Kama hujawahi kusoma hiki kisa; wacha nikusimulie!

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
1,153
1,359
Biblia ina visi vingi sana vingine vinasisimua na vingine vinavyoogofya sana. Kisa hiki cha Yacob ni mojawapo ya visa vinavyosisimua. Yaani kama ingekuwa movie ni zile muvi za Hollywood. Movie la kutisha.

Kama humjui Yakobo, ngoja nikuambie Yakobo ni nani. Yakobo ni mjukuu wa Ibrahim. Baba yake alikuwa anaitwa Isaka na mama yake aliitwa Rebeka. Yakobo alizaliwa pacha. Yeye akiwa Doto na pacha wake alikuwa Esau. Yeye ndie baba wa Taifa la Israel.

Yakobo alikuwa mjanja mjanja sana. Akiwa kijana alimrubini ndugu yake Esau akajitwalia nafasi ya kuwa mrithi kwa supu. Jamaa njaa ilimpiga akauza urithi wake kwa supu. Njaa mbaya asikuambie mtu. Lakini hili baadae lilimcost sana Yakobo.

Wakati wa Yakobo kuoa ukafika. Baba yake akamwambia, mwanangu mimi sitaki uoe mke kutoka miongoni mwa hawa wakanaani. Hebu nenda kwa mjomba wako Laban umuoe mmojwapo wa watoto wake. Laban alikuwa kaka yake Rebeka. Basi Yakobo akakubali. Akaondoka kwenda kwa mjomba ake.

Yakobo alikaa mwenzi mmoja kwa mjomba ake. Mjomba akamuita akamwambia, "Sitaki unitumikie bure. Sema unataka mshahara gani." Aisee, Yakobo akaona mambo Si ndio haya. Akamjibu " Mjomba, mimi nitakufanyia kazi miaka saba hafu nimuowe Rahel" Rahel alikuwa mtoto mdogo wa Laban. Hafu alikuwa mzuri sana. Mjomba ake akamkubalia

Basi Yakobo akajituma, akapiga kazi. Usiku na mchana ili apate mke. Chezea mke wewe. Miaka saba ikaisha. Yakobo akamfuata mjombaake akamwambia, "Uncle, nipe mke wangu, muda tuliokubaliana umekwisha ". Sasa kwa tamaduni yao ilikuwa lazima mkubwa aolewe kwanza. Mjomba akampiga kitendo akamletea binti yake mkubwa akiwa amefunikwa. Yakobo kwenda room akakutanana na Lea. Akalaani kinoma. Mjomba umenifanyania nini.

Yakobo hakuwa na issue zaidi, baada ya wiki mjomba wake akampa Rahel. Jamaa alikuwa anampenda sana Rahel. Akamtumki mjomba ake miaka saba tena mingine. Baada ya miaka saba kuisha akamuowa jumla jumla Rahel. Wake zake wote wakamzalia jumla ya watoto kumi na mbili ambao ndio makabila kumi na mbili ya Israeli!

Hivi huku kwetu bado mabinanu wanaowana?
Hafu hivi bado unaweza kumfanyia mtu kazi miaka saba ili uowe mtoto wake? Mimi siwezi!
 
Cousin!!!!!! Anaolewa tu sina hakika kama vinasaba vya mabinamu ni sawa labda wajuvi walete msaada.
 
Lisa kizuri ila kulingana na umri wa kuishi katika Zama hizi ningumu Sana kukaa miaka Saba kisa mwanamke

Ila sishangai maana wamasai bado wana haka kataratibu hasa "malugunjai"
 
Kama hajaadhibiwa kuna fundisho tena hapo?
Yakobo aliadhibiwa. Na Yesu alipokuja alitufia dhambi zetu baada ya hapo tulipaswa tuishi katika maisha ya utauwa, lakini kwa sababu tunakosa kila siku maana yake tunafanya dhambi
 
Wapi kaadhibiwa?

Yesu akufie dhambi zako wakati yeye mwenyewe alikuwa anamlilia Mungu amuondoshee hicho kikombe? Fikiri.
Nimeanza kuingia na shaka kama biblia unaijua. Yakobo amefanya kazi kwa mjomba ake zaidi ya 23,(ambayo ilikuwa ni adhabu). Yesu alikuwa na mamlaka na uwezo, lakini alisema bali mapenzi yako yatimizwe. Mapenzi gani- kufa msalabani kwa ajili ya wokovu. Na ndio maana biblia inasema watamtazama yule waliyemchoma mkuki.......
 
Sisi Waislam tunawaheshimu sana Manabii na Mitume wa Mungu

Hatutaki dhahaka wala longolongo

Hakuna Mtume aliekuwa na sifa ya Uongo

wala hakuna Mtume aliekuwa Mzinzi

Wala hakuna Mtume aliekuwa mnywaji Pombe

Walikuwa ni watu wema mbele ya jamii iwazunguukayo
 
Sababu kuu ya Yakobo kwenda kwa mjomba wake sio kuoa bali ni kumkimbia ndugu yake Esau ambaye alitaka kumfanya kitu mbaya baada ya kuchukua ukubwa wake na baraka zake.
Kuoa ni minor motive.
 
Nimeanza kuingia na shaka kama biblia unaijua. Yakobo amefanya kazi kwa mjomba ake zaidi ya 23,(ambayo ilikuwa ni adhabu). Yesu alikuwa na mamlaka na uwezo, lakini alisema bali mapenzi yako yatimizwe. Mapenzi gani- kufa msalabani kwa ajili ya wokovu. Na ndio maana biblia inasema watamtazama yule waliyemchoma mkuki.......
Kufanya kazi ni adhabu? we punguani kweli kweli.

Una maana Mungu hakumuondeshea kikombe chake? Kwa maana hiyo Mungu hakuyakubali maombi ya Yesu?

"KUFA" msalabani ni laana kwa mujibu wa biblia. Au hulifahamu hilo?

Hivi hiyo biblia mnaisoma au mnafata ya kuambiwa?
 
Back
Top Bottom