Kama kawaida Unafiki, Kujipendekeza na Kukosa Kujiamini hata kwa Maiti

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
2,651
2,000
watanzania ni WANAFIKI SANA.MPAKA TUNAOGOPESHA. baada ya Ruge kufa kila mtu atamsifia na kujifanya walikuwa karibu n.k

lakini n watu hawa hawa ambao walikuwa wakimsema kuwa ni mnyonyaji n k wasanii wangapi wameathiriwa na Ruge mnawazuia wasiseme wawe wanafiki?

mi nadhani kama kuna mema ameyafanya yasemwe na waliofanyiwa mabaya nao waseme.wasilazimishwe kuwa wanafiki tutakuwa hatuwasaidii walio hai kutengeneza wanapoharibu.

la msingi kusiwe na dhihaka kwa marehemu. ila mabaya yake yasemwe tu. tuacheni unafiki.mabaya kama yapo yasemwe. ruge hawez kwenda mbinguni kwa sisi kumsifia sana.

na hawezi kwenda motoni kwa sisi kumponda sana. ataenda sehemu mojawapo kati ya hizo kwa sababu ya matendo yake tu. aliyoyatenda akiwa hapa duniani.

tuacheni ujinga na unafiki.
 

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
4,524
2,000
Wanaolalamika wamenyonywa nahisi ndio wanafki, kwa sababu hawakuwa mateka,mkila waliloafikiana na jamaa walifanya kwa matakwa yao na hawakuwa watoto...Na hata ukiangalia wanaolalamika dizain dish zao haziko poa
 

Chumchang Changchum

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
4,912
2,000
Itabidi Bunge litoe hoja ya Dharula.. Tutunge sheria mtu akifa hamna kumsema vibaya asije akaadhibiwa kaburini...
Asifiwe mpaka malaika wa adhabu aone nishai kumuadhibu...
Natoa hoja!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom