Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 653
- 1,058
Tayari mpango mzuri na wenye maana kubwa sana katika Taifa letu unaendelea kuandaliwa. Uchaguzi wa Mwaka 2020 utakapokamilika tu na iwapo CCM watakuwa wameshinda kuna kesi itafunguliwa kwa umakini wa hali ya juu kuhusu kwa nini matokeo ya Urais hayapingwi Mahakamani.
Kinachozuiwa nchini mwetu ni kwa kutofungua kesi ya kupinga matokeo ya Urais lakini kuhusu kufungua kesi ya kuhoji kuwa ni "Kwa nini Matokeo ya Urais hayapingwi Mahakamani" hakujazuiwa kufunguliwa kesi.
Tundu Lissu tayari amekuwa katika maandalizi ya kufungua kesi ya hivyo mara tu Uchaguzi utakapokamilika. Iwapo Mahakama Kuu ya Tanzania itakataa kesi ya hivyo kusajiliwa kwao tayari maandalizi ya kuisajili Mahakama ya Afrika Mashariki au ya Afrika nayo yanaendelea. Ushahidi wa mambo yanayotendeka ili kujenga hoja katika kesi hiyo unaendelea kukusanywa.
Inavyoonesha kesi hiyo haitafunguliwa tu iwapo itatokea Upinzani wameshinda kwani watachofanya ni kubadilisha Sheria ya Uchaguzi na kuruhusu matokeo ya URais kupingwa Mahakama Kuu.
Kwa hili CCM tupo tayari kwa kiasi gani kulipokea.