Kama Jamii ya Wafuganyi Wamasai Ngorongoro ni Sehemu ya Utalii Kwanini Wanakufa Kwa Njaa

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Hii ni habari ya ukweli kwenye mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha, hapo nyuma jamii ya wafugaji hawa walikua wanalima maboga pamoja na viazi kwenye ukanda huu wa Ngorongoro maeneo kama ya Engaruka na ukanda wa Lake Natron walikua wanajikimu na kilimo kidogo kidogo kama nilivyotaja hapo juu, lakini chakushangaza kwa mamlaka ya hifadhi hii imewapiga marufu jamii hii ya Wamasai kutojihusisha na ukulima huu na chakushangaza ni kua Wamasai wanakufa kwa njaa ambayo ni aibu kwa mamlaka hii.

Swali la kujiuliza kwa mamlaka hii kama hawataki jamii hii wasijihusishe na kilimo hivi je hela zinazolipwa na mawakala wa utalii nchini zinakwenda wapi? na je kwanini Wamasai hawa wasifaidike na hela hizi kama Hawatakiwi kujikimu na ukulima huu mdogo mdogo kwakuwanunulia chakula na mahitaji mengine? Niko njiani naelekea Lake Natroni nitawajuza nini kinaendelea na ninawasilisha.
 
Back
Top Bottom