Kama Kagasheki anasema kweli: BASI UHUSIANO WA TANZANIA NA QATAR UFUTIKE MARA MOJA.....!

Olaigwanani lang

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
541
175
Majuzi tuu nilimsikia waziri wa maliasili/utalii Balozi Khamis Kagasheki akilalamika kuwa nchi ya Qatar inakataa kutoa ushirikiano katika kuchunguza wanyama waliobiwa hapa Tanzania na inagoma kuruhusu Tanzania kuingia huko ili kuwaona wanyama hao. Sasa kama ndio hivo kuna haja gani kuendelea na mahusiano na nchi hii iliyoshiriki kuiibia nchi yetu maliasili muhimu?
Mimi naona ni bora sasa tu declare diplomatic protest na kumfukuza balozi wao hapa nchini mana nchi yake imetugomea kwa hili.
 
Semeni kweli. Mnatakiwa mlete uthibitisho kamili wa kuthibitisha kuwa wanyama hao ni wenu. Kwani Qatar inachukua wanyama toka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania. Je tanzania mnaweza thibitisha hilo? Hilo limebainishwa wazi na magazeti ya Huku kuhusu sakata hilo.

Kisebu sebu na kiroho papo. Leo wameingia wa Tz wengi sana kuja kuhudhuria mkutano wa mazingira duniani unaofanyika hapa.

Ahlan wa sahalan
 
Udhibitisho utapatikana baada ya tz kuruhusiwa kuingia na kufanya uchunguzi wako Qatar.
Una ndimi zaidi ya moja zinazokufanya u-sound kama joka flani lioga.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
.

Pole sana.

Hata chooni kwa muungwana anabisha hodi.

Qatar ni nchi yenye mamlaka kamili sio public toilet.

Fuata sharia za kimataifa sio kukurupuka.jichunguze mwenyewe kwanza kabla kurukia nchi za wenzako. PELEKA UTHIBITISHO WA KISHARIA KUONYESHA KUNA WANYAMA WAKO PALE NA KUONYESHA WALIFIKAJE.

Kwni waliiba? WALE WAMENUNUA tena kutoka kwa watanzania walio soma na wana akili zao timamu. hivi mtu kaja mchana kweupee, kawinda na kuchukua wanyama hai, kawasafirisha mpaka airport na kuwapandisha kwenye ndege za kijeshi,wakakaguliwa, wakaruhusiwa waondoke halafu leo hii mnaleta maneno ya kitoto!! acheni hizo. kama tuko serious tufuatilie nani mkubwa kabisa aliruhusu biashara hiyo tumfilisi na anyongwe! waacheni QATAR WAPUMUE.
 
.

Pole sana.

Hata chooni kwa muungwana anabisha hodi.

Qatar ni nchi yenye mamlaka kamili sio public toilet.

Fuata sharia za kimataifa sio kukurupuka.jichunguze mwenyewe kwanza kabla kurukia nchi za wenzako. PELEKA UTHIBITISHO WA KISHARIA KUONYESHA KUNA WANYAMA WAKO PALE NA KUONYESHA WALIFIKAJE.

Hakuna kitu kinaitwa SHARIA za kimataifa ni either SHERIA au LAW, SHARIA ni uchafu tupa kule.
 
Huu ni upuuzi mtupu. Tumewauzia Loliondo, tumewaruhusu kuchukua wanyama wanavyo taka kutoka inchini, halafu kuwataka watoe ushirikiano juu ya kuchunguza wanyama walitolewaji inchini. Situnaonekana majuha.
 
Semeni kweli. Mnatakiwa mlete uthibitisho kamili wa kuthibitisha kuwa wanyama hao ni wenu. Kwani Qatar inachukua wanyama toka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania. Je tanzania mnaweza thibitisha hilo? Hilo limebainishwa wazi na magazeti ya Huku kuhusu sakata hilo.

Kisebu sebu na kiroho papo. Leo wameingia wa Tz wengi sana kuja kuhudhuria mkutano wa mazingira duniani unaofanyika hapa.

Ahlan wa sahalan

Utumwa tabu kweli.
Nashukuru Mungu mama zako na baba zako wako Wete, Pemba na hata ufanyaje bado utakuwa m-Qatar mwenye asili ya Uamsho.
Ahlan Wasallan!
 
Tunavyopenda kujikomba hilo la kuprotest sahau mkuu, waprotest teni pacenti (10%) watazitoa wapi? chezea viongozi wa bongo wewe utaoga matope.
 
Utumwa tabu kweli.
Nashukuru Mungu mama zako na baba zako wako Wete, Pemba na hata ufanyaje bado utakuwa m-Qatar mwenye asili ya Uamsho.
Ahlan Wasallan!

Pole sana, kwani maneno yako yanashabihiana na avatar yako kuonyesha kuwa una kuwashakoo.

kwa vyovyote vile kila kitu kinajulikana, hii ni danganya toto kama ilivyokawaida yao kwamba ni upepo tu
 
Barubaru,

..hebu tusaidieni wa-Tanzania tupate HAKI yetu.

..inasemekana kwamba ndege ya jeshi la Qatar ilikuja nchini na kuondoka na wanyama isivyo kihalali.

..uchunguzi unapaswa kuanza kwa kuwajua hao askari wa Qatar walioshiriki ktk wizi huo, ama kwa kujua au kutokujua.

..bila kupata ushirikiano toka Qatar inakuwa vigumu kuwashughulikia mafisadi walioshiriki wizi huo kwa upande wa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:

Mimi naona mnaoneana aibu au ndio ile SERA yenu ya KUVUMILIANA na sio KUHISHIMIANA.

Siku zote uchunguzi unaanzia kwenu kwa kujua je kweli ndege ya Qatar ilikuja na kutua Tanzania. Kumbuka ili ndege kutua lazima ipate kibali cha nchi husika na kuondoka lazima kipatikane kibali cha kuruhusu ndege ile kuondoka na kile ilichopakia. Kwa hiyo ushahidi wenu wa Kwanza kuleta kwa Serikali ya Qatar ni kuleta Vibali vyote vya ndege hiyo kutua, kukaa na kuondoka. Kibali hicho kinaonyesha namba ya ndege na particular muhimu zote.

Pili vibali vya kuchukulia wanyama hao. nani aliidhinisha huko kwenu.

Cha mwisho ambacho kinatakiwa kama ushahidi maalum ni je kuna Medical Doc zozote zinazoweza kuonyesha kuwa mnyama huyu katokea Tanzania na sio kenya wala Ethiopia.

Kwa hiyo utaona kila kitu kinatakiwa kianzie kwenu na huku ni kuja kumalizia tu.

wuhuuuuuuuuuuuuu 2055...watanzania watakuwa wanafunga safari kwenda uarabuni kuangalia wanyama na kusoma vitabu vya historia kwamba kulikuwaga na twiga, tembo nk.....:fish::fish:akili za samaki
 
Qatar si wameshauziwa, ushindwe kulinda wanyama wako na kudhibiti raia wako, ukasumbue raia wa wenzako.
 
Back
Top Bottom