Kama Kenyatta alipata urais, basi hata Lowassa ataupata tu

tatizo ni mfumo... Tatizo ni mfumo...tatizo ni mfumo... Tatizo ni mfumo...... Na viongozi lele mama wa ccm.

Tatizo mi mtu mkuu mbona tunawaona kina Esta Bulaya walikua CCM na walikua wanasumama kidete kuongea fact? Hawa watu ndio wanaotengeneza mfumo mbaya hivyo mfumo haukuwabama ila wameubana wapate wanachotaka. endelea kunielimisha.
 
nyie watu wa ukawa ni wangese sana,mmejazana humu hamjui lolote,siasa za kenya hazina sera,ni za kikabila zaidi.Uhuru Kenyatta alianzisha chama TNA miezi miwili kabla ya uchaguzi na akashinda kwa kuwa tu kabila lake ni kubwa mno kenya-wakikuyu.Hii kitu imeanza tanzania,ikiota sana mizizi wanyamwezi/wasukuma ndio wataongoza hii nchi milele,mtu anaweza kusimama kama mgombea binafsi wakampa

Wanajiita wasomi kumbe ni wasomi uchwara wanaotumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja
 
Siku akipatikana MGOMBEA URAIS ambaye ni msukuma na wasukuma wakamkubali basi Tanzania itatawaliwa na wasukuma milele hadi cku ya kiama na makabila mengine watakuwa wasindikizaji.
 
Tatizo mi mtu mkuu mbona tunawaona kina Esta Bulaya walikua CCM na walikua wanasumama kidete kuongea fact? Hawa watu ndio wanaotengeneza mfumo mbaya hivyo mfumo haukuwabama ila wameubana wapate wanachotaka. endelea kunielimisha.

Alifanikiwa?
 
Acheni ukabila nyinyi fanyeni siasa safi km anavyohimiza edo siasa za ukabila hazina nafasi tz
 
Tatizo ni mfumo na ukae ukijua ni ccm hiyo hiyo imeliweka taifa rehani kwa kuingia mikataba mibovu kabisa.. tena nadhan ni mikataba kama ile ya akina chief mangungo ya kupewa leso na kuachia ardhi... ni ccm hiyo hiyo ambayo wabunge wake wanashirikiana kupinga hoja nzito zenye manufaa kwa taifa kisa tu zimeletwa na upinzani... ni ccm hihiii inayokuwa mstar wa mbele kuzuia mijadal ya kujadili watuhumiwa wa ufisadi na mwisho wa siku wanaumbuka kisa tu upinzan ndio wameleta issue... tatizo ni mfumo wenu mbovu.. mfumo usiowaweka huru mfumo unao walazimisha kushabikia jambo ambalo linaonekana halina maslah na sio haki... ccm mtakufa kifo kibaya...
Tatizo katiba ya Mwaka 1977 Lowasa el wakapinga katiba ya Warioba sasa hivi anajifanya kuikubali baada ya kupigwa chini na Magamba. Swali amekubali serikali tatu
 
Ccm walisha jisahau sana wanakuambia watakaa miaka 800 madarakani
 
nyie watu wa ukawa ni wangese sana,mmejazana humu hamjui lolote,siasa za kenya hazina sera,ni za kikabila zaidi.Uhuru Kenyatta alianzisha chama TNA miezi miwili kabla ya uchaguzi na akashinda kwa kuwa tu kabila lake ni kubwa mno kenya-wakikuyu.Hii kitu imeanza tanzania,ikiota sana mizizi wanyamwezi/wasukuma ndio wataongoza hii nchi milele,mtu anaweza kusimama kama mgombea binafsi wakampa

Kama kilichomsaidia uhuru ni kabila mbona peter kenneth hakushinda?! Make uchaguz ule kabila uhuru walikuwa wanne
 
Mtatoa kila aina ya mifano,, wenye akili wako kimya tu,,, kunatofauti kubwa sana kati ya lowassa na kenyata... Usijifanye huzioni hizo tofauti kwa kutaka tu kusema ukitakacho na ushabiki maandazi...
 
mwaka huu CCM lazima mkione chamoto
mwenyekiti wa ccm arusha na dodoma wamemfata lowasa
 
Mtatoa kila aina ya mifano,, wenye akili wako kimya tu,,, kunatofauti kubwa sana kati ya lowassa na kenyata... Usijifanye huzioni hizo tofauti kwa kutaka tu kusema ukitakacho na ushabiki maandazi...

Wanaamua kujivua nguo wakihisi wako peke yao na wala hawaonwi
 
Kwenye kufanya tathmini za uchaguzi watu awamuangalii kiongozi pekee bali tabia za makundi ya wapiga kura pia kuelekea kwenye uchaguzi. Mali za familia ya Kenyatta sio issue iwapo mkikuyu ana simama na mjaluo kwenye nchi ambayo wapiga kura are voting on principles of tribal identification wakikuyu watamchagua tu Kenyatta (of course like any other african nation kama tayari huyo mwanasiasa ameshajijengea jina kwenye kundi husika).

Kenyatta aliyegombea mara ya kwanza kupitia TANU na kushindwa na 'Kibaki na Odinga' alliance siyo yule yule alieshinda uchaguzi. Kilichowasaidi yeye na Ruto ni umaarufu waliojijengea independently baada ya kuonekana wanajali malsahi ya makundi yao.

Siasa za Kenya zina bargaining to gain majority votes kupitia ukabila, Kibaki kwa kujua anaweza sumbuliwa na Kenyatta kama mrithi wa TANU akakubaliana na Odinga kuongeza nguvu za wajaluo. In return Kenyatta learned his lesson of finding an ally who was also influential in another large tribe na kukimbia kulazimishwa kupelekwa za hague baada ya kujijengea umaarufu kwa makabila yao kujaribu kuongoza nchi and it worked.

Tanzania tuna different voting habits to Kenya at this time kuna kundi makundi madogo madogo mengi ambayo yanazingatia; kuchoshwa na mambo ya kijinga wengi wapo mijini na baadhi wanaamini CCM ni tatizo bila ya kujali kama hao upinzani wanaweza badilisha chochote kwanza ata awajawaambia watafanya nini tofauti na CCM for the most, kuna kundi lingine dogo ambalo limeibuka baada ya katiba mpya na muungano, kuna kundi lingine dogo ambalo pia lina piga kura kwa sababu ya mtu and other petty issues (voter if they like you then can overlook your embezzlement history vinginevyo akina Chenge wasingeshinda kura za maoni and the escrow crew).

Halafu kuna kundi lingine kubwa la CCM ambalo hawa ni 'partisan alignment' wanapiga kura just because CCM is the only thing they know and trust, kuna wengine wanapiga kura CCM kwa sababu yakuona upinzani bado, na baadhi kwakuwa kweli wanajua upinzani ni magumashi.

Kwa hivyo kubadilisha matokeo ya uchaguzi inataka wale walio kwenye makundi madogo madogo ambao ni anti CCM kuweza jikusanya na kujaribu kuleta ushindani; ni impossible kwa sababu kura nyingi za CCM bado zipo vijijini na mijini kwa watu wengi waliosoma na wenye mafanikio.

Kutokana hulka ya watanzania wengi mijini na vijijini na value zetu kama amani, kutopenda kuwekwa njia panda, umoja na mustakabali wa taifa CCM bado ina aminika kwa sababu hizo isitoshe accumalation ya wapiga wa nje bado aizidi ya watu walionao CCM na inaweza badilika anytime who knows Lipumba na Dr.Slaa wakiamua kumwaga sumu wale wanaowaamini wanaweza vipi kuamua kuwaadhibu UKAWA, vipi LOwassa ikijulikana yupo na serikari mbili wangapi wanaweza susia kupiga kura.

Wapiga kura wa upinzani bado ni unstable tofauti na CCM ambao wanajulikana kimsimamo kwa hiyo provided CCM ikifanya attacks zake sahihi upinzani bado sana.
 
Wadau asalaam alaykum!

Ninefanya kazi moja ya kubwa sana ya kufuatilia nyenendo za Rais wa Sasa wa KENYA ndg UHARU KENYATTA kabla ya kua Rais! Nikagundua kwamba kilichokua kinamuumiza sana Kichwa kwenye kampeni zake za Urais zilikua ni tuhuma za MAUAJI kuliko hata zile ni za Ufisadi alizokua akituhumiwa!

Lakini haikutosha wananchi wa KENYA walimchagua kua Rais wa KENYA, Akashtakiwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai(ICC) kwa tuhuma hizo hizo za Mauaji na tena akaletewa lundo la mashahidi!na akawa tayari kuhudhuria kwenye kesi yake kama ilivyopangwa.

Pamoja na tuhuma zote za Mauaji lakini ndugu Kenyatta hakukumbana na pingamizi lolote kubwa liwe ndani au nje ya nchi yake lililomfanya ashindwe kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia waKENYA.

Leo hii tunamtuhumu ndugu EDWARD LOSSA tena bila ushahidi ati hawezi Kuwa kua Rais wa nchi hii! Are we seriuos?
 
Kwa anayeifahamu Kenya atajua kwsmba Kenya ni nchi tofauti sana na Tz. Havifanani si kwa siasa tu, hata kwa tamaduni za maisha yao, maisja ya kijamii na uchumi. Kenya inafanana na Tz kwasababu zote ziko Afrika na mashariki ya Afrika lakini kwa kuzingalia moja moja, zinatofauti kubwa kuanzia malezi hadi makuzi, kuanzia Uhuru hadi leo na hazijawahi kuwa na siasa zinazoshabihana, kwa mwenye kudhani hivyo hajui historia vizuri vinginevyo ni uzembe wa kimakusudi tu kuwaza hivyo.
 
wacha kufananisha UK na Lowassa wengine hatupendi kabisa huyo mvuta bangi! Unatutoa stimu!
 
Back
Top Bottom