Kama kazi ya udaktari na uwalimu ni wito kwa nini ubunge isiwe kazi ya wito??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama kazi ya udaktari na uwalimu ni wito kwa nini ubunge isiwe kazi ya wito???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumishi Wetu, Jul 23, 2012.

 1. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wadau naomba kuuliza ikiwa je kazi ya ualimu na udaktari kama wanavyodai serikalini kuwa ni kazi ya wito, kwa nini kazi ya ubunge isiwwe ya wito pia??? Madaktari wanasomea huo udaktari kwa miaka zadi ya tano mpaka apate uprofesional na mwalimu anasome ualimu hadi afundishe mtoto kuanzia chekechea hadi university!!! Mbunge ana vigezo gani vya kumfanya kazi yake isiwe wito ya daktari ikawa wito???Kwanza wabunge wengine ni STD seven kama tulivyo ona humu na hawajakanusha kwa nini warundikiwe mafedha yote hayo na madokta wafe njaa??? Tena Spika akasema kuwa wabunge wanasaidia watu kwenye majimbo yao huoni kufanya hivyo ni kuchochea rushwa badala ya kukomesha rushwa, kwa namana hiyo rushwa kweli tuata ikomesha???? Kwa nini mbunge asitetee wanachi ili serikali itimize wajibu wake badala ya kuto visenti kwa watu eti anawasaidia si ni kupoza watu ili serikali iendelee kuiba badala ya kutimiza majukumu yake?? Kwa nini ubunge usiwe wito kwa vile wao ni kutete wananchi mafedha yote wanayorundikiwa ni ya nini si kuendeleza rushw aili serikali ipitishe mambo yake bila kipingamizi???
   
 2. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  hoja tamu kwelkwel daktari 975,000/= mbunge 6,000,000/= hahaha wafanye viceversa mbunge 975,000/= na daktari 6,000,000/=
   
 3. malipula

  malipula JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kurudisha heshima ya taaluma ni wataalamu walipwe sana na wabunge walipwe kikawaida hapo ndipo kila mtu atarudi kwenye taaluma yake...tusiwe na watu wengi wapiga porojo wanaolipwa mafao makubwa
   
 4. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mkuu nchi za wenzetu hata Uingereza Mwl hata wa primary analipwa vizuri kama wabunge wao!! Kwa nini mbunge asilipwe posho siku akiudhurua bunge tu tukaacha ufisadi wa kisiasa???

   
 5. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakika kazi zote zinatakiwa kuwa za WITO. Bila WITO kazi inakuwa ya KULAZIMISHWA (forced labour).

  Hata hivyo umesema vyema kuwa habari za ujira ni lazima Serikali na hata Bunge lenyewe libadilike ili wataalam wengine kama Madaktari, Walimu, Waandisi , Wanasheria n.k walipwe ujira na marupurupu zaidi kuliko wanasiasa (Wabunge) na hili halipingiki.
   
 6. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hapo ni kweli Mhe Raisi asidanganye watu eti serikali haina fedha za kulipa madaktari na walimu huku wabunge na wana siasa wakijiongezea posho na mishahara bila kikwazo chochote!! Yatupasa tutambue umuhimu wa wataalamu wetu na walipwe vizuri ni kazi ya serikali kufuta fedha za kulipa professionals mishahara mizuri!!!

   
 7. p

  princedy Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wote mmenena vyema, isipokuwa haya hayabadiliki kirahisi hivyo, mapinduzi haya yanapaswa kupigania. na ndio maana madaktari wanajaribu kuleta mapinduzi haya lakni hawana support, walimu nao vile vile. Tuamke jamani
   
 8. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Naunga mguu hoja!.
   
 9. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tunajaribu kuwaambia hao waheshimiwa walioko mjengoni Dodoma kuwa waangalie na wajue kuwa nao pia kazi yao ni wito hivyo wapiganie maslahi ya walimu na madaktari sio maslahi yao tu na kujaza viroba kama sio matumbo yao tuu!!!!Waibane serikali iongeze maslahi ya wataalamu wetu wagonjwa wasiendelee kuteketea mahospitarini!!!

   
 10. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Nchi ya viongozi mazuzu tu!! Hizo ng'ombe ndo mnaziita "wabunge", wanamwakilisha nani??? Pale bungeni, wanaoweza kuonekana wawakilishi wa wananchi hawazidi 10 out of 300 mps. 95% of mps are "******", and they have nothing to help us rather than looking for their share! Hata kama ni kwa garama ya damu ya Watz, they dont care. Hoja yako ni nzuri sana, ila hawa mazuzu wasingependa kuisoma, trust me. Eti "prof maji marefu", what the hell is this?!
  Naunga mkono hoja kuwa ubunge nayo iwe kazi ya wito ili kuleta uwiano.
   
 11. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja bila marakabisho!
   
 12. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wakielewa kuwa ubunge ni wito wanaweza kuibana serikali ili ibane matumizi yasiyo ya lazima ili iweze kulipa wataalamu vizuri waweze kutoa quality produce!!! Vinginevyo watu wanaendelea kufa na wanafunzi wanazorota mashuleni tunazalisha vilaza sijui nchi itakuwa ya namna gani hii????This is a continuance process the country is deteriorating at a speedy late!!!
   
Loading...