Kama Italy ndo wanakosa kwenda Russia 2018 basi round hii world cup Haina maana

Wanaitwa Azzuri aka Pizza boys watakosekana Moscow kwa Putin kombe la dunia 2018 ni pigo kwa wapenda soka duniani.

Italia wana vionjo vyao vya mpira wakisifika kwa mpira wao wa shoka anzia zama za kina Gattuso ila kwa sasa ushoka wao umepungua kidogo zaidi wanategemea ukuta wao wa chuma ila nao umekua ukuta mlaini tu.

Mabingwa mara nne mara ya Mwisho Materazzi na Zidane wakiingia kwenye kumbukumbu mbaya za kupigana Vichwa na kutoleana maneno mabaya.Tuliona wakongwe wakilia mechi yao ya mwisho na hatimaye Buffon kutangaza kustaafu kucheza timu ya Taifa Azzuri.

Lawama nyingi wanamtupia kocha wao kwa mbinu zake mbovu na kuwaweka mastaa nje kama vile Jorginho hasa game ya mwisho na Sweden.

Tutakukumbuka Pirlo umestaafu na Soka lako pale Italia.
 
Italy kitu gani?mbona mataifa ya kufanya mechi ziwe tamu yako mengi tu? acha kukariri ujinga
 
Italy kitu gani?mbona mataifa ya kufanya mechi ziwe tamu yako mengi tu? acha kukariri ujinga
Utazungumziaje kombe la dunia bila kutaja mataifa kama Brazil,Germany,Italia, usiangalie mchezaji mmoja mmoja angalia timu nzima pamoja na mafanikio yake.

Italia wanahistoria kubwa na kombe la dunia sasa we sijui unataka kuniambia timu gani hizo,Unaelewa kwann Buffon Alilia?
Italia na kombe la dunia ni sawa na Zimbabwe bila Mugabe.
 
Italy mafala sana. Unampa timu ya taifa kocha ventura ambaye maisha yake yote kwenye vilabu anavyofundisha hajawai kutwaa kikombe chochote kile.Uwezi ukaenda Urusi unamwacha insigne nje unampanga gabiadini, vile vile unampanga darmian unamwacha Spinazola. Huwezi kumwacha Zaza au Mkongwe Quagliarela wakati yupo kwenye form. Italy wenyewe wamejitakia kutokwenda Russia.
 
Back
Top Bottom