Kama Kikwete amefanya yaliyo mema kwa miaka 5 iliyopita Gharama zooote za nini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Kikwete amefanya yaliyo mema kwa miaka 5 iliyopita Gharama zooote za nini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by nguvumali, Aug 27, 2010.

 1. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #1
  Aug 27, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kama kweli Rais Kikwete amefanya mengi mazuri , hadi kupigiwa chapuo la kupewa tena uongozi wa juu wa Taifa hili, mi najiuliza gharama zote hizi wanazotumia za nini ?nayatizama mabango njiani hapa Mwanza, na juzi nilikua Mkoani Kagera wameanza kubandika bado sipati picha, jana nikasikia habari kuwa wametumia 1.5Bn kwa gharama ya mabango tu....?bado kuna Tshirt, kofia, chupi na opener za vinywaji.na hakika kila mtu hapa Tz anamjua JK kwa sura, sauti, miondoko na hata mambo yake mengine. Je kuna mantiki yoyote ya kumuuza kwa nguvu Hivyo ama ni ile hadithi Kibaya cha jitembeza.?Bado nafikiri.
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi awamu ya Pili ya mkapa walitumia mabango? kwani kuna mtanzania alie sensitive na siasa asiyemjua Prof. Lipumba au slaa? kwani watu hawawajui? Au ni ushamba unakuhangaisha? Au umeona kwa Kkwete tu? Do not be blind only for some sides. Very unfair
   
 3. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesema kweli kabisa kuwa hao kina Slaa na Lipumba hawajulikani na watu! Hawajawahi kuwa Marais wa kuamuwa kipi kifanywe na kipi kisifanywe.
  Bora ungejibu hilo suwala tu kuliko kuwafananisha Slaa na Lipumba kwa nafasi ya kutenda aliyonayo JK. Hivyo baada ya mazuri yote aliyofanya JK ipo haja ya kugharamika na kupoteza muda kiasi hichi? Hata hizo kazi za Uraisi ameziweka kando. Labda haamini kama kafanya kitu hivyo awaonyeshe wananchi kwa vidole vyake.
  Naona unfairness iko kwa JK kutumia nguvu za Serikali kuzibebesha kwa Chama chake na kupita kukampeni kazi za wananchi wote kwa jumla kuwa ni matendo ya CCM! Basi na ufisadi Serikalini, rushwa na mabaya mengine yatwishwe kwa CCM.
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwa taarifa nilizo nazo JK na chama chake wametumia zaidi ya Tsh 1.5Bn kwa ajili ya kununulia mambango yakuuzia sura zao.sasa kama wamefanya yaliyomema kwa miaka hii 5, gharama yooote ya nini ? bado naamini hawakubaliki, wanatumia gharama kubwa sana kujiuza, maana wao ni takataka.J2, wamelipa Vyombo vya habari 8million, kwa kila gazeti kutoa Tangazo la kuziba eti CHADEMA wasioneshwe kwenye kurasa za mbele. sasa wauza magazeti wakagundua kuwa lile tangazo haliuziki wakalitoa , wakalitoa na kuliingiza katikati
   
 5. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Waliyosema mababu zetu yatajirudia "Chema chajiuza ....Kibaya chajitembeza. Binafsi sioni ubaya wa matangazo lakini to what extremes and using whose costs. Kinachonisikitisha ni kuwa hizo fedha za mabango zingetumika kwa manufaa ya jamii labda kujenga zahanati au kuboresha miundombinu au kununua vitabu basi automatically ingekuwa ni njia ya serikali kujitangaza. Kinyume cha hapo ni sawa na baba ambaye siku zoote hamjali mtoto kuhusu shule, afya na mengineyo halafu anazuka na kutundika picha yake aliyovaa suti (suti ambayo thamani yake pengine angeweza kumnunulia chakula bora na mtoto asipate kwashiakor au kumuandikisha shule) ukutani. Unafikiri huyu mtoto atakuwa na hamu ya kuangalia hiyo picha ya baba ukutani?? haina mantiki na hata asiye na akili atakushangaa unajitangaza kwa nini kwa mtu unayemdhulumu haki zake?
   
Loading...