Kama kijana wa kitanzania kuwa na mawazo yenye tija na maendeleo ya baadae

Gotze Giyani

Senior Member
Feb 28, 2022
121
180
Wadau habarini za muda huu nimeleta hii mada mbele zenu tujadili. Nimekua nikiona maada mbali mbali humu watu wenye uwezo mkubwa kufikiri wakizileta huku na watu wamekuwa wanazipondea mfano mtuu anaweza kuuliza kwa mtaji wa 10m nifanye biashara gani watu wanaishia kumuambia oo sijui anunue mbususu na wengine matusi juu sasa tatizo ni nini haswa wadau au ndio ile watu wengi wanasema hili taifa letu linavijana wa ovyo sana wasio na mawazo yenye tija au maono.

Kama mnabisha ni vijana wangapi ukiwauliza baada ya miaka 5 unataka kuwa wapi na unamiliki nini na nini wataishia kukukosoa tuu japo kukosolewa sio vibaya maana sio lazima tulingane mtazamo ila kuishi bila malengo ni sawa na mtuu mfuu.

Sasa vijana tunafeli wapi wadau nakaribisha mawazo yenye tija kama uwezi kuchangia kaa kimya subiria uzi wa kula kimasiara ukachangie
 
Mkuu vijana Wana mawazo mazuri na wanapambana Sana
SEMA ndio vile milango haifunguki kiurahisi Ila wanahangaika Sana SEMA ukweli
 
Back
Top Bottom