufuli kupimwa upya. Tusiogope kusema ukweli hata kama ukweli huo utatufedhehesha baadhi yetu.
 
Naiona sababu kubwa baadhi ya nchi ambazo raia wanaamua kuandamana na wengine wanaamua kwenda msituni.

Yaaaani serikali na uchafu wooooiiiite huu kwa mjibu wa wao wenyewe lakini bado chama kiko madarakani na serikali yake yooooote iko madarakani?

Na mbaya zaidi kinataka kiendeleee kuwa madarakani.

Hapa kwa mbaaaaaaaali jeshi letu nalo ambalo tuliamini ni safi baadhi vitengo vyetu vinatumika kupitisha ufisadi?

Baaasi ki ukweli wanyonge tulipewa nafasi na sisi ya kupata ka ridhiki maeneo wanayotamani kutufulumusha asee tujiandaeni kuwapisha wenye magari aseeee.

Wapinzani nao badala kuandaa mazingira ya kutupokea, mnaanza na nyie tena kusherekea.
 
Nime note kitu kimoja kutoka kwako nayo ni 'wapinzani' kumbe ulishajiweka tawi la watawala?

Ok ni haki yako lakini kwa binadamu kamili angehoji je, kwanini aliyeninasibu kuwa msafi mithili ya sufi apende kufanya mambo gizani kiasi kile?

Kweli mtu msafi ajiondoe kwenye mikataba ya uwazi?

Kwanini mtu msafi hakuitaji transparency ili umma umsaidie kuwa msafi?

Mnachofanya sasa ni nafsi zinawasuta, mmeachwa kwenye tope msijue nani atawachomoa, mli compromise nafsi zenu kwa vitu vya kipuuzi na kishenzi.

Kinachowauma zaidi mlizoea kuuza maneno sasa hakuna atakaewaamini tena.

Kwa tuliomfahamu Magufuli tangu enzi hatukua tayari kuuza nafsi zetu kwa sifa za kipuuzi na kijumla jumla namna ile.
Pole sana mtafute kazi ya kufanya sasa.

Wewe umeamua kuwa mjinga na sio kuwa watu nafsi zinawasuta

Kwako serikali iliyopita ni JPM!!! sio watendaji sasa hapa usaidiwe nini?

Na hao unaosema wala rushwa si ndio hawa hawa walikuwa madarakani na bado wapo??😜

Shida yako ni uwazi? upi?

umeulizwa hivyo vitu vinajengeka? vipo? vinaonekana? sasa kama mtendaji aliamua kuwa apige kazi na siasa zako weka pembeni...that is a true definition ya mwanaume

Labda na wewe unaungana na wale wajinga wanaodhania JPM alikuwa mpigaji? kwa nguo zile na maisha yale kwake nyumbani mpaka hana paved blocks?

JPM angekuwa mroho wa hela angekuwa tajiri kuliko mengi, bakhresa na manji...kakaa wizara ya ujenzi miaka mingapi?...

sasa huwa tunapenda muwaze pande hizo kuwa HIS MOTIVES were pure genuine and good...

ila ukiwasikiliza watanzania kama wewe nchi haiendi mahali hii....he decided is own way.....alifaulu JPM...wala report ya CAG isikupe faraja yoyote
 
upinzani uko kwenye damu yangu; ila sasa hivi naona kama umepotea maana sijui ni nani amebakia upinzani kweli. Labda tuunde upya kabisa... maana upinzani umekubali jukumu lisilo lao...
Unaandika mithili ya layman. Kwani kuwa mpinzani lazima ujinasibishe na wapinzani unaowaita wamepotea?

Wewe binafsi ume compromise nafsi yako kwakua wengine wamepotea? Really?

Hivi misimamo na ideology za mtu huwa kwa wengine au wewe binafsi?

Kwahiyo huko nyuma ulifanya upinzani kwakua wengine walifanya?

Au kauli na matendo yako yanadhihirisha ulifanya mambo kwa chuki binafsi, chuki za kimaslahi, kikanda, kidini na kirangi? Seriously mtu mwenye upinzani wa Moyoni unaweza sema nilishindwa fanya upinzani maana sikumjua mpinzani wa kweli?

Seriously mtu wa kariba yako ulikuja kuwa simply brainwashed na siasa za watu aina ya akina Magufuli really?
 
Back
Top Bottom