Kama hujayapitia haya maisha, kubali umekosa mengi

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,072
18,258
Utotoni tumefanya ujinga mwingi sana kwa raha zetu.. na mambo mengi tuliyoyafanya yalikua hatarishi sana sijui tumefikaje ukubwani bado wazima.
FB_IMG_1558167320412.jpeg
FB_IMG_1558167323104.jpeg
FB_IMG_1558167329157.jpeg
FB_IMG_1558167331875.jpeg
FB_IMG_1558167334540.jpeg
FB_IMG_1558167337676.jpeg
FB_IMG_1558167340290.jpeg
FB_IMG_1558167343509.jpeg
FB_IMG_1558167353253.jpeg
 
Hii cha mtoto, sisi tulikuwa tunachukua tairi la lori au trekta unaingia hapo katikati unajikunja then wenzio wanakusukuma! Siku ingine wanakusukuma wanapoteza muelekeo wanakuacha upambane na hali yako!
View attachment 1101131
Utotoni kuna ujinga mwingi sana.. na mambo mengi tuliyafanya ni hatarishi sana sijui tumefikaje ukubwani bado wazima.
 
Hii cha mtoto, sisi tulikuwa tunachukua tairi la lori au trekta unaingia hapo katikati unajikunja then wenzio wanakusukuma! Siku ingine wanakusukuma wanapoteza muelekeo wanakuacha upambane na hali yako!
View attachment 1101131
Sitasahau tairi lilipoenda kugonga ubabuni mean oneten iliyokuwa speed wakati naviringishwa kwenye tairi
 
Dah enzi hizo hadi msosi unapotezea kisa michezo.

Ukirudi home mama ananongwa balaa.
Mama yangu ilikuwa ukimiss lunch anakuwekea na share yako ya jion.
Salama yako ule chakula chote, ukibakiza shughuli unayo. Sasa uwe ulikula kwa watu mchana...hakika hata ujitahidi vipi huwezi maliza
RIP mummy. Amenisaidia sana kunilea ktk maadali mema
 
Duh wewe ulikuwa na bahati sana, sisi ulikuwa unaambiwa UTAKULA MIGUU YAKO
 
Siku hizi mambo yamekuwa mengi. Watoto hawawezi kukutana hivyo. Siku hizi motto anatoka shule za Kiingereza saa 11 ana home work atakutana na wenzie saa ngapi? Halafu pia siku hizi kuna stori za watoto kutekwa, kuuawa na kuondolewa viungo, hivyo watu wanalinda watoto wao
 
Sasa hivi nimejiuliza starehe ya kuzungurushwa na lile gurudumu ni nini hata sina jibu!
Nakumbuka niligongwa na baiskeli hadi kuzimia. Nakuja kuzinduka niko home wanajiandaa kunipeleka zahanati.
Nilikuwa naendesha gari ya vigaloni vya bati barabarani. Nikawa nahamahama upande wa barabara mara kulia mara kushoto hamadi paa.
Suti yangu yote ilikuwa damu tupu
 
Kweli mama ako amefanya makubwa..
Dah enzi hizo hadi msosi unapotezea kisa michezo.

Ukirudi home mama ananongwa balaa.
Mama yangu ilikuwa ukimiss lunch anakuwekea na share yako ya jion.
Salama yako ule chakula chote, ukibakiza shughuli unayo. Sasa uwe ulikula kwa watu mchana...hakika hata ujitahidi vipi huwezi maliza
RIP mummy. Amenisaidia sana kunilea ktk maadali mema
 
Nakumbuka niligongwa na baiskeli hadi kuzimia. Nakuja kuzinduka niko home wanajiandaa kunipeleka zahanati.
Nilikuwa naendesha gari ya vigaloni vya bati barabarani. Nikawa nahamahama upande wa barabara mara kulia mara kushoto hamadi paa.
Suti yangu yote ilikuwa damu tupu
Pole sana
 
Hatari sana asee, kuna ile ya kuwinda ndege na manati. Sasa sisi tukawa tukimaliza kuwinda ndege tunaanza kujificha ile kama kombolela ukitoa tu kichwa au mwili unapewa jiwe la maana la manati. Sitasahau siku Rafiki yangu aliponibutua manati ya jicho, nilikaa ndani mwezi mzima bila kuonana na mwanga na makofi juu ya bimkubwa.
 
Kweli mama ako amefanya makubwa..
Kuna siku alinikuta niko juu ya mti nimekalia tawi likinesanesa. Sina hofu kuwa linaweza katika nami nikaumia.
Akaanza kunibembeleza nishuke taratibu huku akinisubiria shinani.
Thubutu yake. Nikaruka juu kwa juu hadi upande wa pili. Ikabidi acheke tu baada ya kuona niko salama na kuniambia alikuwa ananivizia.

Utoto raha sana
 
Hatari sana asee, kuna ile ya kuwinda ndege na manati. Sasa sisi tukawa tukimaliza kuwinda ndege tunaanza kujificha ile kama kombolela ukitoa tu kichwa au mwili unapewa jiwa la maana la manati. Sitasahau siku Rafiki yangu aliponibutua manati ya jicho, nilikaa ndani mwezi mzima bila kuonana na mwanga na makofi juu ya bimkubwa.
Duuu, nyie mlikuwa hatari.
Nimecheka peke yangu kwa sauti hadi majirani watakuwa wamesikia
 
Similar Discussions

24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom