Kama jk amefanya haya tangu aingie madarakani, ccm hakutatoka rais makini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama jk amefanya haya tangu aingie madarakani, ccm hakutatoka rais makini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paul Kijoka, Jul 7, 2012.

 1. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni mambo mengi ya kustaajabisha aliyoyafanya JK kwa kushirikiana na CCM yake ila haya mambo yanashangaza
  sana, kwamba:
  1. pesa za EPA kupitia KAGONDA alizikwapua kwa ajiri ya kuwagawia waislam ili wamuunge mkono kwakuwa walishakitupa ccm na kujiunga na CUF,
  2. aliwaahidi waislam Mahakama ya Kadhi, Organization of the Islamic Conference (OIC) kisha akawatosa kwa kukumbana na mashinikizo
  3. aliwaahidi pia kuwapa wizara nyeti ikiwemo ya fedha, mambo ya ndani, ulinzi na usalama na ma makatibu wakuu pia.
  4. RICHMOND anaijua vizuri kuliko Lowasa na Lowassa ni kafara (lkn haimaanishi kuwa Lowassa ni msafi)
  5. anajua mipango yote ya upotevu wa Dr. Balali

  Habari hizi zinajulikana kila kona kwakuwa sasa hivi JK ameanza kuandamwa kwa kukiuka kubaliano la wizara ya fedha.
   
 2. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  We umetumwa! Hebu lete ushahidi wa huo utumbo ulioumwaga hapa! JK aliahidi mahakama ya kadhi ambayo ameshindwa kuitekeleza kutokana na wakristo kupitia maaskofu kusema damu itamwagika,kwa maana watawaua Waislam ili kuwatokomezea mbali na Tz ibakie kuwa pure christianity country. Kuhusu Kagoda kamuulize Mkapa. Lete ushahidi wa vielelezo kuwa JK aliwahonga Waislam ili ashinde! Hivi wale wa kanisani waliosema JK chaguo la Mungu hukuwasikia? Walipiga kampeni makanisani ili CUF isishinde 2005 kwa kuwaambia JK chaguo la Mungu! Kampeni zenu tunazijua!
   
 3. t

  tocolyitics Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usibishe kishabiki, yote hayo mbona ulimwengu unajua na watanzania wanajua..
   
 4. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ila habari ndo hiyo. Ukweli unauma. Nimefurahi kuona umekiri manaeno yangu unayoyapinga, kumbe unakubali kuwa wakristo waliingia mkenge kwa kumuita jk chaguo la Mungu! Na mwaka 2010 mnajitapa kuwa mliwashinda wakristo! Nadhani hatuendi namna hii. Tunahitaji mtu wa kulikomboa taifa letu kutoka mikononi mwa wakoloni weusi ambao ni hatari kuliko ata wale weupe.

  Tunahitaji mtu atakeyerudisha hela yetu ambayoimekwibwa na wahuni na kukimbizia nchi za nje na wale waliokula kagoda watatapika pia
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  wakati wewe unahangaika na chuki zako,mwenzako yuko bize na shughuli za wananchi za maendeleo.utajiju.

  Jul 7 Jul 7
  [h=1]IKULU:Rais Jakaya Kikwete Akisalimiana na Mtoto Mlemavu wa Ngozi Salma Salum[/h]
  Written by haki | // 0 comments
  [​IMG]
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto mlemavu wa ngozi Salma Salum wakati Rasi alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar Es Salaam Jana.Picha na Freddy Maro-IKULU
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Jul 7
  IKULU:Rais Jaka ayKikwete Ampongeza Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kKwa kKuteuliwa kKuwa Rais wa TEC  [​IMG]
  Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa
  --

  [​IMG]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kwa kuteuliwa kwake kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) akichukua nafasi ya Baba Askofu Yuda Tadei Rwaich aliyemaliza muda wake.

  “Nimefarijika sana na uteuzi wako kushika wadhifa huo muhimu hasa kutokana na imani kubwa waliyonayo Maaskofu kuhusiana na uwezo wako katika kukiongoza chombo hicho muhimu”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake.


  “Ninatambua na kuthamini mchango mkubwa ambao, kwa muda mrefu sasa, Kanisa Katoliki limekuwa likiutoa kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake hasa katika nyanja za huduma za jamii.

  Aidha uhusiano mzuri uliopo kati ya Serikali ninayoiongoza na Kanisa Katoliki unaendelea kunitia moyo, hivyo ninakuhakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza na kuimarisha uhusiano huu kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla”, amesema na kusisitiza Rais Kikwete katika salamu zake za pongezi.

  Rais Kikwete amemtakia Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kila la heri na mafanikio makubwa katika kuliongoza Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.
  6 Julai, 2012
   
 8. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  JK chaguo la 'mola'
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  [h=1]Rais Jakaya Kikwete Atembelea Maonyesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam[/h]
  Written by haki | // 0 comments
  [​IMG]
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya bidhaa zitokanazo na Wannyamapori wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mali asili na utalii katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana
  [​IMG]
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya bidhaa zitokanazo na Wannyamapori wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mali asili na utalii katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana
  [​IMG]
  Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa PPF Bwana William Eriyo akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mradi wa uwekezeaji wa hoteli ya kisasa iliyojengwa na shirika la PPF mjini Mwanza wakati Rais alipotembelea banda la PPF katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana.Picha na Freddy Maro-IKULU
   
Loading...