Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,023
- 18,566
NImeshangaa sana. NImeona upungufu mkubwa kwa upande wa Magufuli, kwamba katika sababu ambazo angependa Ndugai arudi kuwa Spika baada ya uchaguzi, ya maana kuliko zote ni hiyo ya kuunda kamati ya madini.
Kwangu ina maana Magufuli kimsingi anakiri kwamba hakuna cha maana alichofanya Ndugai katika uongozi wake wa Bunge wa miaka mitano. Na sababu kubwa ya kusema hivi ni kwamba Spika kuunda kamati ya madini kama alivyofanya Ndugai ni utaratibu wa kawaida katika kazi za Spika, hakuna cha ziada alichofanya hapo zaidi ya kufanya kazi zake za uspika.
Kwa hiyo alichofanya Magufuli ni sawa na mteja kwenda hotelini, na kuletewa chakula alichoagiza na mhudumu wa hoteli, na mteja kuwaambia watu kwamba huyu mhudumu aendlee kuwa mhudumu hapa hotelini kwa kuwa nilipoagiza chakula aliniletea.
Hivi kweli hapo ndipo Magufuli alipotafuta sifa zote ambazo angeweza kumsifia Ndugai, na kuona hiyo ndiyo ya maana kuliko zote ya kumpigia debe? Kwangu mimi basi kuna tatizo eidha kwa Magufuli au kwa Ndugai.
Labda tuyaache hayo. IKiwa Magufuli anataka Ndugai arudi kuwa Spika, hilo linamuweka wapi Tulia Ackson katika Bunge lijalo ikiwa CCM watakuwa katika nafasi ya wingi wa kumchagua Spika? Pia kuna mambo kadhaa. Labda Magufuli ameona kuwa Tulia hawezi kumshinda Sugu kule Mbeya, au labda Tulia itabidi aridhike kuendelea kuwa Naibu Spika, au pia Tulia anaandaliwa nafasi ya uwaziri. Inawezekana pia kwamba Tulia hayupo katika hesabu za uteuzi wa Magufuli kwa sasa!