Kama ilani ya uchaguzi ni ushahidi wa ahadi kwa mpiga kura: Je, vyama vya UKAWA vinatoa ahadi hewa?

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,589
4,599
Jukwaa hili ni moja ya sehemu ya kuelimishana na kufunguana ufahamu wa mambo yahusiyo siasa hasa za nchi yetu ya Tanzania. Moja ya nyakati muhimu za kisiasa ni wakati wa uchaguzi ambapo wagombea wa vyama vyote wananadi ahadi zao kwa wananchi na wananchi kuchagua mgombea wa chama chenye ahadi nzuri.

CCM imekuwa na desturi wa kutayarisha ilani ya uchaguzi kila baada ya miaka 5 ambapo mgombea wa udiwani, ubunge na urais kupitia CCM hana budi kuinadi na inabaki kumbukumbu kwa mpigakura , kwa CCM na serikali katika kufuatilia utekelezaji wa ilani yake.

Hali hii imekuwa tofauti kwa upande wa pili ambao unaitwa vyama vinavyounda UKAWA wamekuwa na kawaida ya kutoa ahadi za mdomoni bila kuwepo kwa ilani ya kufuatilia utekelezaji wake na hili linanitafakirisha sana na kujiuliza sana. Mfano: Je, wapinzani wakishinda urais wangekuwa wanatekeleza nini? Je, wananchi watabaki na kumbukumbu ipi kama ushahidi wa ahadi? Je, ahadi wanazotoa si hewa na hazitekelezeki hivyo wanaogopa kuandika ilani ambayo itabaki kama ushahidi?

Kwa hali hii inaonesha wazi, watanzania wamekuwa wakidanganywa na kupumbazwa na vyama vya UKAWA wakati wa uchaguzi kwa kutajiwa ahadi za kichwani ambazo utekelezaji wake ni wa kidhahania na mara zote wamekuwa wakipoteza haki zao za msingi kwa kupigia kura wagombea wa vyama hivyo vyenye ahadi za kufikirika. Matokeo ya ahadi hizo za kufikirika leo hii tunayaona Hai, Kawe, Iringa, Mbeya, Tanga, Mwanza na maeneo mengine ambayo wabunge waliochaguliwa huko wanafanya mambo tofauti na waliyoahaidi kwa sababu walivyoahidi ni vya kufikirika tu.

Tai ambayo inakuletea bugudha shingoni ni hatari kwako, fanya uamuzi sahihi sasa tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuchagua viongozi wa vyama wenye ILANI na sera zinazotekelezeka, usikubali kufa na tai shingoni. Ione thamani ya kura yako leo kwa kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi. Tafakari kwa makini maneno ya Mwalimu Nyerere aliposema kiongozi bora atapatikana CCM. CCM inatoa viongozi bora kwa sababu: wanaandaliwa kimaadili wangali wadogo kuwa viongozi, wanakuzwa katika miiko ya kiuongozi, CCM inachagua na kupendekeza wasomi katika nafasi mbalimbali ya kiuongozi na kupamba mbegu ya kizalendo kwa wanachama na viongozi wa chama.
 
Back
Top Bottom