Kama JK anakubalika 61% hofu na ghiliba hizi za nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama JK anakubalika 61% hofu na ghiliba hizi za nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gudboy, Oct 13, 2010.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  [FONT=&quot]Na Gerald Meshack [/FONT]​
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]MJADALA mkubwa kwa Watanzania kwa sasa bila kujali itikadi, dini, kabila ama jinsia, ni Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Ni siku muhimu na yenye maana kubwa kwa mustakabali wa nchi hii, kama waliojiandikisha watapiga kura na kufanya maamuzi sahihi kupata viongozi bora wenye uchungu na kiu ya maendeleo ya nchi yetu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kadiri uchaguzi huo unavyokaribia, ndivyo joto linavyoongezeka kuanzia kwa wagombea wenyewe, kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani kwa kila chama hadi wafuasi wao.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa upande wa wananchi, mbali ya kuwasikia wagombea wa nafasi hizo tatu katika kunadi sera za vyama vyao na nini watafanya kama wataingia madarakani, pia kumekuwa na ghiliba na hila zinazofanywa dhidi ya baadhi ya wagombea hasa wale tishio.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Mfano hai ni mgombea wa nafasi ya urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, ambaye tangu apitishwe na chama chake amezidi kukubalika kila kona ya nchi, hivyo kuzushiwa kashfa mbalimbali.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Walianzia kwenye kashfa ya mke, ingawa weredi wa kuchanganua mambo wamengÂ’amua kuwa, hizo ni ghiliba na hadaa za kisiasa hasa kutokana na kukubalika kwake.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hata kabla ya kupitishwa na chama chake, tayari Dk. Slaa alishajipambanua ni kiongozi wa aina gani na ndiyo maana hata ghiliba na hila zinazoibuliwa dhidi yake sasa, zinaonekana ni mbinu chafu kuelekea Uchaguzi Mkuu.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Mbali ya suala la mke kutumika kama mtaji wa kisiasa katika kampeni hizi, wakaona haitoshi, kwa sababu mbili; mosi tayari suala hilo limefika mahakamani, lakini pili, Watanzania wengi wameonekana kulipuuza, kwani wanachokihitaji Watanzania si huyo mke, bali Dk. Slaa.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Nikiwa mmoja wa Watanzania, niliyebahatika kubaini ghiliba hizi chafu dhidi ya Dk. Slaa, naomba niwasihi Watanzania wenzangu, kuamka kutoka katika usingizi mzito wa miaka mingi na kusema hapana, tunataka mabadiliko badala ya ahadi tamu bila utekelezaji.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Naomba kuchukua nafasi hii kuwapongeza Watanzania wenye mapenzi mema na nchi hii, kiasi cha kubaini kilichojificha nyuma ya hila na propaganda chafu dhidi ya Dk. Slaa, kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Watanzania wanapaswa kukumbuka mtiririko wa visa na uzushi ambao umekuwa ukiibuliwa kila unapokaribia Uchaguzi Mkuu, kwa lengo la kuwahadaa Watanzania kutofanya maamuzi sahihi yenye kuamua mustakabali wa taifa lao.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Nani asiyekumbuka hila chafu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 kuwa, kulikamatwa kontena la majambia ambalo lilihusishwa na Chama cha Wananchi (CUF), ambacho kwa mwaka huo ndicho kilikuwa tishio?[/FONT]
  [FONT=&quot]Tujiulize, majambia yale ambayo yalionyeshwa mbele ya waandishi wa habari kama mfano (sample), yalikwenda wapi ama kutumiwa kwa kazi gani na wahusika walifanywa nini, mbona kimya hadi leo?[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Mwaka 2005 ilikuwa CUF, kwa sababu ndicho kilikuwa chama chenye nguvu zaidi, leo ni Dk. Slaa, kwa vile ndiye tishio zaidi bila kuhitaji utafiti wa Synovate wala REDET ambao wameingia kwenye ghiliba.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya kuona wananchi wengi wamengÂ’amua ghiliba ya suala la mke, kutokana na kutokuwa na tija kwa taifa, wahusika wakaibuka na madai ya mgombea wa CHADEMA, (hawasemi ni nani), kutishia kumwaga damu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kama kweli yupo mtu ndani ya CHADEMA ametoa kauli hiyo, mbona hadi leo hajakamatwa na Jeshi la Polisi kuhojiwa?[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Badala ya kukamatwa na kuhojiwa kwa mhusika (kama yupo), kwa vile hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria, Watanzania wameishia kuona vitisho dhidi ya uzushi huo kwa kumtumia Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Dhamira iliyojificha nyuma ya matamshi ya Shimbo, ni kuwatisha na kuwajaza hofu Watanzania katika kuelekea uchaguzi huo, kama ilivyokuwa kwa Jeshi la Polisi kuelekea uchaguzi wa mwaka 2005.[/FONT]
  [FONT=&quot]Zote hizi ni njama na hila zinazolenga kuwahadaa Watanzania wasifanye maamuzi sahihi kwa utashi wao kuhusu hatima ya nchi yao, ambayo kila kukicha pengo la maskini na matajiri linazidi kuongezeka.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Mbali ya vitisho vya Shimbo, bado kumekuwa na hila nyingi zinazofanywa, kwa mfano zinazodaiwa ni tafiti za kitaalamu kuhusu kukubalika kwa wagombea wa vyama vyote kuelekea Uchaguzi Mkuu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Tangu kutolewa kwa matokeo ya tafiti za REDET na baadaye Synovate, zote zinaonekana ni mwendelezo ule ule wa kuwaaminisha Watanzania kuwa hakuna mgombea anayekubalika zaidi isipokuwa Jakaya Kikwete wa CCM.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Watanzania wajiulize, kama kweli Kikwete anakubalika kwa zaidi ya asilimia hizo 61, kulikuwa na haja gani CCM kuhofia Uchaguzi Mkuu hata kutumia mbinu za ziada kupambana na Dk. Slaa na chama chake?[/FONT]
  [FONT=&quot]Watanzania wenzangu wanapaswa kuamka, kwani CCM imegeuza umaskini wa Watanzania walio wengi kama mtaji wake wa kuzidi kuwahadaa na ndiyo maana wanapingana na sera ya elimu bure, kwa sababu wengi watazidi kufumbuka macho.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hoja ya elimu bure imekuwa ikipingwa na CCM huku baadhi ya viongozi wa chama hicho wakijua fika, wao wenyewe walisomeshwa bure chini ya serikali ya awamu ya kwanza.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kama Mwalimu Julius Nyerere aliweza kutoa elimu bure kwa kuuza nje mazao ya katani, kahawa na pamba, iweje leo isiwezekane kwa Tanzania inayouza Tanzanite, almasi, dhahabu na mazao mbalimbali?[/FONT]
  [FONT=&quot]Iweje CCM iseme elimu bure haiwezekani, ilhali serikali inatumia mamilioni ya walipa kodi kila mwaka kununua mashangingi, ambapo kila moja si chini ya sh mil. 200 hadi 400?[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hivi ni kweli kuwa elimu bure kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu haiwezekani chini ya kiongozi makini mwenye uchungu wa kweli na nchi na watu wake ambao kwao kila kukicha heri ya jana?[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Ukiwasilikiza kwa makini hao wanaojenga hoja kuwa elimu bure haiwezekani, baadhi yao ni wale waliosoma bure katika Awamu ya Kwanza akiwemo Kikwete mwenyewe.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hivi shangingi moja bado halitoshi kununua madawati kwa shule moja ya msingi, kuwaondolea adha watoto wetu wanaopinda migongo wakiandikia magotini huku watoto wa wenye nazo wakisoma shule za kifahari za ndani na nje ya nchi?[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Nikirejea kwenye hoja, vipi fedha za kununua mashangingi kila mwaka ziwepo, isipokuwa za kutoa elimu bure ili kujenga taifa lenye wasomi wengi zaidi katika kupambana na adui ujinga?[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kama haiwezekani, kumbe kwa kipindi chote cha miaka 49 tangu uhuru wa nchi hii, kuna haja gani CCM kuendelea kuwepo madarakani? Angalia leo hii mgombea wa CCM alivyo na ahadi nyingi kuliko hata wagombea wengine, yote hii ni uthibitisho kuwa kuna dosari katika utawala wa CCM.[/FONT]
  [FONT=&quot]Iweje mbadala wa meli ya mv Bukoba iliyozama Ziwa Victoria Mei 21, mwaka 1996 iwe ahadi ya Kikwete mwaka huu kama atachaguliwa?[/FONT]
  [FONT=&quot]Hivi hata hili Watanzania hawalioni kama ni kuchezewa akili?[/FONT]
  [FONT=&quot]La kujenga reli ya treni ya kasi, hospitali saba za rufaa na nyingine lukuki, haya yanaingia akilini kweli wakati hata akishinda, miaka yake si zaidi ya mitano?[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kimantiki, kama CCM ingekuwa imefanya makubwa ya kujivunia mbele ya macho ya Watanzania, leo hii isingetumia nguvu ya ziada na gharama kubwa kujinadi kwa wananchi, kwani ingenadiwa na ufanisi wake.[/FONT]
  [FONT=&quot]Angalia namna ya mbinu chafu zinavyozidi kuibuliwa kila kukicha kuelekea Uchaguzi Mkuu ikiwamo ujumbe wa sms wa kumchafua Dk. Slaa, yote hii ya nini kwa chama kilichodumu madarakani kwa miaka 49?[/FONT]
  [FONT=&quot]Namaliza Mtazamo wangu kwa kuwasihi Watanzania wenzangu kutokatishwa tamaa na hila hizi chafu dhidi ya Dk. Slaa, kwani kuandamwa kwake ni uthibitisho tosha kuwa ndiye tishio kubwa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Watanzania wajiulize, wagombea wa kiti cha rais wapo wangapi? Je, ni kwanini Dk. Slaa ndiye anaandamwa kwa hili na lile?[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Yote hii ni uthibitisho wa wazi kuwa ndiye kitisho zaidi. Nami nasema, majaribu haya yazidi kuwathibitishia Watanzania kuwa Dk. Slaa ndiye tishio zaidi kati ya wagombea wote, kwani dhahabu safi lazima ipite kwenye moto.[/FONT]


  source: Tanzania Daima
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima Slaa ni mbele kwa mbele na tishio zaidi.
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Yaap, msumari huo
   
 4. S

  So Perfect Member

  #4
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania daima=chadema=dr silaha
   
 5. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  hayo sio kweli hili ndilo gazeti la ukweli bana
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sijui umepenyaje ile ban ya mods, naona mnajisajili kwa kasi ya ajabu kama CCM wanavyofuja pesa wakati wananchi hawana hata panadol za watoto hospitalini
   
 7. m

  mozze Senior Member

  #7
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli anakubalika, na kama kweli kikwete ni mtu mashuhuri Tanzania, inakuwaje sasa wanaomba msaada wa wazee wastaafu? Kinana alisema maji yakiwa shingoni wataomba msaada.....so bado Kikwete anafika 61% kukubalika?
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
 9. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Article hii nimeisoma hadi nikasisimka maana imejaa ukweli mtupu. Nakumbuka kikwete alipoingia madarakani kuna ma-benz mapya yalinunuliwa. Je yaligharimu kiasi gani na pesa walitoa wapi? Kama kuna mtu ana data atukumbushe kidogo ili tuweze kulinganisha na kauli anazozitoa kwenye majukwaa.
   
 10. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Matokeo ya pweza wa kombe la Dunia sasa yanaitwa ni utafiti!
   
 11. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  utangulizi: Hata angegombea Dkt Kikwete na Kuga Mziray, you guessed my vote, PKM!
  Sisi em have got bad behaviours I don't like. Here are two of them: 1. Ad Hominem, that is, attacking a person than argument/sera one stands for 2. Straw man arguments: they misrepresent the opponent's position and thereby erecting straw man. They then demolish that straw man.

  Another reason they will NOT get my vote, whether by hooks or crooks
   
Loading...