Kama hujawahi tumia hii Kimbo, basi wewe ni kizazi cha akina Lulu

bila shaka ww ni mchaga manake mlikuwa mnayapata ya magendo kupitia taveta. ila cowboy umeyasahau pamoja na super ghee. enzi hizo tulivaa na ndala za sonex, na chachacha.wengi tuliviita mwisho saa sita. shule tulikwenda na kidumu na ufagio na begi lilikuwa spoti spoti. vitabu hasa vya kiswahili vilikuwa na hadithi kama "brown ashika tama",na somo la uraia liliitwa siasa, na alikuwa siku nyerere anakuja lazima tujipange barabarani kumpokea huku nyimbo kama "tunaimani na nyerere", alama za chama ca mapinduzi jembe na nyundo" yapo mengi ya kukumbuka sana siku hizi watoto wa umri wa akina lulu hawana hizo.
 
Vile vitabu enzi zile vikisomeka sana leo hii ni nadra kuviona : Robinson Crusoe, Sinbad wa Baghdad, Alfu Lela U lela au Siku Alfu na Moja, Hadithi za Kikwetu, Safari za Gulliver, Kisiwa Cha Hazina n.k. Majina ya characters ktk vitabu maarufu, tuliyatumia kama majina ya utani: Bulicheka, Wagagagigikoko,Gagula, Inkoskazi, Umslopogazi, Abunuwas n.k leo hii siyasikii majina haya.
 
KICHWA KIKIUMA

large_222089.jpg
 
kitu kimbo...kipindi tlikuwa tuna tumia sana ma boarding,kimbo unayeyusha unakaangia vitunguu na dagaa mzee afu ikipoa unarudisha kwenye kopo lake lilee la kilombili au mojaa,kitu cha kokoto[makande}au mboga ya serekali[maragwee]ya skul ukichukua una changanya mzee bonge la maungo,mob yenu ikiwa nayo nyie mko juu ndo machecki bobuu......usisahau na kitu cha reiziiiiiiiiiiiiii sabuni kuku au mbuni asee
 
mkuu umenikumbusha mbali sana,hako ka kimbo kadogo kule kwetu rorya wakina mama walikabatiza jina la (CHUORA OCHAYA) yaani mume wangu anipendi,angekuwa ananipenda angeninunulia kimbo ya kopo sio kalatasi.
 
Vile vitabu enzi zile vikisomeka sana leo hii ni nadra kuviona : Robinson Crusoe, Sinbad wa Baghdad, Alfu Lela U lela au Siku Alfu na Moja, Hadithi za Kikwetu, Safari za Gulliver, Kisiwa Cha Hazina n.k. Majina ya characters ktk vitabu maarufu, tuliyatumia kama majina ya utani: Bulicheka, Wagagagigikoko,Gagula, Inkoskazi, Umslopogazi, Abunuwas n.k leo hii siyasikii majina haya.

umekumbuka sinbad he sailor, hadithi za mfale sin sin jamani tumetoka mbali sana. Enzi zile husikii habari za watoto kubakana michezo ilikuwa ni kombolela, kuruka kamba kuogelea tikri(esta esta) kukimbia na kubemea tena local bembea tunazifunga kenye mti tu. mchezo wa nage tena ya udongo au ya vijiti ndo usiseme. wadada na wakaka tulikuwaa na upendo usio wa kufanya mambo ya watu wakubwa. hakika tulipendeza sana. sijui tufanyeje.
 
Back
Top Bottom