Kama hujuma za kampuni ya NAS Dar Airco zingelikomeshwa mapema na watendaji kuwajibika vilivyo, yaliyotokea yasingeendelea kutokea

Nadir Naimuor

Member
Sep 13, 2020
9
45
KAMA HUJUMA ZA KAMPUNI YA NAS DAR AIRCO ZINGELIKOMESHWA MAPEMA NA WATENDAJI KUEAJIBIKA YALIYO TOKEA YASINGEENDELEA KUTOKEA

Salam wakuu,

Naandika haya kama mzalendo ninayetamani kuona mabadiliko Makubwa kwenye Viwanja Vyetu vya ndege Tanzania.

Leo nitazungumzia Kampuni Tata ya NAS-DAR Airco limited. Nitaendelea kuchambua Kampuni na Mtu mmoja mmoja anayerudisha nyuma maendeleo ya Nchi yetu. Nitajikita sana sana kwenye Viwanja vya Ndege vya Dar, Mwanza Kilimanjaro na Dodoma.

Mwaka 2015 Kampuni ya NAS (National Aviation Services, Al Farwaniyah, Kuwait) kutoka Kuwait ilikuja Tanzania na kuingia ubia wa kibiashara na kampuni ya Mwanza handling ya Mwanza kwenye masuala ya uhudumiaji wa ndege.

Baada ya mikataba na mambo mengine NAS na Mwanza handling walitengeneza kampuni iliyoitwa NAS-DAR Airco Company na tenda ya kwanza walipata uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere international nakumbuka uzinduzi ulifanyika katika hotel ya Serena.

NAS-DAR Airco iliwaita wafanyakazi kama 49 ambao iliwaajiri tarehe 2016.

Kampuni hiyo ya Nas dar Airco ilipofika airport ya dar es salam na kuanza shughuli zake, walitumia office za AFS(Africa Flight Services) ambayo ni majengo ya kampuni binafsi yalioko gate no 6.

Kampuni ya Nas dar Airco ilianza kuingiza vifaa yaani equipments na uniforms 2016 kati ya mwezi wa 8 mpka wa 11 na kampuni hiyo ilianza kuhudumia ndege ndogo zilizokuwa zikija hapa nchini kwa kushirikiana na kampuni ya Equity Aviation Services. Pia waliweza kutoa baadhi huduma kwenye ndege za ATCL kwa kutoa huduma za Conveyor Belt Tractor kama ATCL wakiwa na mizigo mizito.

Ilipofika mwaka 2017 Nas dar Airco walipata tenda ya kuhudumia %100 ndege za ATCL.

Walipoanza kazi ya kuhudumia ndege za ATCL, kampuni ya Nas dar Airco walikuwa hawana vifaa kamili vya kufanyia kazi kama sabuni vivuta vumbi kwenye mazulia ya ndege aircraft toilet fluid na kadhalika, ikapelekea kampuni ya Nas dar Airco wafanye mpango wa kuiba Material kwenye shirika la ndege la precision air. Hivyo waliwatumia wafanyakazi wao Kukamiliaha huo mpango. Hivyo wakamtuma mafanyakazi wao anayeitwa God N. akaibe material kama aircraft toilet fluid nk, kwenye shirika la ndege la precision air akishirikiana na mfanyakazi wa shirika hilo aitwaye martin.

Material mengi sana yaliibiwa na kampuni ya Nas dar Airco na kuyatumia kwenye huduma zao wanazotoa kwenye ndege wanazo hudumia hii ni hujuma kubwa sana

(1) Ni hujuma kwa aviation

(2) Ni hujuma kwa ndege wanazo hudumia na hasa ndege za ATCL kwa kuwa ni ndege za Serikali ambapo ATCL wanalipa pesa tena ni kodi za watanzania lakini Nas dar Airco wakitoa huduma ya mali ya wizi.

Pia materials hizo zingeweza kuhatarisha hata usalama wa ndege zetu kwa kuwa upatikanaji wake ulikuwa wa kimagendo.

Nas dar Airco hawakuishia hapo waliweka maji kwenye ndege ambayo hayaja chujwa ambapo huwa ni hatari sana kwenye mifumo ipitayo maji kwenye ndege na haikuchukua muda athari zilianza kujitokeza kwenye ndege za atcl Q400 5H-TCD. Ndege hii ilipata hitilafu kwenye mfumo wa mabomba ya kupitishia maji na kupelekea kutoboka sababu ya maji chumvi.

Kampuni ya Nas dar Airco walipoona mifumo ya maji inatengeneza kutu za chumvi chumvi kupitia mfanyakazi wao God, alileta acid kusafisha kutu zile kumbe ndo aliku akiharibu zaidi. Taarifa zilifikishwa mapema kwa uongozi wa ATCL pale airport ila hatua za haraka na za makusudi hazikuchukuliwa. Pia Uongozi wa ATCL ukamtangaza mtu aliyetoa siri badala ya kufanyia kazi tatizo, hivyo wakamuingiza matatani

Mambo yakazidi kuwa mabaya zaidi kwenye ndege za ATCL kutokana na huduma mbovu walizo kuwa wakitoa Nas dar Airco na cha kushangaza zaidi Nas dar Airco walihudimia ndege za flydubai, RwandAir na ATCL kwa wakati huo lakini uharibifu ulifanywa kwenye ndege za ATCL pekee. Inamaanisha kulikuwa na hujuma za makusudi kwa shirika la ndege la ATCL.

Nas hawakuwa wakihujumu ndege pekee walihujumu mpaka mapato ya ATCL kwa watumishi wake kuiba access yaani pesa zinazolipiwa mizigo iliyozidi Uzito ambazo zimekubalika abiria kusafiri nazo free.

Huu wizi baadhi ya watumishi wa ATCL walishirikiana na wafanyakazi wa Nas dar Airco kufanya hujuma hizo na taarifa zilifika ATCL na wizi wenyewe unafanyikaje wakaambiwa.

Nas dar Airco waliitoboa ndege yetu kubwa Boeing 787 na taarifa za utoboaji huo wakauficha nadhani walikuwa na lengo lao Mungu akasaidia hiyo damage ilionekana mapema na hatua za kuanza kusaka waliofanya hujuma hiyo wapatikane ndipo vyombo vya usalama kwa kushirikiana na wasamaria wema wakamamata watumishi (2) wa Nas dar Airco (1) anaitwa mohd rashid (2) ni Brando baada ya kufanyiwa mahojiano kwa siku mbili vyombo vya usalama walikamata tena watumishi (2) wa Nas dar Airco kubwa la maadui Godfrey ngwenya na mwingine anaitwa Oscar.

Kama hatua zingechukuliwa mapema mengi yasingetokea. Nas dar Airco wamefanya hujuma nyingi sana ila walikuwa wakilindwa na baadhi ya maofisa wetu waliopewa dhamana kusimamia mambo mbali mbali.

Nas dar Airco mbali ya kuhujumu ndege zetu meneja wake aitwae Miguel sierra walikuwa akiingiza wageni kutoka nje ya nchi na kuingia eneo la airport na hawakuwa na vibali vya kufanya kazi taarifa zilifika mpaka kwa kamishina wa kazi wakati huo na pia kwa Naibu waziri wa kazi na watuhumiwa walikamatwa kwenye hotel moja wakiwafanyia watu usaili na bado hiyo issue ikapotelea hewani.

Hapa jambo kubwa ambalo linazungumziwa ni hawa wafanyakazi kuingizwa nchini na kampuni Nas dar Airco kinyemela na kuingia eneo la airport ambapo ni sehemu nyeti sana.

Nas dar Airco wanatumia TIN namba ya Mwanza ground mpaka sasa. TIN namba hiyo ilitolewa na TRA mwaka 2000 mwezi wa Tisa (9) tarehe 13 wakapewa Mwanza ground, cha kushangaza ni TIN namba hiyo hivi sasa inasomeka jina la Nas dar Airco badala ya mwanza ground handling.

Nas dar Airco waliingia mikataba na TAA wafanye ukarabati wa jengo la Warehouse wapangishwe kwenye jengo hilo, cha kushangaza baada ya ukarabati mkubwa kufanyika haikuchukuwa muda mrefu sana Nas dar Airco wakalihama jengo hilo na kurudi kwenye jengo la AFS. Hapa wataalam wa mambo wachunguze kiasi cha fedha zililizotumika kukarabati jengo hilo na kwanini Nas dar Airco walihama ambapo wao ndo waliingia mikataba na TAA kuligharamia?

ATCL iliwatwanga faini Nas dar Airco kwa uharibifu wa ndege za ATCL na baada ya mambo kuwa hadharani sana ndipo ATCL wakaamua kuvunja mikataba yote na Nas dar Airco.

Watumishi wa kampuni Nas dar Airco kupitia kwa meneja wake Miguel alikuwa akiingiza wafanyakazi kutoka Kuwait na kufanya kazi airport bila vibali na vyomba vya usalama waliwashika na uhamiaji kuwaondoa kwa PI cha kushangaza waliingia tena kupitia Kilimanjaro kwa pesa walizokuwa wakimwaga

Baada ya ATCL kuvunja Mkataba, Nas dar Airco wakaanza kutimua wafanyakazi tena wengine bila kufuata sheria. Taarifa zilikishwa kwa kamishina wa kazi na Waziri wa kazi ila hakuna hatua zilizochukuliwa kuwasiaidia Waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni hii ya Kuwait. Hii inaonesha jinsi Watendaji wasivyomsaidia rais.

Nas dar Airco wamekuwa wakitumia vitambulisho vya wafanyakazi ambao wamewafuta kazi huwapigia simu na kuwapa vitambulisho ambavyo vipo office ya HR, watu hao kuingia airport ndani na kufanya kazi kama vibarua kwa vitambulisho vya watu walioacha kazi. Ni jambo la hatari sana hili na taarifa kitambo zilipelekwa panapo husika Nas dar Airco wanatumia sana udhaifu wa baadhi ya watanzania wenzetu waliopewa dhamana kufanya wanachotaka

ATCL imeibiwa sana sana na wafanyakazi wa Nas dar Airco wakishirikiana na wafanyakazi wa ATCL tena wengine wanatolewa taarifa na kukamatwa na kuwekwa ndani ila hatua madhubuti hazichukuliwi. ATCL imegeuka shamba la bibi.

Pia kuna hujuma nyingi sana airport ya dar es salam kama;

(1) Usafirishaiji wa abiria kinyume cha sheria

(2)Wizi uliokithiri

(3) utoroshaji wa nyara za Serekali. Kuna haja ya Serekali kufanya kazi ya ziada pale airport ili kumsaidia rais wetu mhe John Joseph Magufuli na shirika la ndege la ATCL

Nas dar Airco walitumia baadhi ya watanzania wenzetu kufanya mambo ya hovyo kama Ngalapi kuhujumu

ATCL. Naamin vyombo vya Usalama vitafanyia kazi kwani wote wanafahamika wanaoihujumu ATCL kiasi kwamba haipati faida.

Kwa hizi l hujuma za kutoboa ndege za ATCL, ilipaswa ATCL kupitia SEREKALI wawaamrishe Nas dar Airco warudishe fedha zote walizolipwa kwenye huduma ya toilet service na portable water kwa kuwa walikuwa wakihujumu nchi.

Inaendelea
 
mkara mshamba

Member
Jan 15, 2020
65
125
Hii imekaa kaaje Mkuu? Endelea
Ndugu yangu, madudu ya nchi hii ukiyachokonoa yate utakufa kwa mawazo, na unaweze ukaitwa msaliti ama unatumiwa mabeberu. Uzalendo wa nchi hii ni kuona na kunyamaza ama kuunga mkono. Shauri yako mm simo.
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,667
2,000
Nas dar Airco hawakuishia hapo waliweka maji kwenye ndege ambayo hayaja chujwa ambapo huwa ni hatari sana kwenye mifumo ipitayo maji kwenye ndege na haikuchukua muda athari zilianza kujitokeza kwenye ndege za atcl Q400 5H-TCD. Ndege hii ilipata hitilafu kwenye mfumo wa mabomba ya kupitishia maji na kupelekea kutoboka sababu ya maji chumvi.

Niliwahi kusikia kuwa ndege huengenezwa kwa material iziyopata kutu na hasa aliminium, sasa hizi za kwetu kwanini wametumia chuma?
 
Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,152
2,000
Mbongo kwa wizi tu yani hatari. Nakumbuka wafanyakazi wa shoprite supermarket walivyo kuwa wanaiba halafu wakicheleweshewa mshahara wanalalamika. Unakuta wafanyakazi wanaita ndugu zao kufanya shopping wakifika kaunta hawalipi
 
Jiwe katuingiza chaka ndie wakulaumiwa
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,563
2,000
Wacha waibe tu na wakiweza waibe na hizo Ndege zote ,zime tutesa sana na zita endelea kututesa sana kwa Kodi zetu kutumika kulipia Hasara inayopatikana kutokana na Mfumo mmbovu wa hili Shirika la Ndege.Kuanzia alie zinunua mpaka mfagizi Mungu anawaona.
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,667
2,000
Mbongo kwa wizi tu yani hatari. Nakumbuka wafanyakazi wa shoprite supermarket walivyo kuwa wanaiba halafu wakicheleweshewa mshahara wanalalamika. Unakuta wafanyakazi wanaita ndugu zao kufanya shopping wakifika kaunta hawalipi

Na kamera nazo zinashirikiana nao haziwaoni
 
Nadir Naimuor

Member
Sep 13, 2020
9
45
Uzalendo kwa nchi yako uko wa aina nyingi ila kwa makala hii inayo ihusu kampuni ya Nas dar Airco ni maalum kabisa itakayo fichua madudu ambayo wanaohusika au serekal iyashughulikie ipasavyo na iyone kwenye vita hii ya kujenga uchumi tunatakiwa kusimama sawasawa
 
Nadir Naimuor

Member
Sep 13, 2020
9
45
Naamini kila anaehusika upande wa serekal watachukuwa hatua stahiki kabisa nchi hujengwa na wananchi husika lakini pia sio kila mgeni au makampuni ya kigeni huja nchini kwa nia njema watanzania tuondoe zile kasumba zetu jambo linalohusu maendeleo ya nchi yetu tuwe macho nalo mambo ya siasa na itikadi zetu tuweke pembeni kwenye mambo ya kitaifa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom