Kama huna jambo jema la kuzungumza, basi kaa kimya…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama huna jambo jema la kuzungumza, basi kaa kimya…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 7, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp] [​IMG]
  [/FONT]
  [FONT=&amp][​IMG]
  [/FONT]
  Ukimya si mzuri hususan pale wanandoa au wapenzi wanapotofautiana. Wapo baadhi ya wanawake pale inapotokea wametofautiana na wenzi wao hutarajia kuwaona wakipandwa na hasira na kuonyesha hisia zao.. Kitendo cha mwanaume kuongea kwa hasira na kuonyesha kuchukizwa na jambo fulani, mwanamke huamini kwamba, ni hasira za muda tu na baada ya hapo yatakwisah na maisha yataendelea.

  Lakini pale inapotokea kuna jambo ambalo linaonekana limemkera mwanaume lakini akakaa kimya bila kusema neno, au inawezekana mwanamke kafanya kosa ambalo anaamini mume akijua kutazuka balaa, na ikatokea akajua, lakini akabaki kimya, jambo hilo linaweza kumnyima raha mwanamke kwa kiasi kikubwa.

  Inawezekana pia mwanaume akawa amekosea au kuna jambo amefanya ambalo halijampendeza mwenzi wake, lakini pale mke anapokuja juu, mwanaume akabaki kimya bila kuomba radhi wala kusema neno, jambo hilo pia linaweza kuwa tatizo. Hakuna mwanandoa anayependa ukimya wa aina hii… kwani kitakachokwenda kichwani mwa mtendewa ni kwamba atahisi amedharauliwa kwa kiasi kikubwa.

  Lakini wakati mwingine kukaa kimya ni jambo jema. Kuna wakati inaweza kuonekana mwanandoa anayekaa kimya pale anapoudhiwa na mwenzi wake ni utoto na ni njia dhaifu ya kutatua migogoro katika mahusiano, lakini kukaa kimya wakati mwingine kunaweza kusaidia kuzuia mzozo kuwa mkubwa kwani kutofautiana nakutupiana maneno kwa wanandoa kunachukuliwa kama vita ya kuviziana ambayo mwishowe inaweza kusababisha kuzuka ugomvi na wanandoa kushikana.

  Kumbuka kwamba inapotokea kutupiana maneno kwa wanandoa, kuna uwezekano mkubwa wa kila mmoja kutumia fursa hiyo kueleza udhaifu wa mwenzie kwa sababu ya kutawaliwa na hasira kupita kiasi. Jambo hilo linaweza kuzusha ugomvi mkubwa sana kwa wanandoa. Kama unataka kuepusha shari, basi ni vyema ukafunga mdomo wako na kukaa kimya japo kwa muda mfupi itasaidia sana kuleta amani kwa wapendanao.
   
 2. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  pata beer mbii na nyama choma nakuja!
  ukimya lakini saa nyingine unazidisah ugomvi unajua!mi kwa kweli ili nisikie raha ya hasira nata mtu ninayemconfront anijibu sio anitazame kama sanamu tu!hapo natamani kupasuka!au mtu unamuuliza kitu ye huyo anafngua mlango anatoka nje !kha!cha kuniacha na mihasira yangu nini?yani ukirudi unalikuta bado bichi!BORA TUONGEE YAISHE TUSONGE MBELE!
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  snowhite
  nimeelezea uzuri na ubaya wa kukaa kimya na ndio maana nikasema, "kama huna jambo jema la kuzungumza, basi kaa kimya." Nilikuwa namaanisha kwamba si lazima wapenzi kutunishaiana msuli wa kubishana, kwani kuna uwezekano wa kukuza ugomvi na kuwa mkubwa kutokana na wapenzi kutumia maneno makali pale wanapobishana, ni vyema mmoja kukaa kimya kama anaona ugomvi unapoelekea sipo itasaidia kuleta amani......

  [​IMG]
   
 4. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  sa Mtambuzi mi nitakaaje kimya wakati nina hasira na nimeudhika jamani si lazima niongee ili hasira ziishe?well tunatofautiana kwenye kutatua misunderstandings lakini mimi kwa kweli napenda kumaliza ugomvi mapema sana ili niwe na amani manke hasira huwa zinanitafuna ile mbya!na ili saga liishe mapema we nijibu tu maswali yangu jitetee kidogo omba msamaha yanaisah fasta,na ikiwa ni mimi nimekosea napenda zaidi nihojiwe tena na nikuone umekasirika na unimind kweli kweli nijisikie vibaya kwa nilichokifanya,then nijitetee,unisamehe na liishe hapo hapo maisha yanasonga mbele!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  snowhite suppose unaongea na mwenzi wako halafu anakuangalia kwa jicho la namna hii na hajibu kitu, hajitetei wala haombi msamaha.... wewe utamuelewaje hapo.... anakiri makosa yake? au anakupuuza?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kweli unko ukimnya dawa.....wakati mwengine....
   
 7. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  uuuuwih hili jicho hili kha!yani atazidi kuspark hizo hasira manake najua hapo ananidharauje ?thubutuuu!
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Asabaya
  kama hivi...., ndio mpango mzima..... hapo hata tunda haliliki mwanawane
   
 9. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  hapo full kujuta kwanini nimeolewa au nimeoa kisirani huyu............
   
 10. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Psychological punishment is always more than a punishment
   
 11. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Ambao hamjaoa,haya ni mambo ya kawaida sana,tena ni madogo,kuna makubwa zaidi ya haya!Ndoa bwana!
   
 12. T

  Tetra JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Silence is the true friend that never betrays.
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  asante mtambuzi....
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Bora umejua, uache tabia yako ya nagging kwa mwenzio......

  [​IMG]
   
 15. data

  data JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,739
  Likes Received: 6,512
  Trophy Points: 280

  kweli mkuu.!? Always?

  I dont thnk so.
   
 16. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Halina ubishi kuwa kukaa kimya (hata kama wewe si mkimya) ukiwa na hasira ni dawa. Lakini tusisahau kuwa kuongea pia ni hulka. Hivyo ni ngumu sana kwa muongeaji kukaa kimya.

  Na kwa experience yangu mtu mwongeaji akikaa kimya utatamani aongee maana huo mnuno utakuwa una speak louder than voice.

  Kukaa kimya ni one thing...ku pretend as if nothing happened ni another; mimi mume wangu anapenda niongee nikiwa na kitu maana nikikaa kimya namuona anavyohangaika...nyumba inakuwa ndogo...anaweza asile hata kula. Utasikia 'mbona umenuna?; Mi: 'Kwani nimenuna?' Yeye sasa ndio anaanza kununa mara mbili yangu, kisa mimi nimemnunia; inabidi nianze kujiongelesha mwenyewe.
   
 17. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi umenishtua na Heading yako.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  asante sana Mtambuzi, ngoja nii-save hii thread for fyucha use!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Haya makutano yenu yatakua wapi? kama ni pale Maryland Bar nitakuwepo kushuhudia Mtambuzi anavyo timua vumbi kama jamaa. :lol:

  :focus: Sometimes yes, it helps a lot.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  kuna wakati unatamani mtu aongee au akae kimya. sasa jinsi ya kuupangilia huo muda ni ngumu.

  mimi napenda kuongea yaishe, siku nikikaa kimya mjamaa anahisi natunga sheria au bado nakisirani.
   
Loading...