Kama hujawahi tumia hii Kimbo, basi wewe ni kizazi cha akina Lulu

bila shaka ww ni mchaga manake mlikuwa mnayapata ya magendo kupitia taveta. ila cowboy umeyasahau pamoja na super ghee. enzi hizo tulivaa na ndala za sonex, na chachacha.wengi tuliviita mwisho saa sita. shule tulikwenda na kidumu na ufagio na begi lilikuwa spoti spoti. vitabu hasa vya kiswahili vilikuwa na hadithi kama "brown ashika tama",na somo la uraia liliitwa siasa, na alikuwa siku nyerere anakuja lazima tujipange barabarani kumpokea huku nyimbo kama "tunaimani na nyerere", alama za chama ca mapinduzi jembe na nyundo" yapo mengi ya kukumbuka sana siku hizi watoto wa umri wa akina lulu hawana hizo.

na chupi tulikuwa tunavaa za v.i.p
 
Enzi zile maduka ya RTC na USHIRIKA.

Kweli mkuu,

RTCs zilikuwa safi sana kama zisingevamiwa na wezi....

Ila mameneja wa maduka ya ushirika ya vijiji walikuwa watu wa kutisha sana...Ukishindwa kuelewana naye basi wewe sahau mgawao wa kila kitu...kuanzia chumvi, sukari, vitenge na hata vitambaa vya kaniki!!

Kuna mmoja kijijini kwetu alikuwa anatembea na wake za watu kama vile hana akili timamu!!

Babu DC!!
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Ee bwana eh. hiyo ndiyo kimbo orijino enzi za East African Industries. siku hizi EAI imekufa na Unilever ndo inatengeneza Kimbo.
Enzi hizo pia palikuwa na Cowboy halafu huku kwetu Supa Ghee




Super gheeeee ! Enzi zetu boarding,unapewa makopo kadhaa kila mwezi. Mkifunga shule unarudi nayo yaliosalia homu kijijini !
 
Super gheeeee ! Enzi zetu boarding,unapewa makopo kadhaa kila mwezi. Mkifunga shule unarudi nayo yaliosalia homu kijijini !

Jamani kuuliza si ujinga. Hapo kwenye red, mi mwanzisha mada sidhani hata kama nshaitumia hii. Ni nini hii? Na inasomwaje?
 
Dah! Enzi za KNCU-Moshi, NMC na Mengineyo. Nakumbuka boarding schools mafuta ya RAYS ndo yalikuwa yameshika hatam, kwa matumizi mbali mbali yakiwamo kijipaka, kupiga masta, KY na kadhalika.
 
mafuta ya shanti, ashers, yu, rays yalikuwa yananukia balaa.
kuna kipindi fulani wahujumu uchumi walikamatwa wakiwa wamelimbikiza mali. kukawa na kipindi cha redio cha mikingamo!!
tulitumia sana mafuta ya kupikia ya Rajani.
maisha yalikuwa mazuri jamani, hakuna dvd wala game boys, movie tapes za kihindi siku moja moja...tukirudi shule tunacheza kombolela au michezo ambayo ilikuwa trendy
 
Wanajamii leo nimekutana na threads nyingine zikanikumbusha mbali sana,kama hii, nilipokuwa primary school.Ila sijaona kama kuna mtu ametaja mafuta yaliyokuwa yananukia kwa wiki nzima ukijipaka YOLANDA na yale mashati ya 80s JULIANA yenye picha ya Eagle(TAI)mgongoni.hivi AYU ipo mbona siioni? GEISHA ya jana bwana...ghafla nikaiacha nchi hii, sijui nitakumbuka nini tena, nitumieni vya kizazi hiki.

Enzi hizo kwa watangazaji maarufu wa Redio Tanzania Dar Es Salaam (RTD) kama vile Abdallah Mlawa, Jacob Tesha nafikiri ..yes Tido Muhando pia.
 
Jamani Tido si alikuwepo, hata Juma Nkamia. Kuna mwingine kwa sasa ni "Mwenda Zake" nimemsahau kidogo. Uzee tabu kwelikweli.
 
Bia iliyokuwa inatamba ukanda wote wa Afrika Mashariki ilikuwa ni Pilsner (Bia Imara Kama Simba)ikifuatiwa na Safari (1977 hadi katikati ya miaka ya 90)

Note: Mimi si mnywaji ila napenda kumbukumbu.
 
Back
Top Bottom