Kama hukubaliani na aliyekuteua, suluhisho ni kujiuzulu

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,066
Kwa wale wa nafasi za uteule hasa za ngazi za juu ikiwa mtizamo wako ni kinyume cha mtizamo wa aliyekuteua unachotakiwa ni kujiuzulu.

Ikiwa wewe ni Daktari na aliyekuteua anaamini kuwa matibabu ya surua ni udongo wa kichunguu hutakiwi kukubaliana naye bali kiungwana unatakiwa ujiuzulu.

Ukiendelea kukaa hapo maana yake wewe ni MNAFIKI.
 
Sio rahisi kihivyo. Huku kwetu ukiteuliwa siku ya kuapishwa unaenda na ndugu zako wanakuvalisha mataji halafu uje kuachia madaraka kisa unatofautiana na msimamo wa bosi wako, ukirudi nyumbani watakuchapa viboko.
 
Kwa wale wa nafasi za uteule hasa za ngazi za juu ikiwa mtizamo wako ni kinyume cha mtizamo wa aliyekuteua unachotakiwa ni kujiuzulu.
Unajiuzulu ule wapi? acha hiyo watakufuata na kukubambikia uhujumu uchumi , madawa ya kulevya usipate dhamana. In that situation unafanyaje?
 
Kwa wale wa nafasi za uteule hasa za ngazi za juu ikiwa mtizamo wako ni kinyume cha mtizamo wa aliyekuteua unachotakiwa ni kujiuzulu.
Ikiwa wewe ni Daktari na aliyekuteua anaamini kuwa matibabu ya surua ni udongo wa kichunguu hutakiwi kukubaliana naye bali kiungwana unatakiwa ujiuzulu.Ukiendelea kukaa hapo maana yake wewe ni MNAFIKI.
... na kujiuzulu sio tu unalinda heshima yako bali unakuwa umemsadia mteuzi na taifa kwa jumla - kwanza message sent atafikiria mara mbili why? Itambadili mawazo na atafanya kwa busara zaidi. Vinginevyo, wewe ni mzigo sio kwa mteuzi tu bali kwa taifa na mbele za Mungu maana unachoangalia ni nafasi na tumbo lako tu.
 
Tatzo ni njaaa tu ila kiukweli watu wengi tu ilitakiwa wawe wamejiuzulu kuanzia waziri wa afya
 
Kwa wale wa nafasi za uteule hasa za ngazi za juu ikiwa mtizamo wako ni kinyume cha mtizamo wa aliyekuteua unachotakiwa ni kujiuzulu.

Ikiwa wewe ni Daktari na aliyekuteua anaamini kuwa matibabu ya surua ni udongo wa kichunguu hutakiwi kukubaliana naye bali kiungwana unatakiwa ujiuzulu.

Ukiendelea kukaa hapo maana yake wewe ni MNAFIKI.
akijiuzulu tu hiyo nafasi nipatieni
 
Tatizo ni njaa mkubwa. Kwa nchi ambazo masuala ya utawala wa sheria bado hayajakaa sawa, ukiacha kwa stahili hiyo, unaweza dhibitiwa usiweze fanya hata biashara ya genge
 
Back
Top Bottom