Kama JK ni Rais Mteule, Nchi Haina Rais?

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Wakuu, baada ya jk kuapishwa leo na anaitwa Rais mteule, je, Kikatiba hii imekaaje, hatuna Rais hadi kesho jk atakapoapishwa? Au rais mteule = rais kamili? Tujadili!
 
Kulingana na katiba rais aliyeko madarakani urais hukoma pale rais mpya anapomaliza kula kiapo na kukabidhiwa rungu la madaraka. Immediately kila kitu huhamia kwa rais mpya na yule wa zamani anaemaliza muda wake huondoka kama mtu wa kawaida kabisa, anabaki na mlinzi mmoja tu ambaye atakuwa anatembea nae mpaka siku akifa, motorcade zote zinaishia hapo akiondoka anakuwa na gari yake tu na moja ya ya kumsindikiza ila ikitokea bancha kwa bahati mbaya apande na si kukaa barabani akisubiri apelekewe gari nyingine.
 
NEC mbona hawajatangaza mpaka sasa wanasubiri watu walale usingizi halafu waseme mbona tulitangaza jana usiku! mkiamka asubuhi magazeti yote 'NEC YATANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI 2010 HUKU KIKWETE AKIIBUKA KAMA MSHINDI blah blah!' kwa mtindo sahihi bora magazeti yaseme 'RAIS MTEULE WA TANZANIA KUAPISHWA LEO KESHO JUZI etc.'
 
Wakuu, baada ya jk kuapishwa leo na anaitwa Rais mteule, je, Kikatiba hii imekaaje, hatuna Rais hadi kesho jk atakapoapishwa? Au rais mteule = rais kamili? Tujadili!

Kwanza nikusahihishe. JK hakuapishwa kama rais kwa sababu tume ya uchaguzi haina mamlaka ya kumwapisha rais. Tume ilitangaza tuu mshindi wa kura za urais na kumkabidhi cheti cha ushindi. Pili kwani tume ya zanzibar ilipomtangaza Dr Shein kama mshindi nani aliendelea kuwa rais wa zanzibar mpaka alipoapishwa?
 
Back
Top Bottom