CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Kwa mliofuatilia uandaaji na hatimaye kuoneshwa kwa makala maarufu ya Living With Michael Jackson mtakubaliana nami namna mwandishi mashuhuri Martin Bashiri alivyomrubuni, Mfalme wa Pop Duniani, Hayati Michael Jackson, kushiriki kwenye uandaaji wa makala kwa kumhakikishia kuwa makala hiyo ingelimtangaza vema na kubadili mtazamo wa dunia kuhusiana na kashfa alizokuwa akishutumiwa mwanamziki huyo. Hata hivyo badala ya kumsafisha Michael Jackson makala ya Living with Michael Jackson ilizidi kumchafua na kuibua tuhuma nyingi zaidi.
Kwa ufupi Martin Bashiri alikuwa na nia ovu dhidi ya Michael Jackson.
Nimefikiria sana ushiriki wa Rais Samia kwenye makala hii na kuwa na maswali mengi kichwani ikiwa ni kweli waandaaji wake wana nia njema na ya dhati kabisa ya kuitangaza vema nchi yetu na hatimaye kuvutia watalii na uwekezaji nchini. Kabla ya kushiriki ilitakiwa tufanye tathmini ya kina ikiwa ni pamoja na kuweka wazi wafadhili wa mradi huu na lengo lao hasa.
Nimeishi na raia wa nchi za magharibi kwa muda mrefu, pia nimetazama movie na makala nyingi sana zinazoihusisha Africa kwa movie nzima ama sehemu ndogo sijawahi kuona wamerekodi sehemu za kuvutia. Kwao ni umasikini na vita pekee ndiyo kipaombele. Katika vyote ni movie ya Black Panther pekee iliyoionesha Africa kuwa ni sehemu iliyoendelea zaidi japokuwa kwa kutumia fiction.
Ikiwa ni kweli wana nia njema na nchi yetu basi Rais Samia atakuwa amefanya jambo jema sana mbali na hapo tusubiri kuoneshwa umasikini, maradhi na ujinga wa nchi yetu ukitangazwa duniani kote.
Mara ingine nitakuja na ushauri mzuri wa namna bora ya kutangaza utalii na uwekezaji wa nchi yetu bila wala kutumia nguvu nyingi.
Nawatakia siku njema.