GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Hii nimekutana nayo sana tu hadi kunifanya nianze kuwashangaa ' Waswahili ' na pengine hata kudhani labda wana matatizo Vichwani mwao. Ni kwamba kila ukikutana na ' Mswahili / Mtanzania ' atakuimbia kuwa Mtoto ni baraka yake Mwenyezi Mungu lakini hapo hapo Mwanamke akijifungua tu utawaona Watu wanaenda kumpongeza yule ' Mzaaji ' lakini wote maswali yao yatafanana ambapo wataulizia Mtoto aliyezaliwa ni wa jinsia gani?
Na kuna wengine wakijibiwa ni jinsia fulani ambayo pengine Wao hawakuitaka basi huanza ' Kununa ' na hata kuanza ' mikakati ' ya ' kumgombanisha ' Mama yule ' Mzaaji ' na upande wa Mume wake au hata kwa Mumewe mwenyewe.
Ndiyo maana nawaulizeni wana JF kuwa kama Wote tukakubaliana kuwa Mtoto ni zawadi / baraka kubwa kutoka kwa mwenye dunia yake Mwenyezi Mungu / Allah ni kwanini punde wakizaliwa tu huwa tunakimbia kuulizia ni wa jinsia gani?
Karibuni sana ' mtiririke ' na ikiwezekana ' mserereke ' kabisa!